naomba uniambie hiyo dawa naumwaApime H. Pyroli. Dose ya dawa ni package ya aina 3 za dawa . Dawa si chini ya sh 40,000
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
naomba uniambie hiyo dawa naumwaApime H. Pyroli. Dose ya dawa ni package ya aina 3 za dawa . Dawa si chini ya sh 40,000
Kilimanjaro sehemu ganningekuwa Kilimanjaro ningekusaidia bure kuchukuwa dawa nikutumie ulipie nauli tu kuna rafiki yangu alisomaga Moshi tec nilimpeleka Kwa huyo masai alivyopewa huo ugonjwa ulikuwa ndo mwisho wake
Mwambie atumie bidhaa za edmark zitamuondoa kwenye hayo maumivu kabisa mcheck huyu dada 0692948695
Ndugu hebu tupe mrejesho kama uliweza pata tiba, kama bado nikupe ushauri mwingine.Nakuja kwenu wanajamvi kuomba msaada wa mawazo nifanyeje niweze kuondokana na tatizo hili sugu na lililonitesa kwa miaka 22 sasa.
Tatizo hili liligunduliwa kwa mara ya kwanza mwaka 1995 hospitalini na nikaanza kutumia dawa na kufuata masharti mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuepuka aina fulani za vyakula na madawa na pia kubadili lifestyle.
Nikiri kuwa baada ya muda fulani baada ya kuanza matibabu nilipata nafuu kubwa hadi husahau maumivu ya tatizo hili lakini nilijitahidi kubaki katika masharti yale.
Baadaye tatizo lilianza upya na nikaanza kutumia dawa zile zile nilizotumia awali lakini sikupata nafuu. Nimebadilisha dawa mbalimbali lakini bado tatizo limeng'ang'ania. Baadhi ya dawa ninazokumbuka nilizotumia mpaka sasa ni: CIMETIDINE, RANITIDINE, OMEPRAZOLE, PANTOPRAZOLE, LANSOPRAZOLE na Antiacids za maji kama MILK OF MAGNESIA na RELCER GEL.
Nimewahi pia kutumia dawa za kienyeji kadhaa bila mafanikio. Mfano: Unga wa mbegu ya parachichi, mafuta ya ubuyu, asali mbichi na mdalasini, kuchemsha mmea wa mbigili n.k.
Nimeshawahi pia kupima H.PYLORI TEST mara 2. Mara moja nilikutwa Positive nikapewa HELIGO KIT dozi ya wiki 2 na nikaendelea na lansoprazole kwa wiki 2 zaidi. Nilipopima tena H.PYLORI ikasoma Negative lakini bado nikindelea kuumwa.
Mwaka jana nilifanyiwa kipimo cha OESOPHAGOGASTRODUODENOSCOPY hospitali moja ya rufaa na ripoti ya Daktari ilisomeka: "Multiple wounds found around the duodenum". Nilipewa dawa lakini bado sikuona nafuu kubwa.
Hivi leo nina siku ya 6 natumia TINIDAZOLE, LANSOPRAZOLE NA CLARITHRIMYCIN kwa pamoja na bado sijisikii nafuu yoyote. Maumivu ni makali, tumbo linauma na kutonesha (painful & tender), nikila chakula kidogo tu nasikia tumbo limejaa. Siwezi kulalia ubavu wa kulia tena sababu ya maumivu.
Usiku wa leo tumbo liliniuma sana mpaka jasho likanitoka japo kulikuwa na baridi.
Kwa ufupi nateseka jamani na nimekuja kwenu kama kuna mhanga kama mimi aliyewahi kuugua tatizo hili na kupona au madaktari mliomo humu jamvini mnisaidie jinsi ya kufanya.
Natanguliza shukurani nikiomba radhi pia kwa post ndefu. Nimelazimika kuandika hivi ili tatizo langu lieleweke vema.
ASANTENI!
Mwanajamvi mwenzenu anayeteseka.
Ndugu zingatia sana ushauri wa huyu jamaa. Muhimu sana kutambua chanzo cha tatizo na hakikisha unakiondoa.Kingine cha muhimu na wengi tunasahau ni kuanza tiba bila kushughulika na chanzo hasa cha tatizo mara nyingi inakua ngumu kupona, mara nyingi vidonda husababishwa na kuzidi kwa tindikali tumboni hivyo ningekushauri jaribu kutumia vyakula vyenye uwezo wa kuondoa tindikali na kupunguza sumu ndo uanze matibabu na hakika utapona we mwenyewe utashangaa.
Anza kwa kutumia sana juice ya mboga mbichi za kijani, juice ya karoti na tango, watermelon vitakusaidia kwa sana.
Pole nimepitia hayo masahibu ninaelewa maumivu yake, ila wakati mwingine inakua ngumu kumshauri mtu atumie nn hasa kutokana na kutojua vidonda vyako vipo kwenye hatua gani. Ila kwa kukusaidia zingatia sana haya...Niko kwenye mpango wa kujaribu kila dawa hapa.
Mungu asimame. Ndani ya hili Juma moja sijalala mara tatu.
Amepima na kakutwa na hao H-Plyor tena zaid ya Mara mbili kuhusu antibiotic katumia had I za Elfu 40 dose bado wamegoma had I madactar wameimshaur ahamie miti shambaMkuu ana uhakika kuwa ni vidonda vya tumbo? Amefanya checkup gani akajua kuwa ni vidonda? Wataalam wanasema asilimia kubwa ya vidonda vya tumbo vinasababishwa na bacteria wanaoitwa H-plyori. Aliwahi kupima kama anao? Kama alipima akakuta anao alitumia dawa inavyopaswa? Hawa bakteria ni sugu sana na inabidi utumie mchanginyiko wa antibiotic aina mbili kwa muda wa wiki mbili na zaidi. Halafu baada ya mwezi na nusu au miwili ucheck tena kama wameisha. Halfu jambo la kuzingatia ni kuwa wakati wa kucheck usiwe umetumia antibiotic kwa muda au dawa nyingine zinazozoorodheshwa.
Alitumia dose gani na ya muda gani? Dawa kuuzwa bei kubwa siyo kigezo cha kuponyesha! Inashauriwa mtu atumie dose ya siku 14 hata ikibidi na zaidi. Halfu iko combination ya dose mbalimbali, hivyo ikikataa moja unajaribu nyingine. Mambo mengine: 1: Anatumia dose kama inavyohitajika? Nauliza hivyo kwa sababu kuna watu wengine ni waoga dawa na anaweza kunywa siku kadhaa halafu akaachilia mbali. Tena unakuta ni mtu mzima kabisa na anajifanya kumeza kumbe hamezi. Hili nalo usilidharau. 2: Dawa anazotumia mna uhakika nazo? Siku hizi kuna dawa nyingi fake. Nunua dawa kwenye maduka yanayoaminika. 3. Una uhakika hapati uambukizo mpya? Hawa bacteria wanaambukiza kwa njia ya kula mboga au matunda yenye vimelea, au kutozingatia usafi wakati wa kutoka chooni au hata kama ana mpenzi/mume/mke anaweza kuwa namwambukiza. Na mwisho anapima na kupata matibabu sehemu ya uhakika? Bongo achana nayo kabisa ina hospital nyingi sana hawajui kupima.Amepima na kakutwa na hao H-Plyor tena zaid ya Mara mbili kuhusu antibiotic katumia had I za Elfu 40 dose bado wamegoma had I madactar wameimshaur ahamie miti shamba
Duuuuh ngoja nimuulize maana katumia dawa hadi huruma ....Mimi niliona moja inaitwa Omeplazole kitu kama hicho....Alitumia dose gani na ya muda gani? Dawa kuuzwa bei kubwa siyo kigezo cha kuponyesha! Inashauriwa mtu atumie dose ya siku 14 hata ikibidi na zaidi. Halfu iko combination ya dose mbalimbali, hivyo ikikataa moja unajaribu nyingine. Mambo mengine: 1: Anatumia dose kama inavyohitajika? Nauliza hivyo kwa sababu kuna watu wengine ni waoga dawa na anaweza kunywa siku kadhaa halafu akaachilia mbali. Tena unakuta ni mtu mzima kabisa na anajifanya kumeza kumbe hamezi. Hili nalo usilidharau. 2: Dawa anazotumia mna uhakika nazo? Siku hizi kuna dawa nyingi fake. Nunua dawa kwenye maduka yanayoaminika. 3. Una uhakika hapati uambukizo mpya? Hawa bacteria wanaambukiza kwa njia ya kula mboga au matunda yenye vimelea, au kutozingatia usafi wakati wa kutoka chooni au hata kama ana mpenzi/mume/mke anaweza kuwa namwambukiza. Na mwisho anapima na kupata matibabu sehemu ya uhakika? Bongo achana nayo kabisa ina hospital nyingi sana hawajui kupima.
Kwangu mimi naona kama tatizo lake kubwa huenda ikawa sehemu anazotibiwa siyo sahihi i.e. anatibiwa vi-hospital visivyo na utaalam wa kutosha. Hao bacteria kama ukienda hosptal yenye wataalam wanaisha. Halafu jambo muhimu ajaribu kuachana haya matibabu ya mtaani. Atajikuta anaongeza matatizo badala ya kupunguza. 1: Combination ya Amoxicillin 1000mgx2, clarithromycin 500mgx2 na lansoprazol 30mgx2 kwa siku 14 ni standard ya matibabu. Au mbadala wake ni combination ya: Tinidazole, clarithromycin na Lansoprazole. Lakini usijinunulie dawa bila kupima sehemu inayoeleweka na dr akuandikie!Duuuuh ngoja nimuulize maana katumia dawa hadi huruma ....Mimi niliona moja inaitwa Omeplazole kitu kama hicho....
mkuu nakushauri mimi nilikuwa nalo hilo sema sio mda mrefu kama wewe kabla ya yote, nenda kanunue dawa za amoeba meza, hata siku mbili haziishi itakuwa sawa. niamini kama ukifata ushauri wangu naomba marejesho. maana mimi nilisumbuliwa hadi nalia kama mtoto mateso yake asikuambie mtu na unaenda hosp dokta anakuambia haoni tatizo ila saizi niko sawa kabisa japo kuna madogo madogo ya ku fix.Nakuja kwenu wanajamvi kuomba msaada wa mawazo nifanyeje niweze kuondokana na tatizo hili sugu na lililonitesa kwa miaka 22 sasa.
Tatizo hili liligunduliwa kwa mara ya kwanza mwaka 1995 hospitalini na nikaanza kutumia dawa na kufuata masharti mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuepuka aina fulani za vyakula na madawa na pia kubadili lifestyle.
Nikiri kuwa baada ya muda fulani baada ya kuanza matibabu nilipata nafuu kubwa hadi husahau maumivu ya tatizo hili lakini nilijitahidi kubaki katika masharti yale.
Baadaye tatizo lilianza upya na nikaanza kutumia dawa zile zile nilizotumia awali lakini sikupata nafuu. Nimebadilisha dawa mbalimbali lakini bado tatizo limeng'ang'ania. Baadhi ya dawa ninazokumbuka nilizotumia mpaka sasa ni: CIMETIDINE, RANITIDINE, OMEPRAZOLE, PANTOPRAZOLE, LANSOPRAZOLE na Antiacids za maji kama MILK OF MAGNESIA na RELCER GEL.
Nimewahi pia kutumia dawa za kienyeji kadhaa bila mafanikio. Mfano: Unga wa mbegu ya parachichi, mafuta ya ubuyu, asali mbichi na mdalasini, kuchemsha mmea wa mbigili n.k.
Nimeshawahi pia kupima H.PYLORI TEST mara 2. Mara moja nilikutwa Positive nikapewa HELIGO KIT dozi ya wiki 2 na nikaendelea na lansoprazole kwa wiki 2 zaidi. Nilipopima tena H.PYLORI ikasoma Negative lakini bado nikindelea kuumwa.
Mwaka jana nilifanyiwa kipimo cha OESOPHAGOGASTRODUODENOSCOPY hospitali moja ya rufaa na ripoti ya Daktari ilisomeka: "Multiple wounds found around the duodenum". Nilipewa dawa lakini bado sikuona nafuu kubwa.
Hivi leo nina siku ya 6 natumia TINIDAZOLE, LANSOPRAZOLE NA CLARITHRIMYCIN kwa pamoja na bado sijisikii nafuu yoyote. Maumivu ni makali, tumbo linauma na kutonesha (painful & tender), nikila chakula kidogo tu nasikia tumbo limejaa. Siwezi kulalia ubavu wa kulia tena sababu ya maumivu.
Usiku wa leo tumbo liliniuma sana mpaka jasho likanitoka japo kulikuwa na baridi.
Kwa ufupi nateseka jamani na nimekuja kwenu kama kuna mhanga kama mimi aliyewahi kuugua tatizo hili na kupona au madaktari mliomo humu jamvini mnisaidie jinsi ya kufanya.
Natanguliza shukurani nikiomba radhi pia kwa post ndefu. Nimelazimika kuandika hivi ili tatizo langu lieleweke vema.
ASANTENI!
Mwanajamvi mwenzenu anayeteseka.
Naomba huo ushauri mwingine unaweza nisaidiaNdugu hebu tupe mrejesho kama uliweza pata tiba, kama bado nikupe ushauri mwingine.
Ulitafuna matango na maganda yake kwa utaratibu upi ?Nilianza kula kwa wakati na kutafuna matango yakiwa na maganda yake ilinisaidia sana kwa sasa nimepona kabisaaaa