Ugoni bila kutenda nimeumia sana

Ugoni bila kutenda nimeumia sana

Sidhan kama alikusingizia tu from no where jamani hata kama hukuwa ww ulishawah kula mzigo huko nyuma usituchoshe na ww ulishakula mzigo ndio umekamatwa kwa niaba ya wenzio si mbaya maana na ww ni mhusika[emoji3][emoji3]
 
Kama unataka kumaliza bifu hilo ni afadhali lipeleke polisi ili huyo aitwe omba na mumewe awepo athibitishe kama kweli ni wewe kama alivyotamka yeye
 
Habari zenu wana JF,

Kuna jambo ambalo limenitokea jana yaani hadi sasa nina hofu ata chakula hakiliki, ninahitaji ushauri kwenu makaka zangu na madada pia.

Kuna jamaa mmoja anaishi na mke na watoto inavyosemekana juzi usiku saa2 kuamkia jana alitoka kazini hakumkuta mke wake alielekezwa na watoto alikoelekea mama yao, akafuatilia akamkuta kwenye boma la nyumba wakiwa wanafanya mapenzi kwa kuwa ilikua giza hakumjua ni nani aliekuwa na mke wake jamaa katimua mbio.

Akamkamata mke akampiga akimuuliza ulikua na nani baada ya kipigo kuzidi akataja "ni yule mwenye saloon ya kike".

Ndugu zangu nimeumia sana nimetajwa mimi mwanamke simjui hanijui, hajawahi hata kuingia saloon kwangu.

Kiufupi mimi ni kijana miaka 21 nina saloon ya kike kiukweli mama mzima kanifanyia kitendo cha kikatili. Mume wake jana alipelekwa polisi, kinachoniuma kila mtu kitaa ananiambia kuwa mimi walinikosakosa ugoni nikakimbia.

Sina raha kwa kweli nipeni msaada wa mawazo yenu na ushauri nina maswali mengi kichwani kuna nini kati ya mimi na yaye kitaa kizima ameamua kunipa beef na mme wake nilishamkosea nini?

Nashindwa nimalizie wapi asanteni karibu kwa mawazo yenu.
We sema ynapaka rangi kucha za wadada.nyie ni nyokko sana bora alivyokutaja washenzi nyie huwa mnatomasa sana miguu ya wake zetu
 
May be mitandao kwa kufuatlia simu ya huyo mama anaweza kupatikana aliyekuwa na chat naye kw wakati huo. huo ni ushauri tu.
 
Back
Top Bottom