QALLI MIZOH
JF-Expert Member
- Mar 19, 2014
- 2,075
- 698
mdogo wangu amewahi kuumwa ngiri kama miaka 5 {now ana age[ 24]}iliyopita akatumia tiba asili akapona na mzigo akawa anapiga kama kawa..lakini ana kama wiki 2 zimepita anazisikia dalili tena za ngiri..tumbo kujaaa gesi, mgongo unauma, pu,.mb 1 dg 1 kubwa... kukosa hamu ya papuchi nk lakini yey yupo mazingira ya joto tu la kawaida..
labda tumsubiri dr wetu mzizi aje atufahamishe hapa kwa faida ya wengi..
ngoja tuombe ushauri kwa dr wetu MziziMkavu aje atuambie kama vina uhusiano na juu ya tiba ya ngiri
hauna jina lingine huu mmea.. kuna mizzi ya mlimao lemmon} pia nasikia inasaidia sana..Asante kwa kunipa huo uzoefu, mkuu. Kumbe mgonjwa anaweza kukaa muda mrefu hv bila operesheni? Nimefanikiwa kumpa dogo dawa ya mizizi ya mmea wa mturatura ( Solanum incanum)--nimeitwanga mizizi, pamoja na magamba yake, nikachanganya maji kidogo, nikaikamua na kumpa dogo kimiminika chake. Sasa walau maumivu yametulia na hata ameweza kula chakula amekula--mwanzo alikuwa hawezi kula kabisa, maumivu yalikuwa makali. Ngoja niendelee kumwangalia hadi monday nimpeleke hospital aka-undergo surgery. Nakushukuru sana.
hauna jina lingine huu mmea.. kuna mizzi ya mlimao lemmon} pia nasikia inasaidia sana..
Kaka mpeleke hospitali,kienyeji utapoteza muda na pesa bure na hutapata tiba
Mara nyingi tumekuwa tukisikia watu (hasa wanaume) wakitakiwa kukaa mbali na baridi kuwaepusha wasipatwe na ugonjwa wa ngiri. Hivi kuna uhusiano gani kati ya ugonjwa wa ngiri (hernia) na baridi? Baridi huchangiaje uwepo wa ugonjwa huu?
Nauliza hivi kwa sababu kuna mtoto wangu wa kiume mwenye umri wa miaka 4 amepatwa na ugonjwa huu na ninahisi mara nyingi dada anamuacha anakuwa exposed sana kwenye baridi. Ana maumivu ambayo kuna wakati yanapungua na wakati yanaongezeka na sehemu zake za siri zimesinyaa sana (zinafanana kama za mtoto mchanga).
Kuna baadhi ya watu wananishauri nitafute tiba ya asili na wengine wanasema hakuna kitu kama hicho, wanadai kwamba tiba yake ni operesheni tu. Nipo njia panda. Ushauri wenu ni muhimu sana, wakuu. Natanguliza shukurani.
UGONJWA MSHIPA WA NGIRI HERNIA/HYDROCELE'
Ni ugonjwa unaowapata wanaume
na wanawake wa rika
zote.Mshipa wa ngili ni jina
linalokusanya magonjwa kama ngiri kavu'Hernia',ngiri
maji'Hydrocele'na ngiri
nyinginezo kama vile kuvimba
kokwa au mfereji unaopitisha
manii'Epididmorchitis'.NGIRI
KAVU'HERNIA'Aina hii ya ngiri huwapata wanawake na
wanaume tu.Ngiri kavu
inapopata M'mke
huitwa'Fermoral Hernia'kwa
wanaume'Scrotal hernia'kwa
maana halisi ngili au mshipa wa ngili ni hali inayotokea ktka
mwili wa binadamu ambapo
sehemu fulani ya nyama ya
viungo mbalimbali vya mwili
hujipenyeza kupitia sehemu
dhaifu ya mwili na kutokeza upande wa pili.Sehemu hiyo
inayoathiriwa mara nyingi
huwa ni maeneo ya
tumbo,kokwa,pumbu nk
ambapo baadhi ya viungo vya
mwili vilivyomo tumboni hujipenyeza kupitia vitundu
vinavopitisha mishipa ya
fahamu inayohudumia
kokwa'Spesmatic Cord'hivyo
baada ya kujipenyeza
huteremka hadi ndani ya korodani hali ambayo
hukamilisha kuwepo kwa
ugonjwa wa mshipa wa
ngiri.Hata hivyo mshipa wa ngili
hujitokeza sehemu mbalimbali
za mwili na hupewa majina kutokana na
ulipojitokeza,mfano ngiri ya
tumbo huitwa'Abdominal
Hernia',watoto wanaozaliwa na
vitovu vikubwa'Umbilical
Hernia',sehemu ya haja kubwa'Anal Hernia'.Dalili
hazitofautiani hata hivyo ngiri
hujitokeza bila maumivu yoyote
isipokuwa kuna baadhi ya ngili
hujitokeza na maumivu makali
hutegemea ngiri ilivotokeza.DALILI:Uvimbe
unaoteremka kuingia ndani ya
korodani'Direct Scoratal inguina
Hernia',uvimbe unaojitokeza
tumboni na kuteremka hadi
ndani ya korodani dalili zake ni kuvimba uvimbe unaotoka
tumboni na kuteremka hadi
ndani ya korodani,uvimbe huu
hauumi na unaweza
kurudishwa kwa urahisi iwapo
mgonjwa atalala chali na kusukuma kwa vidole,uvimbe
huu ukikubali kurudi ndani
huitwa''Reduible direct scrotal
inguinal hernia'icpokubali
kurudi tumboni hupewa jina
la'Irreduible direct scrotal inguinal hernia'.USHAURI:Ni
vema uwahi kwa Dkt.
unapogundua tatizo.
UHUSIANO NA BARIDI ....wakati wa baridi muscles around spermatic cord zina contract and kwa mtu mwenye hernia means kuna abdominal parts zimeingia kwenye spermatic cord thus ile contraction kutokana na batidi hupelekea maumivu.....
Ndugu God bell,
Pole kwa maumivu.
Kwanza niseme kuwa kwa kiswahili bado kuna mkanganyiko wa neno Ngiri. Wapo wanoiita ngiri kwa maana ya busha (hydrocele), na wengine huita ngiri (Hernia) ambayo ni sehemu ya viungo kuingia sehemu nyingine kwasababu ya kuwa l'oose'
Kwa maelezo yako nadhani unaongelea abdomen hernia ambayo sehemu ya utumbo hutumbukia katika hasua. Hii ni kwasababu sehemu inayozuia (kiwambo) inakuwa imeachia. Utumbo huingia huko na kukuletea maumivu. Siyo maradhi yanayosababishwa na wadudu, hutokea hata kwa watoto wadogo au watu wazima ambao hufanya kazi za nguvu n.k.
Hakuna dawa inayotibu bali zinazopunguza maumivu. Mara nyingi ukilala na taratibu kusukuma hicho unachokihisi kurudi juu, basi hali inaweza kutulia. Itajirudia tena tena kwasababu umesogeza tu lakini hujazuia.
Matibabu yake ni operesheni ya kufunga sehemu hiyo. Matibabu hayo ni muhimu sana kwasababu inaweza kutokea kuwa utumbo umeingia ukajikunja na kushindwa kupitisha damu (strangulated hernia) hivyo sehemu hiyo itaoza na kuweza kuleta madhara makubwa zaidi tusiyotarajia.
Hutokea nadra lakini inapotokea hujui utakuwa sehemu gani ya huduma muhimu na za haraka hapo unaweza kujikuta katika wakati mgumu sana kimaumivu na pengine kimaisha.
Tafadhali kawaone madaktari katika hospitali kubwa kwa ushauri zaidi.
Kabla sijajibu swali lako naomba niweke sawa manenoya Kiswahili ili twende pamoja.Mkuu nimeuona huu uzi nisaidie pia. Mimi ilitokea zamani sana nilipigwa na barid kali nikahikuta sehemu moja ya kende haipo nadhani ilizama ndani. Nafanya sex kama kawaida sisikii maumivu yeyote. Sina hakika kama ilizama au ilisinyaa maana nilikuja kusitukia tu nina nanii moja.
Naomba ushauri tafadhari na jee hali hii ni hatari kiasi gani