Ugonjwa wa Vidonda vya Tumbo (Peptic Ulcers Disease): Kinga, tiba na ushauri

Mkuu ana uhakika kuwa ni vidonda vya tumbo? Amefanya checkup gani akajua kuwa ni vidonda? Wataalam wanasema asilimia kubwa ya vidonda vya tumbo vinasababishwa na bacteria wanaoitwa H-plyori. Aliwahi kupima kama anao? Kama alipima akakuta anao alitumia dawa inavyopaswa? Hawa bakteria ni sugu sana na inabidi utumie mchanginyiko wa antibiotic aina mbili kwa muda wa wiki mbili na zaidi. Halafu baada ya mwezi na nusu au miwili ucheck tena kama wameisha. Halfu jambo la kuzingatia ni kuwa wakati wa kucheck usiwe umetumia antibiotic kwa muda au dawa nyingine zinazozoorodheshwa.
 
Ndugu hebu tupe mrejesho kama uliweza pata tiba, kama bado nikupe ushauri mwingine.
 
Ndugu zingatia sana ushauri wa huyu jamaa. Muhimu sana kutambua chanzo cha tatizo na hakikisha unakiondoa.

Ni muhimu sana ukaweka bayana ni jambo fani unafikiri lilikupelekea kwenye tatizo hili. Kuna mambo kama kukaa na njaa kwa muda mrefu, mawazo yaliyopitiliza n.k

Lifestyle unayosema umeibadili ni muhimu ikawa inaondoa chanzo. Ni muhimu pia ukaweka bayana ni ligestyles fani umebadili ili ushauriwe zaidi.

Zingatia vyakula na kula kwa wakati. Umeshauriwa pia kutumia vyakula kama bamia za kichemsha, kunywa maziwa ya fresh ya viguvugu. Chemsha na kisha yapooze.

Watu wanasema hata mayai mabichi husaidia. Ninaongea haya kwa uzoefu pia. Nilisumbuliwa sana vidonda vya tumbo. Kuna wakati nilipoumwa sana nilikuwa ninakoroga yao bichi kwenye kikombe na kunywa. Jizoeshe pia kula mlenda. Hii inafanana na bamia lakini ukipata ule wa kienyeji kama ule wa singida, itakuwa vyema zaidi.

Epuka vyakula vya nyanya (nyingi) na uji wa ulezi. Unasemekana kukwangua tumbo na hivyo kutonesha vidonda.
 
Niko kwenye mpango wa kujaribu kila dawa hapa.

Mungu asimame. Ndani ya hili Juma moja sijalala mara tatu.
 
Niko kwenye mpango wa kujaribu kila dawa hapa.

Mungu asimame. Ndani ya hili Juma moja sijalala mara tatu.
Pole nimepitia hayo masahibu ninaelewa maumivu yake, ila wakati mwingine inakua ngumu kumshauri mtu atumie nn hasa kutokana na kutojua vidonda vyako vipo kwenye hatua gani. Ila kwa kukusaidia zingatia sana haya...
-epuka vyakula vyenye kusisimua tumbo kama limao, ndimu, pilipili energy drink zote na vyakula vilivyotiwa viungo vingi.
- kama ni mpenzi wa soda, juice za viwandani na pombe zipe talaka muda.
- pia vidonda tumbo husababishwa pia na kuishiwa kwa maji mwilini hivyo jitahidi kila unapoamka asubuhi unywe glass 2 za maji kabla hata ya kupiga mswaki, na uwe unakunywa maji nusu saa au lisaa limoja kabla ya kupata mlo wa mchana au jioni hii husaidia sana kupunguza asidi iliyopo mwilini.
- jitahidi pia kula matunda kama walivoeleza wadau wengine na mboga za majani kwa wingi. Matunda kama parachichi, tikiti tango ni mazuri zaidi.
- japo wengine wanashauri matumizi ya maziwa ila kiuhalisia ni hatari sana kwa wenye vidonda tumbo, tumia soya kama mbadala wa maziwa ile isiyokaangwa.
- achana na kahawa, chai ya rangi nayo si salama, ikiwa unaweza tumia tu mchaichai au soya drink.
- kikubwa zaidi zingatia muda wa kula na kunywa maji ya kutosha, ikiwa utajisikia bado muwako tumboni changanya kijiko kimoja cha chai baking soda(usikijaze sana) na maji glass 1 hii husaidia sana kupunguza tindikali mwilini.
Jaribu kwanza kuzingatia hayo, sikushauri kabisa kukimbizana na madawa ya hospital mie nilishayatumia zaidi ya miaka 10 hayakunisaidia chochote zaidi kutuliza tu maumivu kwa muda na baadae hali inarudi kama mwanzo... Baada ya mwezi mmoja ukiona hali bado tete lete mrejesho nikueleze nini utumie uondokana na hilo tatizo, ila naamini ukizingatia hayo maelezo hapo juu tatizo lako litaisha kabisa.
 
Amepima na kakutwa na hao H-Plyor tena zaid ya Mara mbili kuhusu antibiotic katumia had I za Elfu 40 dose bado wamegoma had I madactar wameimshaur ahamie miti shamba
 
Amepima na kakutwa na hao H-Plyor tena zaid ya Mara mbili kuhusu antibiotic katumia had I za Elfu 40 dose bado wamegoma had I madactar wameimshaur ahamie miti shamba
Alitumia dose gani na ya muda gani? Dawa kuuzwa bei kubwa siyo kigezo cha kuponyesha! Inashauriwa mtu atumie dose ya siku 14 hata ikibidi na zaidi. Halfu iko combination ya dose mbalimbali, hivyo ikikataa moja unajaribu nyingine. Mambo mengine: 1: Anatumia dose kama inavyohitajika? Nauliza hivyo kwa sababu kuna watu wengine ni waoga dawa na anaweza kunywa siku kadhaa halafu akaachilia mbali. Tena unakuta ni mtu mzima kabisa na anajifanya kumeza kumbe hamezi. Hili nalo usilidharau. 2: Dawa anazotumia mna uhakika nazo? Siku hizi kuna dawa nyingi fake. Nunua dawa kwenye maduka yanayoaminika. 3. Una uhakika hapati uambukizo mpya? Hawa bacteria wanaambukiza kwa njia ya kula mboga au matunda yenye vimelea, au kutozingatia usafi wakati wa kutoka chooni au hata kama ana mpenzi/mume/mke anaweza kuwa namwambukiza. Na mwisho anapima na kupata matibabu sehemu ya uhakika? Bongo achana nayo kabisa ina hospital nyingi sana hawajui kupima.
 
Duuuuh ngoja nimuulize maana katumia dawa hadi huruma ....Mimi niliona moja inaitwa Omeplazole kitu kama hicho....
 
Duuuuh ngoja nimuulize maana katumia dawa hadi huruma ....Mimi niliona moja inaitwa Omeplazole kitu kama hicho....
Kwangu mimi naona kama tatizo lake kubwa huenda ikawa sehemu anazotibiwa siyo sahihi i.e. anatibiwa vi-hospital visivyo na utaalam wa kutosha. Hao bacteria kama ukienda hosptal yenye wataalam wanaisha. Halafu jambo muhimu ajaribu kuachana haya matibabu ya mtaani. Atajikuta anaongeza matatizo badala ya kupunguza. 1: Combination ya Amoxicillin 1000mgx2, clarithromycin 500mgx2 na lansoprazol 30mgx2 kwa siku 14 ni standard ya matibabu. Au mbadala wake ni combination ya: Tinidazole, clarithromycin na Lansoprazole. Lakini usijinunulie dawa bila kupima sehemu inayoeleweka na dr akuandikie!
 
mkuu nakushauri mimi nilikuwa nalo hilo sema sio mda mrefu kama wewe kabla ya yote, nenda kanunue dawa za amoeba meza, hata siku mbili haziishi itakuwa sawa. niamini kama ukifata ushauri wangu naomba marejesho. maana mimi nilisumbuliwa hadi nalia kama mtoto mateso yake asikuambie mtu na unaenda hosp dokta anakuambia haoni tatizo ila saizi niko sawa kabisa japo kuna madogo madogo ya ku fix.
 
nilawahi kusumbuliwa sana na tatizo hilo ila nashukuru numepoa. Ila kiukweli siwezi kumbuka nini hasa kilichoniponesha mana nilitapatapa na vitu vingi sana mwisho nikajikuta tu nishapoa. ila kwa vichache ninavokumbuka ni hivi

- nilitumia kunywa mafuta ya habasoda kila siku kijiko kimoja cha chai.
- Juice ya kerotti kila siku glass mbili moja kabla ya kula chochote asubuh na nyengine usiku. (ni karoti tupu na maji kidogo tu yakusagia bila ya sukari)
- nilitumia kula unga wa uwatu kila siku kutwa mara 3 kijiko kimoja cha chakula nachangaya na maji ya uvuguuvugu glass moja.
- na pia nilikua nikitumia kula manjano (japo kijiko kimoja kwenye maji na Thomu japo punje 3
 
Mimi nilikuwa natafuta kabichi mbechi kila siku, ndani ya wiki 2 maumivu yaliisha kabisa
 
Jamaa kapatwa na tatizo symptoms alizonazo ni pamoja na halitosis,bitter test throught the day
Msaada tafadhari medical expert
 
Bacteria that cause stomach ulcers and cancer could also be giving us bad breath, according to research published in the Journal of Medical Microbiology. For the first time, scientists have found Helicobacter pylori living in the mouths of people who are not showing signs of stomach disease.
 
Ahsante sana kwa maelezo na matibabu ya vidonda vya tumbo.

Naomba kuuliza kama kuna dawa ya kutibu homa ya ini HBV ikapona kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…