Ugonjwa ninao changamoto ni matumizi ya dawa

Ugonjwa ninao changamoto ni matumizi ya dawa

Dct Active

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2023
Posts
570
Reaction score
443
Habari za muda huu wakuu,

Naandika hapa nikiwa kijana mdogo(me), pre 20 yrs, nikiwa na heshima kubwa kwa wanajukwaa wote hasa wale walio na uelewa wa masuala ya afya.

Kwa siku kadhaa sasa nimekuwa nikiona damu nyekundu ang’avu wakati wa haja kubwa, hasa pale ninapojikamua chooni. Sina maumivu makali wala muwasho, lakini hali hii imenipa wasiwasi mkubwa. Baada ya kufanya utafiti wa awali kwa kusoma baadhi ya mada humu JamiiForum na vyanzo vingine, nimehisi huenda ni dalili za bawasiri ya ndani (internal hemorrhoids).

Sasa, kabla sijachukua hatua yoyote ya kutumia dawa, nilishauriwa na rafiki mmoja(yeye ni daktari) kuhusu Anusol Suppositories, kama njia ya kutuliza tatizo hili kwa hatua za awali.
Hata hivyo, sijaanza kutumia bado. Nimeona ni vyema kuomba maoni na ushauri kutoka kwa wakuu humu kabla ya kufanya uamuzi wowote.

Sababu kuu iliopelekea nisianze tiba ni matumizi yake hii dawa ipo vice versa wakuu yaani hahiitaji mdomo ndo ule dawa inahitaji anus ndo ile dawa

1. Je, Anusol Suppositories ni salama kwa kijana mwenye umri chini ya miaka 20?


2. Kuna madhara yoyote yanayoweza kujitokeza kwa kutumia dawa hii?

3. Kuna njia mbadala – kama lishe, mazoezi au tiba asilia – ninazoweza kuanza nazo kabla ya kutumia dawa?


Sitafuti tiba kamili hapa, bali mwanga na ushauri kutoka kwa wale waliowahi kupitia hali kama hii au walio na uelewa wa tiba. Niko tayari kusikiliza kila mchango wa kujenga.

Nawashukuru sana kwa kunisoma, na kwa yeyote atakayechangia nitathamini sana ushauri wenu.🙏

Note:Mficha maradhi umauti humuumbua
 

Attachments

  • IMG_20250420_185702.jpg
    IMG_20250420_185702.jpg
    402.4 KB · Views: 43
Kwamba unahisi wakati unajiingizia utakuwa unasikia utamu hadi kupelekea kuzoea na kuanza michezo ya ushoga?
 
Hio dawa watu wakikuona unaitumia wanaanza kukufikiria visivyo kwamba unafanyiwa mchezo mchafu hasa hasa wanawake wakikuona unaitumia mawazo yao yanahamia huko
 
Wewe ndo umenielewa
Wakati unajiingizia ww chukulia kama kitendo cha kupata tiba, usiwe na mawazo ya kupata burudani, maana kubakwa na kufanya mapenzi ni kitendo kimoja ila utofauti upo kwenye hisia.
 
Back
Top Bottom