Ugoni bila kutenda nimeumia sana

Mkuu....
Mimi ukisikia nimesingiziwa issue kama hiyo, basi pigia mstari tu maana hakuna namna tena
 
asante
 
Awamu hii kila mtu kachanganyikiwa. Huyo mama anaweza akaitwa serikali za mitaa na bado akakomaa kuwa ni wewe unayemsimamia kama ngongoti.
Na huyo mumewe usiongee nae hawezi kukuamini kwa lolote. Ila ndio mitihani ya maisha.
Na mara nyingi ishu kama hizi huwatokea vijana ambao hamuonekani mkiwa na demu, nyumba za ibada hamuendi. Mpo mpo tu.
Ripoti kwa mjumbe na polisi. Ila kaa chonjo.
 
Dunia ina maajabu ila watanzania tunashangaza.
Pole aisee kuna jamaa yangu naye kasingiziwa na dada mwingine tatizo tu alikosea maana jamaa alisafiri siku moja kabla.
Pole
 
Kwahiyo huna ushahid wowote kwamba muda huo ulikuwa wapi na unafanya nin?
nilikua saloon mkuu shahidi zangu niliokua nikiwasuka ila inasemekana kua alikomaa na kutaja mimi
 
nilikua saloon mkuu shahidi zangu niliokua nikiwasuka ila inasemekana kua alikomaa na kutaja mimi
Tuma wazee wakaongee na huyo mmewe ili yasikukute mabaya ukapoteza future yako bure.
 
Huu ndulio ushauri pekee
 
Pole mkuu! Ongea na huyo mwanamke...
 
Ondoa hofu hata kama akikufungulia kesi ,, hauna hatia kwa sababu kigezo cha msing kweny ugoni ni kwamba ufumwe na mhusika halfu wawe na mashahid walioshuhudia hiyo kitu lakin kukutaja tu ww haina mantik,,

Tunasema kwamba wenda huyo mwanamke ana kisilan na ww ndo maan akakufanyia hvyo,,, kiukweli hakuna kitu cha kuogopa hapo fanya ishu zako,
 
Acha kutuzuga mtu anaanzaje kukusingizia.
 
Siku zote siri ni ya mtu mmoja na duniani hakuna siri kilichopo unamfucha mme/mke lakini watu wanawaoneni, na hiyo picha aliyemuonyesha mgoni wake wala si watoto kuna mtu wa tatu ambaye ndo aliyetoa picha yote,!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…