Nikutahadharishe tu kuwa sio mara zote dona ni nzuri, hasa nchi zetu za kitropiki. Uki-google kidogo tu utaona kuwa zaidi ya 80% ya mahindi yaliyopo sokoni yamekuwa contaminated na fungi ambao hutoa sumu zinazoitwa mycotoxins. Sumu hizi hususani zile za aflatoxins hazina rangi wala harufu, lakini zina madhara makubwa sana hasa kusababisha saratani ya ini. Ingawa madhara ya papo kwa hapo sio mengi (mfano walipokufa watu zaidi ya 150 Kenya mwaka 2004), madhara ya muda mrefu ndio ndio makubwa na hatari.
Zaidi ya kansa ya ini, sumu hizi husababisha kudumaa (kwa watoto), na upungufu wa kinga za mwili unakopelekea mhusika kupata maambukizo ya magonjwa kama malaria, kuharisha, typhoid, mafua na mengine mara kwa mara. Kwa wamama wajawazito kunakuwa na hatari ya kujifungua watoto wenye ulemavu au kuharibika kabisa kwa mimba.
Kwa bahati mbaya, fungi humea zaidi kwenye kiini na ganda la nje la mbegu ya mahindi, hivyo kuwaweka watu wanaokula chakula kinachotokana na mahindi ambayo hayajakobolewa katika hatari kubwa zaidi. Hapo ndipo linapokuwepo tatizo kwa kula dona, kwani imethibitishwa (huko Benin, Kenya na kwingine), kuwa kuosha na kukoboa mahindi kunaweza kupunguza hadi kiasi cha 60% ya mycotoxins zilizopo...
Pamoja na faida ya kuwa na protini na fibre kwenye dona, hasara ya kuwepo kwa mycotoxins inafanya wataalamu washauri watu wale sembe zaidi na kupata protini, vitamini na fibres kwenye vyakula vingine kama maharage, kunde na mboga za majani...
cc
MziziMkavu Matola miss neddy Joseph