Ugonjwa wa kifafa usikilizeni redioni. Simulizi yake ni ya kutishaa!

Dah pole sana, inasikitisha sana.

katika tembea yangu katika pilika za kutafuta maisha nimewai fanya kazi na mjerumani mmoja mgonjwa wa kifafa, nilichoona jamaa alikuwa anavuta bangi, na alivyosema yeye inamsaidia sana, akivuta anakuwa sawa na anafanya kazi.

Kwa wenye ndugu wenye kifafa labda mujaribu, siyo kuvuta msokoto mzima kwa mara moja, msokoto mmoja anauvuta mara tatu hivi kwa siku, Maybe inaweza ikasaidia.
 
Duh pole sana. Umesema ugonjwa huu hauna tiba lakini labda ni kwa nchi zetu za Kiafrika. Nilikuwa na rafiki yangu mmoja kwa jina Faisal nchi Uingereza miaka ya mwanzo 2000. Yeye alikuwa ni mkimbizi kutoka Somalia, siku moja hatuna hili wala lile tukiwa tunafurahia maisha mara jamaa kadondoka chini anatapatapa mapovu yanamtoka na haja ndogo inamtoka.

Ikaitwa ambulance kufika pale akafanyiwa huduma ya kwanza, wakaona hali alivyokuwa nayo hawaiwezi wakaita air ambulance. Chopa ikaja akapeleka St Thomas hospital London sisi tulikuwa tuna Kaa Canterbury Kent. Kufika St Thomas hospital, jamaa akafanyiwa operation ya kichwa. Alikaa hospital kama miezi 2. Miaka 8 baada ya operation jamaa Hajawahi tena anguka kifafa.

Alikuja twambia kuwa alikuwa na ugonjwa huo toka azaliwe huko kwao Somalia ila mara ngingi alikuwa ana sikia dalili zake hivyo anajizuia shughuli zozote za nje ndio maana hatukujua kuwa ana ugonjwa huo. Pamoja na kupona jamaa amewekwe kwenye scheme ya Disabled allowance hivyo hafanyi kazi yoyote ya kuajiriwa analipwa £ 200 kwa week. Huku kwetu utaziona nyingi saana lakini huko ni pesa ya kawaida sana.
 
Daaaa huu uzi bora ningeupita tu
 
Pole sana kwa yaliyokukuta

Kuhusu njia za kumsaidia mtu mwenye huo ugonjwa kwanini usiweke hapa kwa faida ya wasomaji wa sasa na wa baadae(miaka ijayo)

Naamini sio siku zote utapatikana PM lakini nyuzi za JF huwa zinaishi
@mgaguzi Husika na kichwa cha habari hapa juu
 
Huu ugonjwa usikie tu, unanisumbua almost miaka miwili Sasa. Ikinitokea mkono wa kulia ndo naumia sana na kujing'ata.
Kitu kingine nilichonotice hivi karibuni ni kuwa ikinitokea huwa nakaa kama wiki hivi nakuwa sina kumbukumbu vizuri.
Ee Mungu naomba uniponye!!
 
Kuna Jamaa yangu alipata Ajali mbaya pale Bwawani miaka ya 90 mwishoni aikuwa kwenye Coma karibia miezi mitatu alipopona akarudi kwenye kazi lakini akarudi na Kifafa sema yeye kinakuwa na dalili kwahiyo huwa anapaki Gari na hakimshiki mara kwa mara na anaendesha Petrol Tanker.
 
Pole sana
 
Mcheki mkuu Mganguzi amesema anatoa ushauri kwani ana uzoefu kupitia mzazi wake
 
Reactions: Gru
Yesu anaponya hii ugonjwa bure, mpelekeni kwenye maombi.
 
Aisee pole sana

Miaka miwili iliyopita Kuna kijana hapa mtaani alikuwa na huo ugonjwa.

Sasa huwa anakata majani ya Ng'ombe.

Siku hio akaenda kukata majani karibu kabisa na bwawa la maji.

Ugonjwa ukamtaiti akaangukia bwawani akafia huo baada sana watu wakaja kumkuta humo.

inasikitisha sana.

Wanasema watu wenye vifafa hawahitsji kukaa sehemu zenye mwanga mwanga.
 
Kwanini usiweke tiba yako hapa hadharani kama unampango wa kusaidia??? Huko DM kuna watu wanaweza toka na manundu. Angalizo tu.
Ugonjwa wa. Mfumo wa fahamu huo

Sijawahi sikia kama Kuna Tiba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…