KWELI Uganda walianza kufanya upasuaji kwa ajili ya kujifungua (C-section) kabla ya mwaka 1879

KWELI Uganda walianza kufanya upasuaji kwa ajili ya kujifungua (C-section) kabla ya mwaka 1879

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
Je, hili ni kweli wakuu?

By 1879, Uganda was the only place in the world where C-sections were performed to save both mother and baby. European observers documented this practice, which used local tools, herbal anesthetics & antiseptics.
1772701938198.png
 
Tunachokijua
Kujifungua kwa njia ya upasuaji (Cesarean delivery au C-section) ni utaratibu wa kitabibu unaotumika kumtoa mtoto kwa kufanya chale kwenye tumbo na mfuko wa uzazi wa mama.

Uhalisia wa C-Section kufanyika Uganda

Ufuatiliaji kupitia machapisho na kumbukumbu za kihistoria uebaini kuwa ni kweli Uganda walianza kufanya mchakato huo takribani kabla ya mwaka 1879.

Taarifa zinaeleza kuwa C-Section huko Kahura Uganda ilifanyika kwa kutumia kisu kilichopinda, kilichotengenezwa kwa chuma na chenye mpini wa mbao.

Vifaa hivyo viliundwa na kutumiwa na watu wa Bunyoro kufanya upasuaji wa kumtoa mtoto tumboni uliofanikiwa 1879.

Wasafiri wa karne ya 19 kutoka Ulaya kuja barana Afrika waliripoti matukio ya uzalishwaji kwa njia ya upasuaji kwa Waafrika huku wakitumia mbinu zao za kiasili za kitabibu.

Msafiri wa kiingereza Robert William Felkin alishuhudia upasuaji wa kumtoa mtoto tumboni (caesarean section) ukifanywa na watu wa Uganda mwaka 1879.

Inaelezwa kuwa tabibu huyo alitumia pombe ya ndizi kumlewesha mwanamke huyo kwa kiasi, kisha akasafisha mikono yake pamoja na tumbo la mgonjwa kabla ya upasuaji.

Alifanya chale ya katikati ya tumbo (midline incision) na kutumia njia ya kuchoma kidonda (cautery) ili kupunguza kutokwa na damu nyingi.

Baada ya kumtoa mtoto, alikanda mfuko wa uzazi ili ujikaze, lakini hakuuona haja ya kuushona. Jeraha la tumbo lilifungwa kwa sindano za chuma na kisha kufunikwa kwa dawa ya asili iliyotengenezwa kutoka kwenye mizizi ya mimea.

Felkin anaeleza kuwa mgonjwa alipona vizuri, na jambo lililomfanya alihitimishe kuwa mbinu hiyo ilikuwa imekuzwa vizuri na inaonekana ilitumika kwa muda mrefu.
Back
Top Bottom