PostGE2025 Uganda inatuhumiwa kuingiza wanajeshi siku ya Uchaguzi, Jaji wa Uganda ataweza kuichunguza nchi yake?

PostGE2025 Uganda inatuhumiwa kuingiza wanajeshi siku ya Uchaguzi, Jaji wa Uganda ataweza kuichunguza nchi yake?

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Ile ziara ya Museveni juzi kati na uteuzi wa jaji jana yake ni script iliyonyooka sana kulinda utawala wa kikanda.

Ikigundulika wanajeshi wa Uganda walihusika, ripoti it asema tu walikuja kama watalii wa amani na siyo wavamizi, haya mambo yako wazi sana.
Mkuu hivi walivaa kabisa sare zao za UPDF? Basi tujitafakari kua autuwezi kulinda mipaka yetu.Ondoa CCM
 
Inasemekana hao wanajeshi wa uganda waliwaambia wa jwtz kuwa wakileta za kuleta watalifyeka jeshi lote la jw na wakanywea kama kama jani linavyonyauka kwenye moto.Watanganyika hatuna jeshi kabisa.kazi kula mshahara wa bure.Ipo siku tutaenda kambini kwao kuwacharaza viboko kabisa.
Kumbe mkuu,kwahiyo walipitia mpaka hupi?
 
Samia ameunda tume huku akimteua Jaji Barishaki Cheborian wa Uganda kuwa mmoja wa tume hiyo kuchunguza chanzo cha vurugu.

Soma PostGE2025 - Rais Samia: Tumeamua kuwashirikisha wenzetu kutoka Uganda na Namibia kupata muono mpana. Tume inakwenda kutafuta nani walichochea, waliotoa fedha

Zipo taarifa za wanajeshi wa Uganda kuingia Tanzania siku ya uchaguzi na kuhusika kuua Watanzania ili kuulinda utawala.

Je, Tume ikigundua kuwa ni kweli wanajeshi wa Uganda waliingia Tanzania siku ya uchaguzi huyo jaji anaweza kuwa Neutral?

Pili Uganda haina rekodi nzuri kuhusu haki za binadamu, mpinzani mkuu wa Mseveni Dkt. Besigye yupo kizuizini kwa mashtaka ya uhaini tangu 2024, huyu jaji anayekuja Tanzania kashindwa nini kumshauri Mseveni kumaliza kesi hiyo, je ataweza kuwasuluhisha Watanzania?

Tatu, mwezi Juni Rais wa Namibia, Dkt. Netumbo Nandi-Ndaitwah, alifanya ziara ya siku 3 nchini, juzi Mseveni alikuja kumtembelea Samia, siku moja baadae majaji wa nchi hizo wanateuliwa kuongoza tume inafikirisha na kutia mashaka nia hasa lengo la hii tume.
Museveni alikuja Tanzania juzi tu! Huenda waliyazungumza, Rais wa Angola alikuja Tanzania na ni juzi wa Tanzania alienda Angola, wakazungumza, siku si siku uteuzi wa watu wasio ndani ya serikali yetu unafanywa! Na kupewa mwongozo wa yapi ya kuyachunguza!
Kenya yalitokea na wameyamaliza na hata waliokuwemo kulipwa kisa! Sisi huku eti maridhiano huku wanaoridhiana wanachunguzwa! Nataka Sitaki.
 
Mkuu hivi walivaa kabisa sare zao za UPDF? Basi tujitafakari kua autuwezi kulinda mipaka yetu.Ondoa CCM
Mkuu, mimi nimetoa tu mtazamo wangu kwamba ikigundulika......

Kuhusu suala la wao kama walivaa au hawakuvaa, sifahamu chochote.
 
Screenshot_20251217-065939~2.png
 
Back
Top Bottom