Kama ni ACIDS pekee management yake ikoje?msaada tafadhari
Sent using
Jamii Forums mobile app
Lengo ni kupunguza uzalishaji wa acids na kiwango cha acid (increasing pH) tumboni. Hivyo management ifuatayo itafaa:
• Kutumia dawa ambazo zinajulikana kama antiacids
• Kuzingatia ratiba (muda) wa chakula
• Kuepuka vyakula na vinywaji vyenye acids kwa wingi, n.k.
+ Ratiba ya chakula
Breakfast: 0600-0800 Hours
Lunch: 1200-1400 Hours
Dinner: 1830-2000 Hours
+ Kulala baada ya walau masaa mawili baada ya kula chakula cha usiku.
+ Kutumia mto utakaoinua kichwa kwa sentimita 15-20 wakati wa kulala
+ Kutokula vyakula vyenye majimaji mengi sana wakati wa usiku
+ Kuepuka vyakula vyenye:
> Mafuta mengi
> Chumvi nyingi na sukari nyingi
> Viungo/vikolezo/nyanya nyingi, n.k.
> Kahawa
+ Kuepuka matunda yafuatayo:
> Parachichi
> Ndizi mbivu
> Matunda jamii ya machungwa
> Matunda yenye uchachu
+ Kuepuka vinywaji vifuatavyo:
> Carbonated drinks zote (soda, juisi za kopo, n.k.)
> Maziwa
> Malta
> Energy drinks
> Red bull
> Ice cream
Note: Wagonjwa wote wa vidonda vya tumbo, bila kujali chanzo kama ni acids au H. pylori, wanapaswa kuepuka dawa zifuatazo: diclofenac, ibuprofen, diclopar na aspirin.