Kigoma Region Tanzania
JF-Expert Member
- May 25, 2021
- 230
- 611
Unapikwa kwa mhogo pekee?Huu ni ugali usioharibika hata ukikaa mwezi mmoja, Ugali huu unaitwa Rowe hapa kwetu Kigoma. Unatengenezwa kutokana na muhogo, Masharti yake usihifadhiwe kwenye jokofu ama sahani. Unaandaliwa kwa siku 4
Daaaah you made my day asee nimecheka mno!Hizo siku 4 unakua upo tu jikoni?
una mzungumziaje mwendazake!Tuendelee kuombea amani ya nchi yetu, nchi yetu ina tofauti kubwa sana na nchi nyingi.
Nchi majirani zetu na nchi nyingi zina mila lakini mila zetu kama watanzania ni tofauti na mila.zao,tunajuana makabila
Unatengenezwa kutokana na muhogo pekee, mihogo hiyo hutwangwa kwenye kinu na kuwa mfano wa unga, kisha ndio mchakato rasmi wa kuuwandaa ugali wa Rowe unaanza.Unapikwa kwa mhogo pekee?
Hapana, mchakato upo namna hii...Hizo siku 4 unakua upo tu jikoni?
Ni kweli nduguMaprofesa wa Tanzania badala ya kushindana kuja na njia mbali mbali za kurahisisha maisha yetu wamejazana kwenye siasa huko wanapiga porojo tu.
Ona sasa Ugali tu unapikwa Kwa siku saba.
Kule Kwa wazungu wangetafuta mashine ya kupika Kwa masaa machache tu,
Elimu ya kukaririshana madesa haina tija.
Hapana mwezi haufiki kwa kushiba, bali ukiula ugali huo unakuwa na nguvu sana na unaweza chukua muda mrefu bila ya kula chochote kitu, ni ugali uliotumika kwenye safari ndefu kutoka Kigoma hadi Dar es salaam kwa njia ya treni au kutoka Kigoma hadi Zambia kwa njia ya Meli.Nasikia ukila huo ugali bc umeshiba mwezi mmoja.
Ahsante ndugu, lakini unakosea sana. Ugali huo asili yake ni Kigoma na wala sio nchi hizo zenye machafuko, ispokuwa soko kuu liko kwenye nchi hizo za vita. Tunatengeneza kisha tunakwenda kuwauzia wakati wa machafuko. Lakini asili yake haswa huo ugali ni hapa kwetu Tanzani mkoani Kigoma.Tuendelee kuombea amani ya nchi yetu, nchi yetu ina tofauti kubwa sana na nchi nyingi.
Nchi majirani zetu na nchi nyingi zina mila lakini mila zetu kama watanzania ni tofauti na mila.zao,tunajuana makabila tunheshimiana tunataniana tunaoleana
Nchi nyingi zina dini lakini jinsi watu wenye imani tofauti wanavyokaa kwa upendo, kuvumiliana, kuheshimiana kuoleana Tanzania ni tofauti kbisa kiistoria na kijamii kuhusu imani na mataifa mengi hata kule dini hizo zilipotoka. Ukiona mtu anaanzisha chokochoko za kidini au kikabila ujue hana asili ya Tanzania ama ana backup ya watu ama taasisi kutoka nje yenye lengo la kuharibu umoja wetu.
HUU UGALI wa LOYA una asili ya nchi zilizowahi kupigana civil war na umewafanya waweze kupona kufa njaa misituni kwa kuwa unadumu muda mrefu
Sisi watanzania mbinu hizo hatuna kwa sababu tumezaliwa kwenye amani na tunakulia kwenye amani. Tuheshimu tunu zetu za amani ili kuepuka matumizi ya vyakula kama hivi. MUNGU IBARIKI TANZANIA
Nimewahi kula huu ugali kwenye kijiji kinaitwa Mzenze. Ukila kwa nyama ya mbuzi ya kuchoma safi sanaHuu ni ugali usioharibika hata ukikaa mwezi mmoja, Ugali huu unaitwa Rowe hapa kwetu Kigoma.
Unatengenezwa kutokana na muhogo, Masharti yake usihifadhiwe kwenye jokofu ama sahani. Unaandaliwa kwa siku 4 mpaka 7.
Ugali wa Rowe baada ya kusongwa unahifadhiwa kwenye majani maalum ya mgomba, unaliwa kwa mboga ama bila mboga, unaweza kusafiri nao popote kwenye begi. Ni chakula cha asili cha watu wa Kigoma hasa kabila la Waha na wamanyema.
Ugali huu ni biashara inayopata umaarufu mkubwa siku hadi siku, magharibi mwa Tanzania na nchi za Rwanda, Burundi na Congo.
View attachment 1831816
View attachment 1831820
Muwape na kayoga.πππHuu ni ugali usioharibika hata ukikaa mwezi mmoja, Ugali huu unaitwa Rowe hapa kwetu Kigoma.
Unatengenezwa kutokana na muhogo, Masharti yake usihifadhiwe kwenye jokofu ama sahani. Unaandaliwa kwa siku 4 mpaka 7.
Ugali wa Rowe baada ya kusongwa unahifadhiwa kwenye majani maalum ya mgomba, unaliwa kwa mboga ama bila mboga, unaweza kusafiri nao popote kwenye begi. Ni chakula cha asili cha watu wa Kigoma hasa kabila la Waha na wamanyema.
Ugali huu ni biashara inayopata umaarufu mkubwa siku hadi siku, magharibi mwa Tanzania na nchi za Rwanda, Burundi na Congo.
View attachment 1831816
View attachment 1831820
Hapana, ugali huu hauwekewi chumvi bali una ladha yake ya asili ambapo hukufanya wewe mlaji uweze kuula bila hata mboga, na pia unaweza kuukata kata kwa vipande mfano wa beskuti kama picha hiiKwahio huu ni kama biscuits / cookies; preservation ni ukavu au wanaweka chumvi pia
Huwa kuna biscuit fulani za jeshi ngumu kama mbao, ila zinashibisha
Ndio, unaweza kuula kwa nyama ya kuchoma, au kwa samaki wa kuchoma au kwa dagaa wa bichi wa Kigoma (Masembe na Nyamnyam) au hata bila mboga unalika.Nimewahi kula huu ugali kwenye kijiji kinaitwa Mzenze. Ukila kwa nyama ya mbuzi ya kuchoma safi sana.