Uganda imepiga marufuku michezo ya kamari na Kampuni za michezo hiyo hazitapewa tena kibali

Uganda imepiga marufuku michezo ya kamari na Kampuni za michezo hiyo hazitapewa tena kibali

Hivi hili nalo linahitaji Kubisha kuwa tokea ujio wa ' Betting ' hapa nchini hata ' Ufanisi ' katika Maofisi mengi umepungua kwakuwa asilimia kubwa ya Wafanyakazi akili zao wameziweka katika kuwaza au kwenda ' Kubeti ' huku wengine hadi wakifikia hatua hadi ya Kudanganya Ofisini Kwao kuwa ' wanaumwa ' ili asiende Kazini na aende ' Kukesha ' katika Vibanda vya Kubeti? Utakuwa ni ' Mpumbavu ' wa Kimataifa.
Vp kugegedana nako sio addicted kwa watu wengi maana wapo wanao waza kugegedana wakiwa ofisini na kiasi cha kipato chao wana kielekeza huko

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ofisi ngapi za Siku hizi zinaruhusu Wafanyakazi wake kuwa ' online ' muda wote? Kumbuka kuna Ofisi zingine sasa hivi zimeweka Sheria kwamba zikimfuma tu Mfanyakazi wake ' anabeti ' hasa muda ule wa Kazi basi na Ajira yake nayo ndiyo itakomea / itaishia hapo hapo. Acha ubishi / bambi Watu wengi hasa Wafanyakazi huwa wanakuwa huru ' Kubeti ' wakiwa nje ya maeneo yao ya Kazini japo kuna wale ' Watukutu ' fulani ambao wanaweza hata ' Kubeti ' mbele ya ' Bosi ' wake.
Kumbe unazungumzia waajiriwa!!!?? Wengine ndo waajiri wenyewe (tumejiajiri)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna nchi yoyote ile Kubwa duniani imeendelea kwa Kodi za Kubeti? Kuna Watu huwa mnanilazimisha niwe ' nawadharau ' kila Uchao hapa Jamvini / Jukwaani. Jifunze Kujenga Hoja tafadhali.
Tanzania inajiendesha kwa kodi za kubet 18% inachukua kwa mshindi mfano jamaa aliyekula m90 unajua serikali imekwapua sh ngapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndo mimi nashangaa, nimeona hadi madaktari wanabeti sasa utasemaje watu hawafanyi kazi

Hao Madaktari ' wanabeti ' Siku nzima? Bado unataka niendelee tu ' Kukudharau ' kwa huu Utetezi wako wa Kipuuzi?
 
Kubet kumeharibu akili za watu wengi kazi hawafanyi wanashinda kwenye mashine kubet tu
 
Ikiondoka Biko watu watafanya kazi, maana sasahivi watu hawafanyi kazi kila siku kutegemea bahati nasibu ya Biko

Ni wenye ' Akili ' za Kutukuka wachache ndiyo watakuelewa hili jambo zuri uliloliandika hapa ila ' Mapopoma ' wengi hawatakuelewa na Watakupinga kwa hii ' Hoja ' yako. Na isiondolewe tu hiyo BIKO na ' Hoja ' yangu siyo hii michezo ya Bahati Nasibu iondolewe kabisa bali napenda Mamlaka husika zije tu na utaratibu fulani ambao hautaathiri ' Utendaji ' wa Watanzania katika maeneo yao ya Uwajibikaji. Michezo hii ya ' Kubeti ' imeharibu mno Kizazi na Ufanisi maeneo mengi na hili halihitaji Ubishi / Bambi.
 
Kwenda zako, mlipiga marufuku watu kucheza pool table na kunywa pombe asbh what did you achieve? Vitu vingine ujinga tu mnafanya

Unaposema sijui tulipiga marufuku na vitu vingine tunafanya ni Ujinga umeambiwa GENTAMYCINE ni Rais Dkt. Magufuli au ' unawashwawashwa ' tu? Halafu ' logically ' tu ' achievement ' ya Maamuzi fulani siyo lazima uyaone au uyashuhudie Wewe ' directly ' bali wengine wanaweza wakayashuhudia ndiyo maana ikawa ni Jamii na Jamii haipo tu hapo ambapo upo na unaishi. Kuna Watu hadi mnanifanya nijiulize huko Vyuo Vikuu mlienda Kusomea nini kama bado hata tu Ujengaji wenu wa ' Hoja ' ni wa chini hivi?
 
kwa hili nakubaliana na mhe. Museveni , taifa haliwezi kujengwa na vijana wasiojibiidisha kufanya kazi na kutegemea kamari na michezo ya bahati nasibu kama ajira.

Serikali ya Tanzania inabidi ichukue hatua haraka kuwatoa vijana katika addiction hii ya kamari, ipige marufuku kabisa vijana kujihusisha na kamari.

Kama haitawezekana , serikali kupitia ofisi za wakuu wa wilaya iandae utaratibu wa kutengeneza vitambulisho kuwasajili vijana wanaotaka kucheza kamari au bahati nasibu na kijana atakayesajiliwa awe na kazi nyingine kama sifa ya kupewa kibali cha kucheza.

Njia nyingine kama suluhisho , kamari na bahati nasibu zote zichezwe kupitia huduma za simu kama tatu mzuka na biko. Hii itasaidia kuona flow ya pesa ambayo kijana anaitumia kwenye kamari na hivyo serikali kupitia TCRA kudhibiti pesa hiyo. serikali iweke sheria kuwa kwa wiki mtu yeyote anatakiwa kutumia 1000/ au 2000/ tu kwa michezo ya kubahatisha na si zaidi ya hapo.

greybakuza na Timm Wu Siku zingine jitahidi Kufikiri Kisomi kama huyu na acheni Kujidhalilisha kwa kutokujua Kufikiri vyema.
 
Kubeti ni kucheza kamari, watanzania tumeingia mtegoni na kamari. Vijana siku hizi hawafanyi kazi wamekalia kucheza kamari tu, sio vijana hata watu wazima wasiojitambua wako busy na mikeka kweli waafrika tunapaswa tutawaliwe tena ili tupate maendeleo!

greybakuza na Timm Wu mnajisikiaje kuona Watu ' Werevu ' kuwazidi wakitoa ' Hoja ' zenye mashiko na mantiki kama hii?
 
Hatimaye Rais wa Uganda Mwanamume ' Mwamba wa Mbarara ' au ' Mwamba wa Kinyankole ' Yoweri Kaguta Museveni amefuta rasmi na kuzuia kabisa michezo yote ya Kubahatisha ( Betting ) nchini humo kwa kusema kwamba imesababisha Waganda wengi wawe Wavivu na Kuirudisha nchi nyuma Kimaendeleo kwakuwa hawajitumi katika Kuwajibika na Kuijenga nchi hiyo.

Haya na wale Marais ' Watoto ' wengine igeni hili upesi ili nchi zetu nazo zipige hatua haraka.

Nawasilisha.
HAPA TANZANIA WAFUTE BIKO, TATU MZUKA, VIBANDA VYA KUBET. WAACHE KUBET MTANDAONI
 
Safi sana hii kitu inaniuzi sana ni janga la taifa

Sent using Jamii Forums mobile app

Rais Dkt. Magufuli nae ' akiliiga ' hili basi GENTAMYCINE nitakuwa ni mwenye furaha Kubwa sana kwani Afrika ya sasa haiwezi Kuendelea na Kukimbizana na waliotuacha au kutukimbia ' Kimaendeleo ' ulimwenguni endapo tutakuwa na ' All the time Betting Generation '. Upuuzi huu huwezi Kuukuta China, Korea, Japan, Israel, Singapore na Malaysia ila kwa Tanzania ndiyo umeshaota ' Mizizi ' tayari.

Halafu bado kuna ' Mijitu ' inatetea kabisa hadi ' Mishipa ' ya Shingo inawatoka!

Cc: greybakuza , Timm Wu
 
GENTAMYCINE Mbona unatumia nguvu kubwa unapojibu maoni ya wadau kwenye uzi wako? Jitahidi kuwavumilia, usitumie lugha kali kuwakosoa, ndiyo maoni yao ati. Binafsi sijawahi kuingia chumba chochote cha kubeti.
 
GENTAMYCINE Mbona unatumia nguvu kubwa unapojibu maoni ya wadau kwenye uzi wako? Jitahidi kuwavumilia, usitumie lugha kali kuwakosoa, ndiyo maoni yao ati. Binafsi sijawahi kuingia chumba chochote cha kubeti.

Sasa kama ni ' Mangumbaru na Mapopoma ' niwavumilie tu? Siwezi Mkuu nitatiririka na kuserereka nao tu hadi nao wawe ' Great Thinkers ' pia.
 
Back
Top Bottom