Pole sana mkuu. Kwanza, ni muhimu kufahamu sababu kubwa za vidonda vya tumbo (Peptic Ulcer Disease-PUD). Vidonda vinasababishwa na
(i) Kuambukizwa vijidudu vijulikanavyo kama Helicobacter pylori
(ii) Mawazo yaliyopitiliza, yani, "Excessive stress"
(iii) Utumiaji wa dawa zijulikanazo kama Non Steroidal AntiInflammatory drugs (NSAIDS) mfano Diclofenac, Diclopar, Aceclofenac etc
(iv) Unywaji pombe uliopitiliza.
Kwa Africa, tafiti nyingi zinaonyesha sababu kubwa kwetu ni infection ya huyo mdudu aitwaye H. pylori.
Vipimo vya muhimu vya kufanya kwa mtu anayesemekana kuwa na tatizo la vidonda vya tumbo ni
i. Serology for H pylori, ambapo damu yako itatolewa na utapimwa kuona kama umeathiriwa na huyo mdudu na labda OGD (OesophagoGastroDuodenoscopy)/ Endoscopy kwa ajili ya kuangalia Koo lako ikiwa limeathiriwa na Tumbo lako pamoja na sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo (Duodenum). Pia, unaweza kufanyiwa Barium Meal (inaweza kuona kama kuna kidonda) au Abdominal Ultrasound kwa ajili ya kuondoa uwezekano wa sababu nyinginezo za maumivu ya tumbo.
Ikiwa utaonekana kuwa na vidonda na sababu ikawa ni H pylori (yani Serology for H pylori ikawa Positive), basi matibabu ni kwa ajili ya vidonda na pia kwa ajili ya H pylori. Ikiwa H pylori ikiwa negative, basi matibabu yatakuwa kwa ajili ya vidonda tu. Lakini ikiwa hutokuwa na majibu ya H pylori, basi matibabu yatakuwa kama mtu mwenye H pylori, maana wengi wetu wenye vidonda tunakuwa tuko infected na huyo mdudu.
Sasa, matibabu yako namna hii kwa upande wa dawa (Pharmacological treatment) kwa mtu mwenye H pylori na vidonda:
i. Proton pump inhibitor, mfano, Omeprazole au Esoneorazole au Rabeprazole. Kati ya hizo tatu, kali zaidi ni Rabeprazole.
Dozi, tukichukua mfano wa Rabeprazole (unatumia dawa moja tu, si zote tatu) ni:
Rabeprazole 20mg PO BD kila siku kwa wiki 6
ii. Antibiotics 2, zote unatumia kwa pamoja. Dozi zake ni:
a. Amoxycillin 1g PO BD kila siku kwa wiki 2 na
b. Azithromycin 500mg PO OD kila siku kwa wiki 2. Ikiwa una uwezo, badala ya kutumia Azithromycin unaweza kutumia
c. Clarithromycin 500mg PO OD kila siku kwa wiki 2.
OD=Unakunywa mara moja kwa siku
BD=Unakunywa mara mbili kwa siku
PO=Unameza (unakunywa kwa mdomo)...ni vidonge.
Aidha, tumbo likiwa linauma uma unaweza kutumia
a. Magnesium Trisilicate au
b. Relcer gel au Lucid Suspension au Mucogel 15mls PO TDS
Pia, kaa mbali na vyakula vyenye acid, kwa mfano, maharage na vyakula vyote vya jamii ya maharage, matunda machachu, ndizi mbivu na kuendelea. Pia, kaa mbali na pombe na kaa mbali na dawa za aina ya NSAIDs (Aspirin, Diclofenac, Diclopar, Aceclofenac etc). Pia jaribu kupunguza kuwa na msongo wa mawazo au kukaa na njaa kwa muda mrefu. Ukifuata yote hayo una uwezekano mkubwa wa kupona in no time. Best of luck & pole sana mkuu!