Ugoni bila kutenda nimeumia sana

Ugoni bila kutenda nimeumia sana

Mkuu....
Mimi ukisikia nimesingiziwa issue kama hiyo, basi pigia mstari tu maana hakuna namna tena
 
Duuuhhhh kazi kweli kweli kweli.

Tumeumbwa wengi, kama jambo hujafanya na "Mwenyezi Mungu" mwingi wa Rehema ni shahidi wa Hilo. Wasiwasi wako nini.

Kilicho muhimu jichunguze tabia yako. Ni vizuri kujijengea "TASWIRA" nzuri kwenye jamii ili hata ukisingiziwa jambo basi jamii ikutetee na si wewe ujitetee.
asante
 
Awamu hii kila mtu kachanganyikiwa. Huyo mama anaweza akaitwa serikali za mitaa na bado akakomaa kuwa ni wewe unayemsimamia kama ngongoti.
Na huyo mumewe usiongee nae hawezi kukuamini kwa lolote. Ila ndio mitihani ya maisha.
Na mara nyingi ishu kama hizi huwatokea vijana ambao hamuonekani mkiwa na demu, nyumba za ibada hamuendi. Mpo mpo tu.
Ripoti kwa mjumbe na polisi. Ila kaa chonjo.
 
Dunia ina maajabu ila watanzania tunashangaza.
Pole aisee kuna jamaa yangu naye kasingiziwa na dada mwingine tatizo tu alikosea maana jamaa alisafiri siku moja kabla.
Pole
 
Kwahiyo huna ushahid wowote kwamba muda huo ulikuwa wapi na unafanya nin?
nilikua saloon mkuu shahidi zangu niliokua nikiwasuka ila inasemekana kua alikomaa na kutaja mimi
 
duuuh pole sana mkuu isije ikawa ni mbinu za kibiashara wakufukuzishe mtaa kijanja,INAONEKANA UNAPATA KIPATO KIZURI AU HUYO DADA ALIKUWA ANAKUPENDA TOKA KITAMBO AKAONA BORA AKUTAJE WEWE HATA KIKISANUKA AHAMIE KWAKO.DAAAH ILA BINAMU WABAYA AISEE SASA AKIKUFANYIA KITU MBAYA NA MZIGO HUJALA ITAKUWAJE.

THEN NENDA KAREPORT KITUO CHOCHOTE CHA POLICE WAKUPE ULINZI LIKITOKEA LA KUTOKEA
Huu ndulio ushauri pekee
 
Ondoa hofu hata kama akikufungulia kesi ,, hauna hatia kwa sababu kigezo cha msing kweny ugoni ni kwamba ufumwe na mhusika halfu wawe na mashahid walioshuhudia hiyo kitu lakin kukutaja tu ww haina mantik,,

Tunasema kwamba wenda huyo mwanamke ana kisilan na ww ndo maan akakufanyia hvyo,,, kiukweli hakuna kitu cha kuogopa hapo fanya ishu zako,
 
Habari zenu wana JF,

Kuna jambo ambalo limenitokea jana yaani hadi sasa nina hofu ata chakula hakiliki, ninahitaji ushauri kwenu makaka zangu na madada pia.

Kuna jamaa mmoja anaishi na mke na watoto inavyosemekana juzi usiku saa2 kuamkia jana alitoka kazini hakumkuta mke wake alielekezwa na watoto alikoelekea mama yao, akafuatilia akamkuta kwenye boma la nyumba wakiwa wanafanya mapenzi kwa kuwa ilikua giza hakumjua ni nani aliekuwa na mke wake jamaa katimua mbio.

Akamkamata mke akampiga akimuuliza ulikua na nani baada ya kipigo kuzidi akataja "ni yule mwenye saloon ya kike".

Ndugu zangu nimeumia sana nimetajwa mimi mwanamke simjui hanijui, hajawahi hata kuingia saloon kwangu.

Kiufupi mimi ni kijana miaka 21 nina saloon ya kike kiukweli mama mzima kanifanyia kitendo cha kikatili. Mume wake jana alipelekwa polisi, kinachoniuma kila mtu kitaa ananiambia kuwa mimi walinikosakosa ugoni nikakimbia.

Sina raha kwa kweli nipeni msaada wa mawazo yenu na ushauri nina maswali mengi kichwani kuna nini kati ya mimi na yaye kitaa kizima ameamua kunipa beef na mme wake nilishamkosea nini?

Nashindwa nimalizie wapi asanteni karibu kwa mawazo yenu.
Acha kutuzuga mtu anaanzaje kukusingizia.
 
Siku zote siri ni ya mtu mmoja na duniani hakuna siri kilichopo unamfucha mme/mke lakini watu wanawaoneni, na hiyo picha aliyemuonyesha mgoni wake wala si watoto kuna mtu wa tatu ambaye ndo aliyetoa picha yote,!
 
Back
Top Bottom