Samia ameunda tume huku akimteua Jaji Barishaki Cheborian wa Uganda kuwa mmoja wa tume hiyo kuchunguza chanzo cha vurugu.
Soma PostGE2025 - Rais Samia: Tumeamua kuwashirikisha wenzetu kutoka Uganda na Namibia kupata muono mpana. Tume inakwenda kutafuta nani walichochea, waliotoa fedha
Zipo taarifa za wanajeshi wa Uganda kuingia Tanzania siku ya uchaguzi na kuhusika kuua Watanzania ili kuulinda utawala.
Je, Tume ikigundua kuwa ni kweli wanajeshi wa Uganda waliingia Tanzania siku ya uchaguzi huyo jaji anaweza kuwa Neutral?
Pili Uganda haina rekodi nzuri kuhusu haki za binadamu, mpinzani mkuu wa Mseveni Dkt. Besigye yupo kizuizini kwa mashtaka ya uhaini tangu 2024, huyu jaji anayekuja Tanzania kashindwa nini kumshauri Mseveni kumaliza kesi hiyo, je ataweza kuwasuluhisha Watanzania?
Tatu, mwezi Juni Rais wa Namibia, Dkt. Netumbo Nandi-Ndaitwah, alifanya ziara ya siku 3 nchini, juzi Mseveni alikuja kumtembelea Samia, siku moja baadae majaji wa nchi hizo wanateuliwa kuongoza tume inafikirisha na kutia mashaka nia hasa lengo la hii tume.