Kwavile mnajidanganya Watanzania hawajui Kiingereza, bila kufahamu tofauti ya Watanzania na Wakenya, ni shobo kwenye lugha ya Kiingereza!!
Hivi kabisa unaamini mtu amesoma History, Kiswahili, and English kwa miaka 4, kisha akaenda A-Level akasoma History, Kiswahili, English (HKL),au (HGL) kwa miaka 2!
Baada ya hapo, anaenda chuo akasoma ama Linguistic, BA, n.k, na kwa madogo wa siku hizi, wapo wengi sana waliosoma English Medium kuanzia shule ya msingi; lakini bado unaamini wote hao hawajui Kiingereza?!
Unachekesha!! Unachekesha kwa sababu usichofahamu ni kwamba, wakati nyie mnaonea fahari kuongea Kiingereza hata pasipo na sababu za msingi, Watanzania wengi wanaamini kuongea Kiingereza pasipo na sababu za msingi ni ushamba na ulimbukeni!!
Kwa mfano, ukinikuta nimesimama kwenye kituo cha daladala ukaniongelesha Kiingereza, amini usiamini, ama sitakujibu, na kama nitakujibu, basi nitakujibu kwa Kiswahili!
Nitakujibu kwa hiyo lugha ya kigeni endapo tu utakuwa hufahamu Kiswahili!!
Halafu kingine usichokijua ni kwamba, Watanzania wengi tatizo lao ni kwenye Kiingereza cha kuongea lakini sio cha kuandika!!!
Kwenye kufundisha Kiswahili, Mfundishaji anahitajika kuwa na ufahamu wa kawaida wa lugha ya Kiingereza lakini anatakiwa kuwa na ufahamu wa juu wa Kiswahili, lakini sio ufahamu wa juu wa Kiingereza na ufahamu wa kawaida wa Kiswahili!!