AFYA BORA
VIDONDA VYA TUMBO NI UGONJWA GANI?
Ugunduzi uliofanywa na watafiti kutoka mji wa Perth magharibi ya Australia mwaka 1982 na Prof. Robin Warren na Dr. Barry Marshall kutoka chuo kikuu cha Western Australia na washindi wa tuzo ya Nobel ya afya ya mwaka 2005.
Mabingwa hawa wa tiba waligundua kuwa, vidonda vya tumbo ni ugonjwa wa kuambukiza (communicable disease). Binadamu anaugua vidonda vya tumbo baada ya kupata maambukizi ya vimelea jamii ya bacteria vinavyoitwa Helicobacter Pylori.
Ugunduzi huu ni mapinduzi makubwa kabisa katika sayansi ya afya duniani katika karne 21, kwani unafuta dhana ya kwamba vidonda vya tumbo vinatokana na mawazo, kuchelewa kula na ugonjwa wa kurithi.
Wale wenye mtandao wanaweza ku google Helicobacter Pylori kujifunza zaidi juu ya vidonda vya tumbo na chanzo chake.
Tafiti zimethibitisha kuwa vimelea hivi Helicobacter Pylori vinaambukiza kati ya mtu na mtu kupitia mate (Saliva) na pia uchafuzi wa kinyesi cha binadamu kwenye maji na chakula.
Kwenye nchi maskini ukosefu wa maji salama, uchafuzi wa mazingira, na makazi duni yenye msongamano wa watu wengi, unachangia watu wengi sana kupata maambukizo ya vimelea hivi, hivyo kupelekea kuugua vidonda vya tumbo.
Kulingana na shirika la afya duniani nchi za Africa, kusini mwa jangwa la sahara, asilimia 80% ya wakazi wake wanaishi na vimelea vya Helicobacter Pylori na asilimia 20 % waugua vidonda vya tumbo.
Kimelea Helicobacter Pylori kinayvosababisha vidonda vya tumbo.
Baada ya mtu kumeza vimelea hivi kupitia mate ya mgonjwa, maji yasiyo salama, chakula kilichoandaliwa kutoka mazingira yasiyo salama na mikono michafu.
Vimelea hivi huweka masikani kwa kujichimbia ndani ya uteute unaofunika ngozi laini ya ndani ya mfuko wa chakula na kuzaliana na kuwa vingi.
Kulingana na ugunduzi wa mabingwa hawa, vimelea hivi huzalisha aina mbili za kemikali ambazo ni sumu kwa binadamu.
Kemikali sumu ya kwanza inajulikana kama Cag A
Sumu hii hufanya uharibifu kwenye mfumo wa uzalishaji wa tindikali (Hydrochloric Acid) kwenye mfuko wa chakula na kusababisha tindikali hii kuzalishwa kali sana na nyingi kuliko inavyohitajika (gastric atrophy) na kupelekea vimengenyo vya chakula kushindwa kumeng'enya chakula vizuri (dispepsia).
Mgonjwa hujisikia kama anaungua kwa ndani na maumivu makali ya tumbo, tumbo kujaa gesi na kuunguluma (bloating),
Maumivu makali sehemu ya juu ya tumbo, chini ya kifua, (chembe ya moyo)
Kupata kiungulia hasa baada ya kula chakula chenye asili ya tindikali kama vile viazi, maharage nk.
Kufunga choo au kupata choo kigumu wakati mwingine kinakuwa kama cha mbuzi na chenye uteute mwingi (constipation).
Mgonjwa mwenye maambukizi makubwa ya vimelea hivi, hali huwa mbaya zaidi, kwani kemikali sumu hii huzalishwa kwa wingi sana, uhalibifu unakuwa mkubwa zaidi, kemikali sumu hii na tindikali hufyonzwa na kusambaa mwili mzima, kupitia mishipa ya damu hivyo kuharibu kila kiungo muhimu cha mwili.
Mgonjwa hujisikia mchovu, mapigo ya moyo kuwa ya juu na ya kasi, homa za mara kwa mara, kuumwa kichwa na kipanda uso (migrane headache).
Maumivu yards viungo na misuli ya miguu, mikono, mgongo, mabega ,shingo n.k
Hisia za baridi, joto au ganzi kwenye nyayo za miguu, vidole vya mikono na miguu.
Kichefuchefu, kizunguzungu na kukosa hamu ya chakula.
Aina ya pili ya kemikali sumu inaitwa VacA
Kemikali sumu hii, husababisha uvimbe kwenye mfumo wa chakula (Inflammatory Bowel Disease-IBD), ukiambatana na maumivu ya tumbo.
Uvimbe kwenye koromeo la chakula unaitwa -Esophagitis, uvimbe kwenye mfuko wa chakula -gastritis, uvimbe kwenye sehemu ya juu ya utumbo mdogo -duodernitis, uvimbe kwenye utumbo mdogo -enteritis, uvimbe kwenye utumbo mpana -crown’s disease, au hemorrhoid- bawasili.
Hatari ya kuwa na uvimbe wa mfumo wa chakula (Inflammatory Bowel Disease-IBD) ni kuziba njia ya chakula hivyo mgonjwa kuhitaji upasuaji mkubwa. Hatari nyingine, mgonjwa anaweza kupata saratani ya mfuko wa chakula -Gastric Cancer au MALT –Lymphomas
Kemikali sumu VacA pia inasababisha kutokea kwa vidonda kwenye mfumo wa chakula (Bowel Ulcer Disease) na maumivu makali ya tumbo.
Vidonda kwenye koromeo la chakula vinaitwa -Esophageal ulcers, vidonda kwenye mfuko wa chakula -Gastric ulcers, vidonda kwenye sehemu ya juu ya utumbo mdogo -Duodernal ulcers, vidonda kwenye utumbo mdogo- Illem ulcers, vidonda kwenye utumbo mpana -Ulcerative colitis
Hatari ya kuugua vidonda kwenye mfumo wa chakula (Bowel Ulcer Disease) – mgonjwa kuishiwa damu mara kwa mara kwa sababu vidonda vinavujisha damu kwa ndani, kinyesi cha magonjwa hubadilika rangi na kuwa cha kahawia, damu nyingi ikivujia mgonjwa hutapika na kuharisha damu mbichi au iliyoganda.
Kidonda kilichojichimba kinaweza kutengeneza tundu kwenye tumbo hivyo kusababisha uozo ndani ya tumbo na kusababisha kifo.
Tafiti mbalimbali zimethibitisha kuwa kemikali sumu CagA, VacA na tindikali nyingi mwilini kutokana na maambukizi makubwa ya vimelea helicobacter pylori ni kisababishi kikuu cha magonjwa yafuatayo :-
Magonjwa ya Inni (Biliary Cirrhosis, Liver Sclerosis) na mawe kwenye kifuko cha nyongo –(Gall Stone Disease).
Magonjwa ya moyo (Cardiovascular Disease) na mishipa ya damu (Artherosclerosis), moyo kupanuka na kuwa mkubwa -Ischaemic heart disease(IHD), Shinikizo la damu – Hypertension, Shinikizo la damu kwa wajawazito- Pre- Eclampsia.
Ugonjwa wa kisukari- (Diabetes Mellitus II)
Magonjwa ya maumivu ya viungo
Kuvimba joints -Gout, baridi yabisi - Arthritis, yabisi kavu - Osteoarthritis.
Magonjwa ya ngozi, na kupata mzio -Allergies nk.
Tafiti nyingi zimethibisha kuwa mgonjwa mwenye maambukizi makubwa ya vimelea Helicobacter Pylori anauwezekano mkubwa wa vimelea hivi kuweka masikani ndani ya utumbo mpana,na kuzalisha kemikali wa sumu CagA, VacA na Ammonia kwa wingi.
Mlundikano mkubwa wa kemikali sumu hizi ndani ya utumbo mpana husababisha uvimbe na maumivu kwenye utumbo mpana na pia husambaa sehemu ya chini ya tumbo na kiunoni na kusababisha kuvimba na uharibifu kwenye viungo na misuli vinavopatikana sehemu hizi yakiambatana na maumivu makali ya mgongo na kiuno Chronic Pelvic Pain (CPP)
Pelvic Congestion syndrome (PCS) kwa wanaume au Pelvic Inflammatory Disease (PID) kwa wanawake, ni mjumuisho wa magonjwa yanayotokana na maambukizi ya vimelea Helicobacter Pylori ndani ya utumbo mpana:-
Magonjwa ya njia ya mkojo na figo kama vile :-
Uvimbe na vidonda kwenye figo- Chronic Kidney Injury (CKD) Ugonjwa wa mawe kwenye figo -(kidney stone disease) na kibofu cha mkojo -urine blader stone disease, , uvimbe,vidonda na kusinyaa kwa njia ya mkojo-Urethritis-UTI sugu, na kuvimba tezi dume kwa wanaume-Prostatitis
Matatizo ya uzazi -Reproductive disorders
Uvimbe kwenye njia ya mayai- Salpingitis –uvimbe ndani ya mfuko wa uzazi- Endometritis-mchango, kukosa nguvu za kiume-Erectile Disorder, kushindwa kushika mimba, na kuharibika kwa mimba changa- Spontaneous Abortion.