Ugonjwa wa Vidonda vya Tumbo (Peptic Ulcers Disease): Kinga, tiba na ushauri

Ugonjwa wa Vidonda vya Tumbo (Peptic Ulcers Disease): Kinga, tiba na ushauri

mm nilianza kusumbuliwa na vidonda nikiwa chuo mwaka 2 vilinitesa mpaka mwaka wa 4, nilisoma kwa shida sana..

sasa hivi tatizo kubwa linalo nisumbua sana ni kichefu chefu, yaan vinaniletea kichefu chefu sana ingawa tumbo halisumbui kama mwanzo...

naomben msaada wenu wadau ni dawa gani naweza kutumia ili kuondoa hii hali ya kichefu inaninyima raha sana..

huwa kuna dawa yakuongeza appettite naitumiaga (famactin) hii inanisaidia kwa muda then baada ya week kama 3 au 4 kichefu chefu kinarudi tenaa..


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hizo dawa za nje gharama ni kama kiasi gani kwa dozi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kusema ukweli sijui. Inabidi uulizie sehemu yenye kuaminika. ehemu kama Oysterbay Pharmacy nadhani wanaweza kuwa nazo. Ila nikupe tahadhari kuwa siyo kila wanaomambiwa wana H-plory basi wanakuwa nao kweli au wanatakiwa kunywa dawa. Kuna aina ya H-plory ambayo haina madhara na baadhi ya madaktari wanashauri ukiwa nao haihitaji kutumia dawa.
 
Kama ni ACIDS pekee management yake ikoje?msaada tafadhari

Sent using Jamii Forums mobile app
Lengo ni kupunguza uzalishaji wa acids na kiwango cha acid (increasing pH) tumboni. Hivyo management ifuatayo itafaa:

• Kutumia dawa ambazo zinajulikana kama antiacids

• Kuzingatia ratiba (muda) wa chakula

• Kuepuka vyakula na vinywaji vyenye acids kwa wingi, n.k.

+ Ratiba ya chakula
Breakfast: 0600-0800 Hours
Lunch: 1200-1400 Hours
Dinner: 1830-2000 Hours

+ Kulala baada ya walau masaa mawili baada ya kula chakula cha usiku.

+ Kutumia mto utakaoinua kichwa kwa sentimita 15-20 wakati wa kulala

+ Kutokula vyakula vyenye majimaji mengi sana wakati wa usiku

+ Kuepuka vyakula vyenye:
> Mafuta mengi
> Chumvi nyingi na sukari nyingi
> Viungo/vikolezo/nyanya nyingi, n.k.
> Kahawa

+ Kuepuka matunda yafuatayo:
> Parachichi
> Ndizi mbivu
> Matunda jamii ya machungwa
> Matunda yenye uchachu

+ Kuepuka vinywaji vifuatavyo:
> Carbonated drinks zote (soda, juisi za kopo, n.k.)
> Maziwa
> Malta
> Energy drinks
> Red bull
> Ice cream

Note: Wagonjwa wote wa vidonda vya tumbo, bila kujali chanzo kama ni acids au H. pylori, wanapaswa kuepuka dawa zifuatazo: diclofenac, ibuprofen, diclopar na aspirin.
 
Back
Top Bottom