bless on
JF-Expert Member
- May 22, 2026
- 1,213
- 2,938
Fikiria unatembea mtaani, kisha unamwona jirani yako anatoka nje na kuanza kucheza muziki katikati ya barabara. Hakuna spika, hakuna radio, wala hakuna wimbo wowote unaopigwa... lakini anacheza kwa kasi kubwa huku akivuja jasho.
Baadaye jirani wa pili anajiunga naye, wa tatu, na ndani ya siku chache mji mzima unakumbwa na janga la kucheza muziki hadi watu kuanguka na kufa!
Hii si filamu ya kutisha; ni tukio la kweli lililotokea mwaka 1518 katika mji wa Strasbourg (ambao leo upo nchini Ufaransa) linalojulikana kama "The Dancing Plague of 1518".
Mwezi Julai 1518, mwanamke mmoja aitwaye Frau Troffea alitoka nje ya nyumba yake na kuanza kucheza muziki barabarani.
Alicheza bila kusimama siku nzima hadi usiku mnene.
Pamoja na miguu yake kuvuja damu na viatu kupasuka kwa uchovu, alishindwa kujizuia au kusimama!
Kufikia mwisho wa wiki hiyo, watu 34 walikuwa wamejiunga naye mtaani wakicheza usiku na mchana.
Fumbo hili lilipozidi kuwa kubwa, viongozi wa mji waliiomba msaada mabaraza ya madaktari. Madaktari wa zama hizo walitoa hitimisho la ajabu: Walidai kuwa wagonjwa hao walikuwa na "damu ya moto" (hot blood), na njia pekee ya kuwatibu ilikuwa ni kuwaacha waendelee kucheza usiku na mchana ili damu hiyo ipoe!
Ili "kuwatibu", serikali ya mji ilifanya makosa makubwa zaidi:
Walikodi wanamuziki na wapiga ngoma waje kupiga muziki mtaani.
Walijenga majukwaa makubwa ya mbao katikati ya mji na kukodi wachezaji wa kulipwa ili wawachochee watu hao waendelee kucheza.
Matokeo yake yakawa maafa makubwa! Kufikia mwezi Agosti, zaidi ya watu 400 walikuwa wanacheza bila mpangilio mtaani. Kila siku, watu kati ya 15 hadi 20 walikuwa wanaanguka chini na kufa kwa mshtuko wa moyo (heart attack), uchovu uliokithiri (exhaustion), na kiharusi (stroke)!
Mwezi Septemba 1518, mlipuko huo ulianza kupungua taratibu baada ya waathirika waliobaki kupelekwa kwenye matibabu na kupumzishwa