kwa kweli wanawake wengi tunatabia hiyo ya kununa kwa sababu ambazo si za msingi na mara nyingi huwa tunafanya hivyo kama kukomoa, au kwa matarajio ya kubembelezwa, na pia huwa ni dalili ya udhaifu, mtu anaudhiwa na kusema hawezi either mume ni mkorofi au haingiliki basi anaamua kununa tu kama njia ya kuonyesha au kueleza hisia zake n.k n.k. na tabia hii mara nyingi huwa nao couples ambao hawana mawasiliano ya kutoasha, hawawezi kuambiana ukweli, wanaogopana n.k. ila kwa wale ambao hawana mambo ya pembeni wako wazi kuambiana mambo yote mazuri au mabaya huwa hawana tabia hizi. LAKINI WANAUME jamaniii looh ndio usiseme. wakitaka kupata sababu ya kuondoka nyumbani bila kuaga, kuacha KULA nyumbani, kuweka distance n.k. huwa nao wanatabia kama hiyo, jambo dogo atalivalia njuga, atalipaka wanja na uturi alimradi tu linukie weee liwe kubwa apate justification ya kufanya mambo yake bila bughudha! achani hizo na nyie:biggrin: