Ugonjwa wa kifafa usikilizeni redioni. Simulizi yake ni ya kutishaa!

Nakumbuka kuna bint mmoja alikuwa na kifafa sasa walienda shambani kulima yeye akawa ameenda kwenye mto jirani na shamba lao, asee yule bint alifia pale pale kwenye mto baada ya kuangukia kwenye mto
 
Duh pole mno, Ila inasemekana mgonjwa wa kifafa akianguka na akaungua moto hata kidogo tu basi kupona Ni km haiwezekani tena
 
ubarikiwe
 
tahadhari ukimuona mtu yoyote anaelezea kitu cha kijamii na hakuweza kutoa faida wazi na kusema munifuatee kwenye Dm yangu nawaombeni muwapuuze ni matapeli wakubwa na ni hatari na wengi wanakuja kwa njia ya matibabu . wewe kama unania ya kusaidia mtu kwanini husemi hadharani kila mmoja apate faida unamwambia aje chumbani kwako ili afanyeje?
 



Itoshe tu kusema umenitonesha kidonda!

Marehemu mama yangu alikuwa na huu ugonwa, naomba nisiongee sana maana madhila yake siyo ya kusimulia.
 
Itoshe tu kusema umenitonesha kidonda!

Marehemu mama yangu alikuwa na huu ugonwa, naomba nisiongee sana maana madhila yake siyo ya kusimulia.
Pole sanaa broo
 
Binam zangu wawili waliteseka sana na huu ugonjwa...
Kama unavyosema mda wote miili yao ina majeraha ya kutisha.
Mmoja alifariki tu akiwa amelala...
Mwingine bado yuko hai. Nakuja dm utusaidie dawa
 
bibi na babu yako walikuwa wazazi wa hovyo kupata kutokea,hawakustahili lawama tu bali hata adhabu.ukute mambo ya kimila walimsindikiza mtoto wao(mama yako).
mgonjwa wa kifafa ni kilema kama wengine,anahitaji ukaribu wa hali ya juu,yaani hata kama ni kazi anafanya hatakiwi kufanya akiwa peke yake.

kifafa kimeua dogo niliyekuwa naye,amekua nacho kwa muda mtefu alivyokua mtu mzima akaanza kuachwa peke yake,nilikuja kuambiwa alitumbukia kisimani akakutwa ameshapoteza maisha.

kilimkosa kosa mshkaji ambaye ana kovu kubwa mguuni mpaka leo baada ya kuangukia jiko la kuni,yaani aliiva kabisa sehemu ya mguu.


kifafa kibaya kabisa ni cha uzazi,maana kwanza mnakuwa hamjui kama ndugu yenu anacho,mpaka ashike mimba,tarehe za mwisho mkitarajia atashikwa na uchungu kama wanawake wengine aombe msaada,pale pale anakula kabali.ilibaki kidogo nipoteze dada yangu kwa aina hii ya kifafa,aliyemuokoa ni rafiki yake ambaye huja kushona naye nyumbani pale,kaja amekuta sister anakoroma tu mapovu sakafuni.

pole sana mkuu.
 
Binam zangu wawili waliteseka sana na huu ugonjwa...
Kama unavyosema mda wote miili yao ina majeraha ya kutisha.
Mmoja alifariki tu akiwa amelala...
Mwingine bado yuko hai. Nakuja dm utusaidie dawa
Pole sana kwa masaibu ya wajomba zako ila nakushauri muombe msaada atakaotaka kukupa aupandishe hapa jukwaani sisemi ni tapeli ila ni salama zaidi na utakuwa na msaada kwa wengine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…