sina uhakika sana ila kipindi nataabika vitu nilivyozuiwa kula ni vyakula vyote vyenye acid kwa wingi, mafuta mengi kwenye chakula, vyakula vyenye caffein, vyakula vyenye vichocheo kwa wingi so nilikuwa sili jamii yote ya kunde labda kama itakuwa imetolewa maganda, vyakula vyenye vichocheo kama pilau, mikate yenye blue band pia nilikuwa sili, soda kama cocacola nilikuwa sinywi na mpaka leo sinywi, chai ya rangi/kahawa sikuwa nakunywa ilikuwa vyema nitumie maziwa fresh au uji lishe na ndio hasa niliiokuwa nautumia kwa kipindi chote niliichokuwa kwenye matibabu kama kifungua kinywa na wakati wote nipendao.
so mara nyingi niliikuwa nala vyakula simple ambavyo havijaungwa sana kama wali, wali wa nazi, ugali, viazi mringo, ndizi n.k nyama, samaki lakini chukuchuku, mbogamboga kwa wingi, matunda i.e karoti, embe, chungwa yale matamu, papai, water melon, n.k
kwa ujumla siwezi kukwambia chakula halisi ni kipi ila kama hali sio nzuri ni bora ujiepushe na vyakula vinavyochochea vidonda kuuma ila ukazane na vyakula vinavyosaidia vidonda kupona kwa haraka.
katika somasoma vitabu niliona hot paper inasaidia vidonda kupona hata ndimu ila ukiitumia wakati vidonda ndio vibichi vinauma ni kama ukijikata ukaweka ndimu inasaidia lakini maumivu yanakuwa makali hii nafikiri ni kwa sababu ya ile acid. la muhimu ni kuwa mwangalifu ujijue uko katika hali gani ule nini na kwa wakati gani unapopangilia kiukweli unapona. Pengine wengi tunashindwa pona kutokana na maisha ya mihangaiko mingi kutwa uko kutafuta na ule muda wa kula huna sana sana tunakimbilia kwa mama ntilie au kwenye buffet, ukirudi jioni nyumbani ndio hivyo ushakuwa usiku na chakula kizuri ambacho kingesaidia mwili ni kile cha asubuhi, mchana na jioni sio usiku.
Na mtu mwenye vidonda anatakiwa asikae njaa muda mrefu angalau anaweza kula baada ya masaa manne mpaka sita. Je wote twaweza haya?