Intelligence Justice
JF-Expert Member
- Oct 23, 2020
- 3,840
- 4,414
Wakuu,
Mikoa ifuatayo haikugawanywa kwa kuzingatia Jiografia rafiki kwa uendeshaji wenye ufanisi na tija.
1. Arusha kupata mkoa wa Manyara: ingefaa usianzishwe mkoa wa Manyara badala yake wilaya mbili za Simanjiro na Kiteto ndio zingeunganishwa na mkoa wa Kilimajaro.
2. Mkoa wa Pwani umekaa kama upinde na ngao kwa mkoa wa Dar Es Salaam: miundo mbinu ya mkoa wa Pwani kutoka wilaya moja hadi nyingine ni changamoto kubwa hasa kutoka Kisarawe kwenda Mkuranga, Rufiji, Kibiti, na Mafia ambapo iliyopo ni lazima uchepuke kupitia mkoa wa Dar Es Salaam wilaya ya Ilala na Temeke/Mbagala wakati mawasiliano ya miundo mbinu ya barabara kati ya Kisarawe kwenda Kibaha, Chalinze na Bagamoyo hayana tatizo kubwa ijapokuwa kwa nyakati za masika kutoka Kisarawe kwenda Kibaha ni shida.
Pendekezo nusu ya wilaya za Bagamoyo na Chalinze zigawanywe kwenda Dar Es Salaam na Tanga. Kuanzia Vikindu na Mwandege zihamishiwe wilaya za Kigamboni na Temeke/Mbagala. Mkoa wa Pwani uundwe kwa wilaya za Kisarawe, Mkuranga, Rufiji, Kibiti na Mafia; [Nyongeza au mabadiliko ya majina kwa wilaya kama Kisiju kule Mkuranga na Masaki kule Kisarawe.
3. Mkoa wa Morogoro: Mtandao wa eneo lilivyo una changamoto kubwa hasa kutoka Morogoro kwenda wilaya za Kilombero (Ifakara), Ulanga (Mahenge) na Malinyi ziko mbali sana kutoka makao makuu ya mkoa. Wilaya ya Morogoro vijijini huko Mvuha ambayo haina zaidi ya miaka mitatu tangu ihamishiwe huko, miundombinu bado ni changamoto kubwa sana.
Ni bora Mkoa wa Morogoro ungepunguziwa wilaya za Ulanga na Malinyi ambazo zinaweza kugawanywa katika mikoa ya Iringa na Njombe, huku Morogoro ikibaki na wilaya sita za Kilombero, Morogoro mjini, Morogoro vijijini ibadilishwe jina na kuwa Mvuha, Kilosa, Mvomero na Gairo;
4. Mkoa wa upunguziwe eneo la kaskazini linalopakana na Kigoma kisha iongezewe eneo kutoka mkoa wa Tabora ambao pamoja na Lindi ndio mikoa yenye maeneo makubwa sana kwa sasa.
5. Mikoa ya kanda ya ziwa imegawanywa sana kiasi ambacho inaondoa uhalisia wa jiografia ya pande nne za dunia ambazo wakazi wake wanajitambulisha atokeapo kwa mfano kabila la wasukuma kaskazini wanaita sukuma lakini pia wanaamini ndio kitovu cha uzazi wao hapo Kwimba baada ya kuhamia miaka kadhaa iliyopita kutokea Afrika magharibi kupitia Kongo {Hapa sijapigia chapuo ukabila wa jamii yoyote ila kwa kuzingatia historia zao kama wanavyoelezea]