Kuna kitu yaitwaWakuu habari za leo, nina ndugu yangu anasumbuliwa sana na vidonda vya tumbo tangu mwaka 1993 alipopima na kugundulika kuwa ana matatizo hayo.
Ombi langu kwenu kama kuna mtu anafahamu dawa ya vidonda vya tumbo hata kama ya kienyejei naomba msaada wenu wa wapi inapatikana na kiasi gani. Alishatumia dawa za aina mbalimbali mpaka ile dozi kubwa ya HELIGO KIT, lakini bado.
Naomba msaada wenu!
pole dada sikuona hii mapema, ulibahatika pata tiba?Naomba huo ushauri mwingine unaweza nisaidia
Ya kweli hayaNitangulize pole kwa wale wote ambao mmekuwa mkiteseka kwa maradhi haya.
Nipende kukiri kuwa mimi sio mtaalamu wa masuala ya tiba,ila kutokana na usaidizi wa maelezo ya aliyekuwa "mhanga'' wa maradhi haya na sasa amepona naiweka kwenu tiba kama ifuatavyo;
1. MAHITAJI
1. Asali halisi - ½ lita.
2. Vitunguu thomu - ½ kg vilivyomenywa.
3. Habbat sauda - ya unga vijiko 3 vya chakula au ya mafuta vijiko 2 vya chakula.
4. Mdalasini wa unga - kikombe kimoja cha chai.
2. UANDAAJI
Vitunguu thomu lazima vitwangwe.
Kisha,changanya items zote ktk chombo kimoja,safi.
(Kwa mchanganyiko mzuri,unaweza kutumia kipekecho/ blenda)
Baada ya mchanganyiko huo ambao utakuwa uji mzito,hifadhi katika chombo safi na salama kitakachokupa uhuru wa matumizi,it can be a jar.
3. MATUMIZI
Tumia kijiko kimoja cha chakula 1 x 3 kila siku. Mchanganyiko huo ukiisha unaweza kuandaa mwingine,kulingana na maendeleo yako.
Maelezo niliyoyaweka hapa ni kwa mujibu wa aliyekuwa mgonjwa wa ulcers kama nlivyotangulia kusema,na sasa amepona kabisaaa,hana miiko tena, anakula hadi ndizi za kupikwa,maharage aina zote na pilipili anatafuna bila shida yoyote.
Ikiwa una lenye faida,usiwanyime na wengine.
Wasalam.
Vema.Asante kwa darasa mkuu, siye wahitaji ngoja tujaribu.
Asante pia.Asante mkuu. Nimekua nahitaji hii
Kuhusu asali mi sipingi kabisa, nimetumia asali pekee mwezi mzima asubuhi na jioni kila siku, ajabu sasa hivi sisikii hata dalili, aisee asali noma! na ukichanganya na huo mchanganyiko wa mtoa mada si ndo inakua tiba kamili kabisa.Ahsante sana kwa somo zuri.
Kabisa!Kuhusu asali mi sipingi kabisa, nimetumia asali pekee mwezi mzima asubuhi na jioni kila siku, ajabu sasa hivi sisikii hata dalili, aisee asali noma! na ukichanganya na huo mchanganyiko wa mtoa mada si ndo inakua tiba kamili kabisa.
Hiyo namba 3, Habbat sauda ni kitu gani, unaweza tupa jina jingine kama hutojaliNitangulize pole kwa wale wote ambao mmekuwa mkiteseka kwa maradhi haya.
Nipende kukiri kuwa mimi sio mtaalamu wa masuala ya tiba,ila kutokana na usaidizi wa maelezo ya aliyekuwa "mhanga'' wa maradhi haya na sasa amepona naiweka kwenu tiba kama ifuatavyo;
1. MAHITAJI
1. Asali halisi - ½ lita.
2. Vitunguu thomu - ½ kg vilivyomenywa.
3. Habbat sauda - ya unga vijiko 3 vya chakula au ya mafuta vijiko 2 vya chakula.
4. Mdalasini wa unga - kikombe kimoja cha chai.
2. UANDAAJI
Vitunguu thomu lazima vitwangwe.
Kisha,changanya items zote ktk chombo kimoja,safi.
(Kwa mchanganyiko mzuri,unaweza kutumia kipekecho/ blenda)
Baada ya mchanganyiko huo ambao utakuwa uji mzito,hifadhi katika chombo safi na salama kitakachokupa uhuru wa matumizi,it can be a jar.
3. MATUMIZI
Tumia kijiko kimoja cha chakula 1 x 3 kila siku. Mchanganyiko huo ukiisha unaweza kuandaa mwingine,kulingana na maendeleo yako.
Maelezo niliyoyaweka hapa ni kwa mujibu wa aliyekuwa mgonjwa wa ulcers kama nlivyotangulia kusema,na sasa amepona kabisaaa,hana miiko tena, anakula hadi ndizi za kupikwa,maharage aina zote na pilipili anatafuna bila shida yoyote.
Ikiwa una lenye faida,usiwanyime na wengine.
Wasalam.
Asante mkuu. Nimekua nahitaji hii
Kumbe na wewe ni mhanga? Pole Sana
Viliniishaga naona vimerudi kwa kasi. Toka jumapili mpaka leo nahangaika navyo