Ugonjwa wa kifafa usikilizeni redioni. Simulizi yake ni ya kutishaa!

Primary nilisoma na jamaa tens jirani, alikuwa anaanguka though sio sana. Mara ya kwanza kumuona nilishangaa sana, sikujua ni kitu gani. Shule ya upili nililala dom moja na jamaa alikuwa anaanguka balaa, yani karibia kila mwezi mwamba alikuwa anaanguka, hilo povu analotoa sasa ni balaa.

Sad sana
 
Daaahh... Huzunii sana
 
Ads
Pole sna kiongozi nami nilikuwa na Mama mdogo wangu naye alikufa kw a kuungua moto zamani mwaka 1996 ndo alikufa huu ugonjwa ni hatari Sana Ila ,nilisimuliwa kuwa huyu Mama mdogo alilogwa
A
Pole sna kiongozi nami nilikuwa na Mama mdogo wangu naye alikufa kw a kuungua moto zamani mwaka 1996 ndo alikufa huu ugonjwa ni hatari Sana Ila ,nilisimuliwa kuwa huyu Mama mdogo alilogwa .
ANte sana mkuu
 
Ina
Instisha sana
 
Dahh, Pole sana mkuu. Mungu amrehemu mama yetu mpendwa [emoji120][emoji120][emoji120]
 
Dah pole sana nimejikuta mpka chozi limenitoka aisee pole sana mkuu
 
Ndugu me binafsi na mdogo wangu ambaye amekuwa akitesela na huo ugonjwa ni muda sasa kifafa kimemfanya ad adhoofike afya tumeshajarib kila namna apone lakin imekuwa ni kaz bure hasa kikifika kipindi cha mwezi kuchomoza limekuwa ni tatzo kubwa ndan ya familia kama unaujuz wowote kuhus huo ugonjwa tujuzane
 
Sitokuja kusahau mwaka 1998 nasafiri na basi dogo DCM toka Tukuyu kwenda Ushirika, nimekaa siti ya mlangoni ghafla nikamuona konda anakakamaa ameshika chuma cha pembeni ya mlango na mlango upo wazi na gari ipo kwenye spidi ya kawaida, anauma ulimi wake anatoa mate anakakamaa kashika chuma kile cha kushika kama unapanda kwenye daladala bahati alikuwa amegeuka anaangalia ndani ya gari anahesabu pesa zake.
Nilichomoka kama komandoo kipensi kabla hajaachia chuma kumdaka na kumshikilia kwa nguvu sana huku nikimpeleka kwa ndani ya gari asianguke nje na kugonga kichwa chini na gari kumpitia na tairi ya nyuma.
Alinishika kwa nguvu sijawahi ziona toka nazaliwa alinishika mikono chini ya mabega lakini mimi nilishika shingo badae akaachia mikono akashika nguo kwa nguvu za ajabu mpaka zikatatuka mifuko ya kifuani.

Kuna mama mmoja akamwekea kanga mdomoni mimi nimemshika yule jamaa kama dakika 15 hizi nikaona ameanza kulegea. Shati lake limetapakaa mate na mimi nimetapakaa mate na mambo mengine ya kibinadamu.

Niliambiwa nimuache pale pale atulie na tukafika ushirika stendi jamaa akiwa bado amepoteza fahamu. Lakini lile tukio siwezi kulisahau maishani mwangu. Nilipewa sifa nyingi sana kwa tukio lile. Kuna jamaa alikuwa anaitwa Mwakibete alininunulia shati pale ushirika maana la kangu lilichanika kwenye kwapa ile vuta nkuvute na kidogo nilitapakaa mate ule mgusano wa nguvu kama tunacheza mieleka vile.

Jamani kifafa ni ugonjwa hauna mfano kwa kuogofya,kustua na kutesa watu wa Mungu.

Mwenyezi Mungu atusaidie sana sisi waja wake. Amina
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…