He nailed it. Tatizo la watanzania waliopo kwenye hili jukwaa ni wazalendo wa magufuli na wamemezeshwa propanda za uzalendo usiohitaji kuhoji mambo. Na hili la kushindwa kuhoji au kuwa na respectful dialogue kuhusu mitazamo tofauti pia wamelirithi, ukimuhoji mtu kitu chochote kuhusu serikali hatokujibu ataishia kukutukana au kukukaushia kama hajaona binafsi najisikia vibaya sana sababu vijana wengi wa kitanzania waliopo humu ni wasomi wa vyuo lakini na wao pia wanabehave kama watu ambao hawajawahi kugusa darasa.
Nitakupa mfano, viwango vya ustawi wa nchi unapimwa kwa vitu vingi kama demokrasia, haki za binadamu, uchumi na uwajibikaji sasa katika hivyo watakwambia magufuli amefanya hiki amefanya kile ukimwambia chagua kitu kimoja ambacho upo tayari unaona amefanya vizuri tujadiri anakimbia, sasa hii ni tabia ya kushindwa kujadili inapelekea matusi na ndio vijana wengi wa humu wapo hivyo, kama kuna wazee nimewajumuisha pia.
Magufuli ni kiongozi pekee ambae ametumia propaganda kuliko kiongozi mwingine yoyote katika nchi hii. Watakwambia kikwete na mkapa walikuwa mafisadi hawajafanya kitu ukiwaambia tuwalinganishe na magufuli wanakimbia kifupi ni wabebaji wa kila alichokuwa anasema magufuli.
Nchi hii haijawahi kurudi nyuma tangu ipate uhuru sio kwa miundombinu na wala sio kwa uchumi wa GDP lakini vijana hilo hawajui wanajua wanayomezeshwa kwamba tumepigwa sana lakini hawahoji 1.5 trilioni ilienda wapi hadi CAG akatumbuliwa baada kuliamba bunge kuwajibika.
Sio vibaya kumpenda kiongozi fulani sababu ana mazuri ameyafanya lakini kugeuka kuwa unamwabudu hilo ni tatizo. Nina imani Mama Samia atawashangaza wengi wanaomchukulia poa sasa hivi.