Ugomvi wa P-Square unamvyomnufaisha Diamond Platnumz

Ugomvi wa P-Square unamvyomnufaisha Diamond Platnumz

Daaaaaaaaaaaaaah,

Hivi jamani tuwe wakweli, "HIVI UNAANZAJE KUMCHUKIA HUYU JAMAA"?

Hebu angalia namna anavochangamkia fursa, juzi kati alikwa na ziara Ulaya, kizarizari kakutana na Papa Wemba hakuchelewa hata sekunde akamaliza kazi..!!! Neyo alikuja kibahati kwenye tuzo kule South dogo fasta sana akarusha ndoano nayo bila ajizi ikanasa ulimi wa mkali huyo wa freestyle toka USA.

Anakazi kibao ziko store, kina Fari Ipupa wanapigana vikumbo kutafuta miguu ya dogo iliko wafanye jazi dogo anawapangisha foleni..!!!

Aaaaaah, Wakenya sasa tunawakalisha kwenye sector moja hadi nyingine, Msikilize #Rudeboy psquere anachosema hapo juu "Supporting The king of East Africa" RIP The Great, ungekuwepo hays Manyangau tungekuwa tunayasambaratisha mpaka kwenye Filamu.

Kiukweli dogo anajua, tumsapoti. Dogo ni mali yetu, tujivunie. Ushamba wa kuponda na kutukana umepitwa na wakati ijapokuwa kukosoa si dhambi.

Congratulations Mr Chibu Dangote

BACK TANGANYIKA
 
Hao jamaa hawana ugomvi... Wanajatibu vitu tofauti
 
Mbona ngoma hatuzioni mara p square mara neyo mara swez beat mara jey z lakini hakuna kitu #au kiki za msimu?
 
Mi mpaka sasa ni shabiki wa kiba japo ananiboa kwa upuuzi wa kuchezea kipaji chake..yaani sijui yupoje..hajui kujieleza kwenye inteview hana mikakati inayoeleweka ..unaweza kutetea mziki wake humu kumbe mwenzio yupo jangwani anacheza mpira ..hana hata mpango wa kujisumbua studio..haf siku hizi ana swaga za kibwege bwege yaani aaghh.....watu wakikua ndio wanapata akili lkn yeye ndio anakua kama zezeta...kiba wa macmuga na Cinderella sio huyu kabisa...yaani sasa amebaki yoooo..yooo..yooo..sa ndio nini....aggh ngoja nilale mm
Pole mkuu
 
Ujackia kibakuli anatafuta timu aanze kucheza mpira tena juzi anagojea msimu wa usajili aende majimaji au toto afrika
 
Nimepata kuusikia kidogo, wimbo ni mzuri lakini labda ni masikio yangu utaniprove wrong.. Wimbo wa Nuh Mziwanda ft. Alikiba unafanana baadhi ya vitu na wimbo wa #bado harmonize ft. Diamond in terms of beat n melody sema kuhusu mashairi cna uhakika.. Utanijulisha kama nmekosea
 
ATA MM NILIKISIKIA KIPANDE NA KUNA VITU FLANI VYA KWENYE WIMBO WA BADO VIMEIGWA SASA WACHATUSIKIE NGOMA NZIMA ILA BADOO BADOO KUMFIKIA MOND
 
Ali Kiba yupo bize anashoot na Nuh Mziwanda.
mkuu mimi nilikuwa team Kiba ila ukweli lazima tuukubali dai yuko juu sana ya kiba kwa sasa kwa hiyo kumfananisha kiba na diamond ni kumrudisha nyuma maana level hizi bifu za kitz ameshapita huko tumuombee afike mbali zaidi ya hapo nahitimisha dai na kiba ni vitu vi2 ambavyo havifanani kabisa
 
Back
Top Bottom