wambagusta
JF-Expert Member
- Nov 28, 2014
- 2,825
- 2,292
Sarut
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mbona Tanzania tunapiga marufu viroba lakin wao mbona hawatuigi,Serikali ya Uganda imepiga marufuku michezo ya kubashiri maarufu kama betting kutokana na lundo kubwa la vijana nchini humo kujikita katika michezo hiyo huku wakishindwa kujishughulisha na kazi rasmi.
Kwa kuanzia, serikali imekataza utoaji wa vibali vipya kwa makampuni mapya ya betting, na yale makampuni ambayo leseni zao zimeisha, hawatapata vibali vipya kwa mwaka huu 2019.
My take:
Ni wakati muafaka kwa serikali yetu kulitazama pia suala hili la michezo ya kubahatisha kwa jicho la umakini.
Naona kaisikia sasa hivi BBC, Tena kabla ya taarifa kamili! yeye kaileta hapa,
wakati habari ipo hapa tangia mchana
Uganda yapiga marufuku michezo ya ku beti - JamiiForums
Mambo mazuri hayahitaji haraka actually hii taarifa niliiona toka mchana nikaona si vyema nikatulia nakuleta kitu.Huyu jamaa kaja mwendo kasi nikajua anaufafanuzi
Yote fyekelea mbali pamoja na tatu sijui uzushi vile.
Hatimaye Rais wa Uganda Mwanamume ' Mwamba wa Mbarara ' au ' Mwamba wa Kinyankole ' Yoweri Kaguta Museveni amefuta rasmi na kuzuia kabisa michezo yote ya Kubahatisha ( Betting ) nchini humo kwa kusema kwamba imesababisha Waganda wengi wawe Wavivu na Kuirudisha nchi nyuma Kimaendeleo kwakuwa hawajitumi katika Kuwajibika na Kuijenga nchi hiyo.
Haya na wale Marais ' Watoto ' wengine igeni hili upesi ili nchi zetu nazo zipige hatua haraka.
Nawasilisha.
Kama hawafanyi kazi pesa ya kubetia wanapata wapi? Hii ni sawa na kusema watu hawafanyi kazi wanakunywa pombe tu. Je, hizo pombe wanagawa bure?!
Hivi kweli kubeti kunazuia watu wasifanye kazi? UjingaHatimaye Rais wa Uganda Mwanamume ' Mwamba wa Mbarara ' au ' Mwamba wa Kinyankole ' Yoweri Kaguta Museveni amefuta rasmi na kuzuia kabisa michezo yote ya Kubahatisha ( Betting ) nchini humo kwa kusema kwamba imesababisha Waganda wengi wawe Wavivu na Kuirudisha nchi nyuma Kimaendeleo kwakuwa hawajitumi katika Kuwajibika na Kuijenga nchi hiyo.
Haya na wale Marais ' Watoto ' wengine igeni hili upesi ili nchi zetu nazo zipige hatua haraka.
Nawasilisha.
Hahaha wakifanya tz italeta minong'ono maana ndio maisha ya watu hayo.
Ila kuna tatizo kubwa sana la watu kuwa addcted na betting
Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa bongo hii....nadhani mapato yatapungua kwani 80% ya watu waliopo mjini wanabet....hivyo kufungia itakuwa ni kinyume na mikakati tuliyojiwekea ya ukusanyaji wa mapato hasa kodi.
Sent using Jamii Forums mobile app