Intelligence Justice
JF-Expert Member
- Oct 23, 2020
- 3,840
- 4,414
Mkuu,Hii mikoa mara nyingi inagawanywa kwasababu za kisiasa tu, ndio maana inaonekana kuna matatizo katika ugawanyaji wake.
Umeulizwa pale no 4 unamaanisha mkoa gani ? Mbona hujajibu mkuu ?Mkuu,
Changia mawazo yako kwa pamoja na wengine wakubwa wapate ujumbe hata kama hatazingatia lakini historia itayaibua mbeleni kwa faida ya vizazi vijavyo. Ndio maana kuna maeneo huko Katavi tangu Uhuru mbali na Rais kutofika lakini pia hata mkuu wa mkoa, wilaya hawajawahi kumuona!!! Nakumbuka TAL alijaribu kufika huko kwa kutumia helikopita wakati wakati wa kampeni kama sijakosea.
Hivi kumbe mbagala sio dar?Ni kweli mkuu kwa mfano MBAGALA,VIKINDU NA MWANDEGE iwe sehemu ya wilaya ya Kigamboni kwa Jiji la Dar es Salaam yaani kila kituo cha basi watu wa maeneo ya mbagala ni wengi kama dagaa,ukienda mbezi ita watu mbagala ni wengi hatareee ,kariakoo,mwenge,tabata,tandika,posta,balaaa
Mkuu,Hivi kumbe mbagala sio dar?
ndugu yangu, ni rahisi kugawa mkoa kupata mkoa mpya kuliko kuunganisha wilaya kuwa sehemu ya mkoa mwengine, huko ninkushusha hadhi mamlaka ya eneo hilo, ni sawa na jiji kurudi kuwa manispaa, oliskia wapi, hilo kuwezekanaWakuu,
Mikoa ifuatayo haikugawanywa kwa kuzingatia Jiografia rafiki kwa uendeshaji wenye ufanisi na tija.
1. Arusha kupata mkoa wa Manyara: ingefaa usianzishwe mkoa wa Manyara badala yake wilaya mbili za Simanjiro na Kiteto ndio zingeunganishwa na mkoa wa Kilimajaro.
2. Mkoa wa Pwani umekaa kama upinde na ngao kwa mkoa wa Dar Es Salaam: miundo mbinu ya mkoa wa Pwani kutoka wilaya moja hadi nyingine ni changamoto kubwa hasa kutoka Kisarawe kwenda Mkuranga, Rufiji, Kibiti, na Mafia ambapo iliyopo ni lazima uchepuke kupitia mkoa wa Dar Es Salaam wilaya ya Ilala na Temeke/Mbagala wakati mawasiliano ya miundo mbinu ya barabara kati ya Kisarawe kwenda Kibaha, Chalinze na Bagamoyo hayana tatizo kubwa ijapokuwa kwa nyakati za masika kutoka Kisarawe kwenda Kibaha ni shida.
Pendekezo nusu ya wilaya za Bagamoyo na Chalinze zigawanywe kwenda Dar Es Salaam na Tanga. Kuanzia Vikindu na Mwandege zihamishiwe wilaya za Kigamboni na Temeke/Mbagala. Mkoa wa Pwani uundwe kwa wilaya za Kisarawe, Mkuranga, Rufiji, Kibiti na Mafia; [Nyongeza au mabadiliko ya majina kwa wilaya kama Kisiju kule Mkuranga na Masaki kule Kisarawe.
3. Mkoa wa Morogoro: Mtandao wa eneo lilivyo una changamoto kubwa hasa kutoka Morogoro kwenda wilaya za Kilombero (Ifakara), Ulanga (Mahenge) na Malinyi ziko mbali sana kutoka makao makuu ya mkoa. Wilaya ya Morogoro vijijini huko Mvuha ambayo haina zaidi ya miaka mitatu tangu ihamishiwe huko, miundombinu bado ni changamoto kubwa sana.
Ni bora Mkoa wa Morogoro ungepunguziwa wilaya za Ulanga na Malinyi ambazo zinaweza kugawanywa katika mikoa ya Iringa na Njombe, huku Morogoro ikibaki na wilaya sita za Kilombero, Morogoro mjini, Morogoro vijijini ibadilishwe jina na kuwa Mvuha, Kilosa, Mvomero na Gairo;
4. Mkoa wa upunguziwe eneo la kaskazini linalopakana na Kigoma kisha iongezewe eneo kutoka mkoa wa Tabora ambao pamoja na Lindi ndio mikoa yenye maeneo makubwa sana kwa sasa.
5. Mikoa ya kanda ya ziwa imegawanywa sana kiasi ambacho inaondoa uhalisia wa jiografia ya pande nne za dunia ambazo wakazi wake wanajitambulisha atokeapo kwa mfano kabila la wasukuma kaskazini wanaita sukuma lakini pia wanaamini ndio kitovu cha uzazi wao hapo Kwimba baada ya kuhamia miaka kadhaa iliyopita kutokea Afrika magharibi kupitia Kongo {Hapa sijapigia chapuo ukabila wa jamii yoyote ila kwa kuzingatia historia zao kama wanavyoelezea]
ni sababu za kiuchumi, geita ilipokuwa sehemu ya mwanza, uwekezaji mkubwa ulifanywa mwanza mjini kwa faida zilizopatikan geita, wanageita wakaomba wawe mkoaHata mimi sijaonaga sababu ya kuugawa mkoa wa mara na mwanza..zingeendelea kuwa mkoa mmoja tu.
Mkoa wa chato wenye makao makuu yake kijijini chatoBado mkoa mmoja tutazindua kabla ya 2025.
Umezungunza vema sana,Wakuu,
Mikoa ifuatayo haikugawanywa kwa kuzingatia Jiografia rafiki kwa uendeshaji wenye ufanisi na tija.
1. Arusha kupata mkoa wa Manyara: ingefaa usianzishwe mkoa wa Manyara badala yake wilaya mbili za Simanjiro na Kiteto ndio zingeunganishwa na mkoa wa Kilimajaro.
2. Mkoa wa Pwani umekaa kama upinde na ngao kwa mkoa wa Dar Es Salaam: miundo mbinu ya mkoa wa Pwani kutoka wilaya moja hadi nyingine ni changamoto kubwa hasa kutoka Kisarawe kwenda Mkuranga, Rufiji, Kibiti, na Mafia ambapo iliyopo ni lazima uchepuke kupitia mkoa wa Dar Es Salaam wilaya ya Ilala na Temeke/Mbagala wakati mawasiliano ya miundo mbinu ya barabara kati ya Kisarawe kwenda Kibaha, Chalinze na Bagamoyo hayana tatizo kubwa ijapokuwa kwa nyakati za masika kutoka Kisarawe kwenda Kibaha ni shida.
Pendekezo nusu ya wilaya za Bagamoyo na Chalinze zigawanywe kwenda Dar Es Salaam na Tanga. Kuanzia Vikindu na Mwandege zihamishiwe wilaya za Kigamboni na Temeke/Mbagala. Mkoa wa Pwani uundwe kwa wilaya za Kisarawe, Mkuranga, Rufiji, Kibiti na Mafia; [Nyongeza au mabadiliko ya majina kwa wilaya kama Kisiju kule Mkuranga na Masaki kule Kisarawe.
3. Mkoa wa Morogoro: Mtandao wa eneo lilivyo una changamoto kubwa hasa kutoka Morogoro kwenda wilaya za Kilombero (Ifakara), Ulanga (Mahenge) na Malinyi ziko mbali sana kutoka makao makuu ya mkoa. Wilaya ya Morogoro vijijini huko Mvuha ambayo haina zaidi ya miaka mitatu tangu ihamishiwe huko, miundombinu bado ni changamoto kubwa sana.
Ni bora Mkoa wa Morogoro ungepunguziwa wilaya za Ulanga na Malinyi ambazo zinaweza kugawanywa katika mikoa ya Iringa na Njombe, huku Morogoro ikibaki na wilaya sita za Kilombero, Morogoro mjini, Morogoro vijijini ibadilishwe jina na kuwa Mvuha, Kilosa, Mvomero na Gairo;
4. Mkoa wa upunguziwe eneo la kaskazini linalopakana na Kigoma kisha iongezewe eneo kutoka mkoa wa Tabora ambao pamoja na Lindi ndio mikoa yenye maeneo makubwa sana kwa sasa.
5. Mikoa ya kanda ya ziwa imegawanywa sana kiasi ambacho inaondoa uhalisia wa jiografia ya pande nne za dunia ambazo wakazi wake wanajitambulisha atokeapo kwa mfano kabila la wasukuma kaskazini wanaita sukuma lakini pia wanaamini ndio kitovu cha uzazi wao hapo Kwimba baada ya kuhamia miaka kadhaa iliyopita kutokea Afrika magharibi kupitia Kongo {Hapa sijapigia chapuo ukabila wa jamii yoyote ila kwa kuzingatia historia zao kama wanavyoelezea]
Kweli mkuu, halafu wengine wanajitokeza humu kutetea eti ilivyogawanywa ni sahihi kwa sababu watu wa eneo husika ndio waliomba. Kijiografia, kijamii , kiuchumi na kiutawala Simanjiro na sehemu ya Kiteto ipelekwe Kilimanjaro maana ardhi ya Kilimanjaro hasa hasa Arusha chini kule kahe, Kikavu, Kikuletwa, Mijomgweni (Mikocheni), udongo ni wa magadi na jua kali utafikiri uko Dar au Dodoma. Sehemu nyingine ya Kiteto ama ipelekwe wilaya ya Kondoa-Dodoma au wilaya ya Kilindi-Tanga.Umezungunza vema sana,
Mkoa wilaya za Simanjiro na Kiteto zimekuwa na administrative cost kubwa kwa ya kugawa mikoa kwa maslahi yasiyo mapana na yenye tija. Imagine mkurugenzi akiitwa Mkoani anaoita Mkoa wa Kilimanjaro, Arusha ndo anafika mkoani n8 zaidinya Km 400+ kutoka wikayani hadi mkoani, wakati kama ugawaji wenye tija ungefanyika ingepunguza zaidi ya Km 300+ ambapo Simanjiro ingekuwa either Kilimanjaro au Arusha.
Watawala wawe wanafanya maamuzi yenye tija ilinkupunguza cost ambazo fedha zake zingeweza kufanya shughuli zingine za maendeleo.