Ugonjwa wa manjano kwa watoto wachanga elimu zaidi itolewe kwa jamii

Ugonjwa wa manjano kwa watoto wachanga elimu zaidi itolewe kwa jamii

Miss Natafuta

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2015
Posts
27,031
Reaction score
49,928
Kuna huu ugonjwa wa manjano kwa watoto wachanga ni hatari sana ila nashangaa huwa wamama hawafundishwi chochote Matokeo yake wamama wengi wanapoteza watoto kizembe.

Wakati najifungua hosp pale asilimia 90 watoto wote walipata manjano. Mimi mwenyewe niliponea chupuchupu mloganzila hospitali.

Namshukuru pro jamani sio kwa huduma zile.

Naomba elimu itolewe kwa wamama toka wakiwa wajawazito.

Mfano kumbe ukila miwa ukiwa mjamzito mtoto hapati manjano. Sasa Mimi niliambiwa ukila miwa mtoto anazaliwa kakatika katika kama jongoo.

Nikiwa mjamzito nilikuwa nakimbia miwa vibaya mno
Hata kupona kwa mtoto niseme kweli pamoja na matibabu ya hospnilikunywa Sana juice ya miwa akawa ananyonyea miwa.huko kwenye maziwa.

Nimeongea hili baada ya kwenda CCBRT na kuona watoto ambao wameathirika na manjano.bahati mbaya manjano haikupata dawa wamekuwa walemavu
 
Sababu kuu ya ma njano kwa mtoto ni nin ??
Mtoto kukosa maziwa ya kutosha??
 
sasa Mimi niliambiwa ukila miwa mtoto anazaliwa kakatika katika kama jongoo .nikiwa mjamzito nilikuwa nakimbia miwa vibaya mno
Hata kupona kwa mtoto niseme kweli pamoja na matibabu ya hospnilikunywa Sana juice ya miwa akawa ananyonyea miwa.huko kwenye maziwa
Nimeongea Hili baada ya kwenda ccbrt na kuona watoto ambao wameathirika na manjano.bahati mbaya manjano haikupata dawa wamekuwa walemavu
Uliambiwa na ukaamini?! Bila shaka ulibeba mimba ya utotoni.
 
Kama mtoto ana manjano mama jitahidi upate maziwa ya kutosha mnyonyeshe mara kwa mara manjano yanaisha
 
Tatizo mnapenda kusikiliza watu wasio na utaalamu wa mambo husika.
Mtu sio Daktari lakini unamsikiliza kwa ishu za kidaktari

Alafu wengine wamesoma Kabisa.

Bure Kabisa
 
  • Thanks
Reactions: I M
Kama mtoto ana manjano mama jitahidi upate maziwa ya kutosha mnyonyeshe mara kwa mara manjano yanaisha
Kama huna my dear .utakiwana maziwa ukatae kumpa mtoto .mwili unachelewesha maziwa unafanyeje?
 
Kuna huu ugonjwa WA manjano kwa watoto wachanga ni hatari sana ila nashangaa huwa wamama hawafundishwi chochote Matokeo yake wamama wengi wanapoteza watoto kizembe. Wakati najifungua hosp pale asilimia 90 watoto wote walipata manjano .mimi mwenyewe niliponea chupuchupu mloganzila hosptal.namshukuru pro jamani sio kwa huduma zile
Naomba elimu itolewe kwa wamama toka wakiwa wajawazito
Mfano kumbe ukila miwa ukiwa mjamzito mtoto hapati manjano.sasa Mimi niliambiwa ukila miwa mtoto anazaliwa kakatika katika kama jongoo .nikiwa mjamzito nilikuwa nakimbia miwa vibaya mno
Hata kupona kwa mtoto niseme kweli pamoja na matibabu ya hospnilikunywa Sana juice ya miwa akawa ananyonyea miwa.huko kwenye maziwa
Nimeongea Hili baada ya kwenda ccbrt na kuona watoto ambao wameathirika na manjano.bahati mbaya manjano haikupata dawa wamekuwa walemavu
Mambo mengine ni kukosa elimu tu. Ugonjwa wa manjano unatibika bila hata gharama kubwa. Mchukue mtoto anika kwenye jua la saa 4 kwa nusu saa. Baada ya week hamna ugonjwa na ni tiba ya uhakika.
 
Tatizo mnapenda kusikiliza watu wasio na utaalamu wa mambo husika.
Mtu sio Daktari lakini unamsikiliza kwa ishu za kidaktari

Alafu wengine wamesoma Kabisa.

Bure Kabisa
Wewe nawe bna issue za wanawake unaponda Tu
Utakuja kuoa kiazi dunia nzima
 
Mambo mengine ni kukosa elimu tu. Ugonjwa wa manjano unatibika bila hata gharama kubwa. Mchukue mtoto anika kwenye jua la saa 4 kwa nusu saa. Baada ya week hamna ugonjwa na ni tiba ya uhakika.
Ndo elimu itolewe mkuu.ulishawai kuona unazungumziwa popote?
 
Mimi pia mtoto wangu wa mwisjo alipitua hii changamoto nashukuru Mungu tulivuka salama kwenye hili.
Nachoona ni mtoto kukosa maziwa kwa wakati mimi huwa nakaa mpaks siku 2 ndo maziwa yanatoka. Waruhusu maziwa mbadala kwa wale wenye changamoto ya kukosa maziwa mara baada ya kujifungua
 
Nakumbuka mwanangu alipata hiyo njano na homa kali kakiwa na wiki moja cheeii nlichanganyikiwa, ila Dr alimpa amoxylin syrup na ebufen ya kutuliza homa....ndani ya siku 3 akawa tu poa na unjano ule ukaisha
 
Tanzania kuna ombwe kubwa sana la taarifa zisizo sahihi na watu huziamini!, ama naweza sema kuna imani nyingi za uongo watu wanazifuata!, Naamini ktk uhalisia na elimu mama yani ile ya practical hiyo ndo huleta majibu hizi imani ni mzigo sana!.

Mama mjamzito ama mwenye mtoto anatakiwa awe makini sana na vilevile aangaliwe kwa ukaribu pia msosi natural ndo yanatakiwa yawe maisha yake.
 
Back
Top Bottom