Uganda imepiga marufuku michezo ya kamari na Kampuni za michezo hiyo hazitapewa tena kibali

good move and Tanzania should move in that way
 
Siku magufuli aliyozungumza na wachezaji wa timu taifa ikulu waziri mwakyembe aliweka wazi mkakati wa serikali kuanzisha kampuni ya michezo ya kubahatisha mbele ya Rais wa jamhuri ya muungano.

Na wamepiga marufuku kamari ila matangazo ya kamari yanaendelea kwenye TV station za nchi yao.
 
Na hapa Tanzania napo mamlaka zisitishe michezo hii. Kusema kweli inachosha na sasa wameiweka katika vyombo vya habari. Yaani ukifungulia redio au luninga mambo ni hayo tu. Tunawafundisha nini watoto wadogo?. Zamani kamari zilichezwa kwenye makasino.

Hali ikiendelea hivi tutakuja kujuta sana baadae

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ikipigwa marufuku hapa vijana wengi watabaki mabachela
 
Raisi wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni ameiagiza serikali yake kutokutoa leseni mpya na kutoendeleza leseni za uendeshaji kwa kampuni za kubashiri (kamari) katika michezo.
Waziri wa mambo ya fedha bwana David Bahati amethibitisha hili huku akisema chanzo ni mchango hasi wa michezo ya kamari hasa kwa vijana ambao badala ya kufanya kazi kwa bidii wamekua wakibashiri na kutegemea kupata hela kwa uraisi.

Michezo ya kubashiri ni maarufu sana nchini Uganda ikikadiriwa kuwa zaidi ya asilimia 70 ya waganda wenye umri chini ya miaka 30 wanajihusisha na kamari, hii pia Imechangiwa na makampuni ya kubahatisha mtandaoni (online betting) ambayo kwa sasa Uganda yanakadiriwa kuwa zaidi ya 400 yaliyopo ndani na nje ya Uganda, haya yamewezesha watu wengi zaidi kubet huku wakiendelea na shughuli zao kama vile za maofisini.

Uganda's Yoweri Museveni 'bans' sports betting - Daily Nation

Tanzania tunasubiri nini ? Ukizingatia makampuni haya mengi ni ya nje yanakuja tu na kuvuna hela kiurahisi huku wakipumbaza vijana wetu kwamba unahitaji ela kidogo tu na kubet ili upate nyingi zaidi.

Big up Uganda hakuna uzuri wa Kamari si Duniani wala Peponi.




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serikali ya Uganda imepiga marufuku michezo ya kubashiri maarufu kama betting kutokana na lundo kubwa la vijana nchini humo kujikita katika michezo hiyo huku wakishindwa kujishughulisha na kazi rasmi.

Kwa kuanzia, serikali imekataza utoaji wa vibali vipya kwa makampuni mapya ya betting, na yale makampuni ambayo leseni zao zimeisha, hawatapata vibali vipya kwa mwaka huu 2019.

My take:

Ni wakati muafaka kwa serikali yetu kulitazama pia suala hili la michezo ya kubahatisha kwa jicho la umakini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…