Ugoni bila kutenda nimeumia sana

Yaani akutaje tuu bila kosa, au akipita huwa unamtolea machooo
 
Sioni kwa nini uwe na wasiwasi kiasi hicho wakati wewe sio mhusika. Kwani kwenye hiyo salon haujaajiri vijana wa kiume? Huyo mwanamke ametaja tu ili kumwokoa huo mchepuko wake, na mumewe angetaka kukudhuru wewe angekuwa tayari kakuvamia. Au ukute anataka akunase live hivyo kama wewe si mhusika haitatokea hivyo uwe na amani.
 
Ni ngumu kuamini kabsa yaani mwanamke hana mahusiano na wew yeyote Yale eti amekurupushwa ugoni akutaje wew mmmh kuna kitu nyuma ya pazia
 
Pole sana mkuu.
Fanya haraka wahi kwa mwenyekiti wa mtaa jieleze na uende polisi kutoa taarifa.
Issue kama hii inaweza kupelekea wewe kupata matatizo makubwa kama kifo ukipuuzia.
Tafuta hata wazee watu wazima kaa nao waeleze na ingekuwa vizuri kuwe na mazungumzo kati yako wewe,mwenye mke na mkewe pamoja na wazee ili aseme kwanini akutaje na atoe vithibitisho vitakavyoonyesha kama unahusika kwa namna moja au nyingine.
Wanawake tuna matatizo sana kuna mmoja kasababisha mwenzie auwawe na yeye kujeruhiwa vibaya juzi kati tu hapa kwasababu ya fumanizi
 
asante mkuu.
 
Kaka fanya hivi... karipoti kituo cha polisi.... kuhusu hii ishu..
Usiache ukaumia hivi hiv kwa kes ya kusingiziwa... karipoti pia na kwa mwenye kiti wa mtaa
nashukuru kwa ushauri wako.
 
naashukuru.
 
asante kwa ushauri.
 
Hiyo kiukweli ni beef ila cha kufanya mtafute huyo mama akwambie kwanini amekutaja wewe na ingekuwa vzuri mme wake awepo ukiwa unamuhoji
spendi ata kuona sura yake ila nashukuru kwa ushauri wako.
 
we kwanza katoe taarifa polisi tena hapo hapo walipomkamata hapo utajiwekea kinga kwan hawrz kuja kukudhuru physically labda aende kwa sangoma..sasa kuhusu kujikinga na mambo ya sangoma labda ngoja kina mshana wapite huku watakushauri na wao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…