Ugomvi na ushoga usiwe kigezo cha watoto kukosa mchele wenye virutubisho, tutaonekana majuha

Kuna tatizo gani ukisaidiwa na wewe ukamsaidia aliyekusaidia baadaye, yani wewe unataka kula tu vya watu halafu hutaki vya kwako kuliwa! Hata walevi Bar wanapozungusha round wanategemea na mwenzao azungushe round. Mahusiano yote ya watu wasio ndugu au mke na mume yame base kwenye reciprocity, hiyo ilipaswa kuwa no brainer kwako na wenzako wenye mawazo mgando.
 
Moshi Ushoga umeshika kasi bwashee
Itakuwa uliolewa na mchaga alafu ukaachwa! Unachuki sana na moshi nilini ulifanya utafiti ukagundua hilo!!!
Angalia usijejikuta familia yako inakuwa hivyo unavyosemea wengine...
 
Hili la mchele hapana kwa kweli. Vijana wetu wasijeanza kuwashwa.
 
Nazn tuna mkemia wa Taifa afanyie kazi


Mpenda dezo lazima alipe gharama ya dezo
 
Wachague kaya na watoto wa viongozi wa CCM wawagawie... Tz Haina shida ya chakula... Wapelekee Kenya huko.
 
Nani amekuambia huo mchele haujapimwa??
Shida yenu ni mchele haujapimwa na kufuata taratibu za kuingiza chakula nchini au shida yenu ni mmepewa mchele wa bure na Wamarekani??
 
Nazn tuna mkemia wa Taifa afanyie kazi


Mpenda dezo lazima alipe gharama ya dezo
Umejuaje huo mchele haujapimwa kama mafuta, sukari, ngano, pringles, soda, juice na apple mnavyoagiza kutoka nje??
 
Pendeleeni kupewa misaada itawaponza sana iko siku wanaotoa misaada nao watataka na nyinyi muwalipe fadhila sijuwi mutawalipa kitu gani? Ukizoea kusaidiwa ipo siku itabidi ulipe fadhila je utalipa kitu gani? jiulize halafu upate jibu.
Mimi hata siku moja sipendizwi na misaada. Katu! Kuanzia mimi binafsi kwenye maisha yangu, mpaka kwa nchi yangu. Wanaopenda misaada ni CCM na ubovu wao katika kuongoza ndiyo unafanya tuhitaji misaada. Hivi nchi yetu ilivyo na ardhi kubwa yenye rutuba na hali ya hewa nzuri pamoja na mito na maziwa, ni ya kutegemea misaada? Point yangu ni kuwa kama wewe ni maskini njia pekee ya kukataa misaada ni kufanya kazi kwa bidii ili ujitosheleze. Huwezi kuwa fukara halafu ukaamuru wanaokusaidia wakusaidiaje.
 
Naunga mkono hoja! Binafsi sioni tatizo la kupewa msaada huo! Kama hauna masharti yo yote sioni shida.
Kinachotakiwa TBS au shirika linalohusika na vyakula lichukue sampuli lipime ili kujidhirisha kuwa hauna matatizo ya kiafya kwa walaji.
 
Ni nani aliwaambia wamarekani kuwa watoto wetu wana upungufu wa virutubisho hivyo tuomba msaada wa mchele wenye virutubisho? Mwisho wa siku watoto waanze kunona mikundu huku tukipiga vigelegele kuwa watoto wamenona na wana afya kumbe mikundu yao inafukuta inataka chorongo. Kama unataka peleka guta pale ukachukue kilo zako 400 wapelekee nyumbani kwako!
 
Pendeleeni kupewa misaada itawaponza sana iko siku wanaotoa misaada nao watataka na nyinyi muwalipe fadhila sijuwi mutawalipa kitu gani? Ukizoea kusaidiwa ipo siku itabidi ulipe fadhila je utalipa kitu gani? jiulize halafu upate jibu.
Ukiwa kama taifa huwezi kukosa kitu cha kutoa kwa taifa lingine. Uhusiano wetu na Marekani katika historia kwa muda wote umekuwa wa kulipana fadhili, kuna watu wanaouza dawa za kulevya wanatafutwa na Marekani tumewahi kusaidia kukmatwa kwao, kuna taarifa za intelejensia zenye maslahi kwao Marekani wanapata kutoka vyombo rasmi vya uchunguzi nchini mwetu, sisi ni soko au wateja wakubwa wa bidhaa za Marekani kuanzia computer, softwares, vinywaji, sanaa, silaha, nguo n.k
 
Wamarekani hawahitaji kuambiwa kujua hilo, unafikiri ubalozi wa Marekani mkubwa hivyo na unaolindwa kwa zana za kisasa kwamba Balozi na wafanyakazi wake wako hapo kutoa visa na kuuza sura tu?? Kuna taarifa Wamarekani wanazo hata viongozi wako wengine wakubwa tu hawanazo
 
Ipo hivi...Target hapa ni madini na sio madin tuu....ni madin yanayo hitajika sana sana Duniani...na haya madini yapo mengi sana Dodoma...Nyerere alipokuwa anakomalia makao makuu yawe Dodoma alikuwa anajua....awamu nying zilipita bila mafanikio ya kuwezesha hilo mpaka pale alipo ingia Mh Magufuli....ikulu ikashushwa pale pale pamoja na makaz ya watumishi wa serikali...huku ardhin pakijaa uraniam....hii ni kukomoa kwamba wakitaka kuchimba basi waanze kubomoa ikulu na makaz ya serikali....kitu ambacho ni mtihan kwao....

Hivi umeshajiuliza kwa nn mkakati wa huu mchele umepelekwa dodoma na si mikoa mingine? Hivi ni kweli mchele utoke marekan...mpaka bongo...utoke dar ufike dodoma bila hata serikali kutojua?? Wazir wa kilimo ametolea ufafanuz ni kwamba alikua hana taarifa..???
Mambo ni mengi....kikubwa tuzidi kumuomba Mungu...hii nchi ni ngumu sana sana...ni miaka mitatu sasa tokea atutoke...Mwenyez Mungu amlaze mahala pema peponi..
 
Virutubisho vinaleta na kusababisha saratani...
Hiyo sio zawadi, tatizo humu wengi hatujui operation za grants na loans, mkuu hiyo hela inalipwa na nchi baadae, Tunachezewa vya kutosha
Awali ya yote, tena unakuta hao wakulima wanaodaiwa kutoa hiyo misaada, aidha wamesamehewa mamilioni ya makodi ama wamelipwa ruzuku za mamilioni za kutosha.

Nina wasiwasi pia hiko chakula ni kile kilichokosa masoko kwao wakati wa kipindi cha covid. Kilichopelekea chakula hicho kuwa unfit, kulingana na stamdard zao, kwa maana nyingine hakiuziki Marekani, wamekisafisha(bleach) na kuongeza hivyo virutubisho

Kuna watu humu ukiwasoma, unaelewa ni watu wa aina gani likija suala la kulazimisha mambo. Lugha zao zinaeleweka
Watanzania tuwe makini. Tusikubali tu

Niseme tu hili, hili sio suala la Ushoga au Lah.


Ni suala la kujiheshimu kama nchi.

At some point we must say 'Thank you, but NO thank you.

Serkali ifungashe huo mchele na uupeleke kwa Wasudani, wanakufa njaa. Kama wanavyosema makada kule USA-For real For real.
 
Mchele nimezalisha hapa hakuna soko, kilo sh 800 je kuna haja gani kuletewa mchele na wafanya biashara wa Marekani.

Hivi vimiradi uchwara ndio JPM alikuwa anavilima nyundo
Naomba kg 100
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…