Kigoma Region Tanzania
JF-Expert Member
- May 25, 2021
- 230
- 611
Huu ni ugali usioharibika hata ukikaa mwezi mmoja, Ugali huu unaitwa Rowe hapa kwetu Kigoma.
Unatengenezwa kutokana na muhogo, Masharti yake usihifadhiwe kwenye jokofu ama sahani. Unaandaliwa kwa siku 4 mpaka 7.
Ugali wa Rowe baada ya kusongwa unahifadhiwa kwenye majani maalum ya mgomba, unaliwa kwa mboga ama bila mboga, unaweza kusafiri nao popote kwenye begi. Ni chakula cha asili cha watu wa Kigoma hasa kabila la Waha na wamanyema.
Ugali huu ni biashara inayopata umaarufu mkubwa siku hadi siku, magharibi mwa Tanzania na nchi za Rwanda, Burundi na Congo.