Ugonjwa wa Vidonda vya Tumbo (Peptic Ulcers Disease): Kinga, tiba na ushauri

Ugonjwa wa Vidonda vya Tumbo (Peptic Ulcers Disease): Kinga, tiba na ushauri

Mkuu hio ni sample wamechukua vinyama tumboni, wamefanyia culture kama sikosei. Sion sababu ya kurudia. Anyway sio wazo baya pia naweza rudia kesho tena.Asante
Rudia kipimo cha H-Pylori na kula sana Mboga za majani na matunda hasa tikiti maji na Avocado pia tumia zaidi vyakula vya majimaji
dah mkuu mm nlikuwa na kama yako but mwisho wa siku nilipoba kwa dawa za asili
Mkuu tushirikishe ulitumia dawa gani tafadhali.
Asante
 
Kabeji
Kunywa juisi ya kabeji mbichi baada ya kuikatakata vipande kisha isage kwenye mashine ya kutengenezea juisi (Blender). Baada ya hapo pima kwenye kikombe kimoja cha chai na unywe mara nne kwa siku. Tiba hii inaweza kutibu tatizo la vidonda vya tumbo kwa muda wa siku kumi. Kumbuka kuzingatia masharti ya msingi yaliyoainishwa hapo juu.

Asali
Asali ina chembechembe za asili zenye kuua bacteria na virusi ambazo vina uwezo wa kuua helicobacter Pylory ambao ni wadudu wanaosabisha ugonjwa huu kitu kinachomaanisha kuwa ina uwezo wa kutibu vidonda vya tumbo. Kingine ni kwamba asali huweza kulainisha umio, mfuko wa chakula na utumbo hivyo huweza kufunika vidonda vilivyopo tumboni.

Kutokana na kufunika vidonda maumivu ya kuchoma pamoja na dalili nyingine za vidonda vya tumbo hupungua.

Asali pia huweza kusafisha uvimbe na kusafisha vidonda ambavyo hujitokeza kwenye njia ya chakula. Asali inayopaswa kutumika kwa kusudio hili inapaswa iwe mbichi na isiwe imeongezewa vitu vingine na dozi yake ni vijiko vya chakula viwili mpaka vitatu kwa siku.

Vitunguu Swaumu
Viungo hivi ni tiba nyingine inayofaa sana katika kutibu vidonda vya tumbo kutokana na kemikali zinazoua wadudu pamoja na virusi zilizomo ndani yake na hivyo huweza kupambana na kuua bacteria wanaosababisha vidonda vya tumbo.

Viungo hivi hufahamika kwa kusaidia katika kutibu vidonda vya tumbo hata pale vinapotumika vikiwa vimechanganywa na vyakula vingine kutokana na nguvu nyingi iliyomo ndani yake pamoja na chembechembe zenye kuamsha na kuboresha mwili zilizomo ndani yake ambazo huwezesha kuukinga mwili dhidi ya maambukizi kama vile vidonda vya tumbo.

Hivi ndivyo unavyopaswa kutumia vitunguu swaumu kwa ajili ya kutibu tatizo hili:
Kula punje tatu mpaka nne za kiungo hicho kwa siku zikiwa zimechanganywa na kijiko kimoja au viwili vya asali kwa siku.
 
mimi niliumwa au tuseme bado naumwa vidonda but now niko na afadhali sana, nilikutana na DK mmoja wakati narudi Dar es salaam kutoka mkoa fulani kwenye basi(Chaula), yule Dk alipanda akaongeaongea na abiria na kuelezea dawa nyingi mno but mimi nilimsikiliza zaidi alipofika kwenye vidonda,

Alisema 'dawa ya vidonda unachukua yale matunda ya parachichi 10 kwa wale ambao vidonda havija anza kusumbua sana, unayakausha juani mpaka yanabadilika rangi na kua meusi ivi, then unasaga utapata unga unga, ule ungaunga unakua unachukua kijiko kimoja kikubwa unachanganya na glas moja ya maziwa (alisema kwa ubora zaidi yawe maziwa ya ngamia) but hata ya ng'ombe sio mbaya.

Tthen kwenye huo mchanganyiko unaweka asali mbichi kipimo utakachoona kinakuwezesha kunywa huo mchanganyiko bila tabu maana huo mchanganyiko unakua hauna ladha ndhuri. Kama ukiweza kunywa tu bila ya kuchanganya na asali(kwa upande wangu mimi sichanganyi na asali but huwa naramba asali after kunywa hiyo dawa).

nilitoka hapo na kuja kujaribu hii kitu na kiukweli imenisaidia sana. God bless you.
 
Nilitumia dawa za hospitali kwa miaka 3 mfululizo sikupona, ila nilitumia zile za natural sasa nimepona.

Mwanzoni majibu ya hospitali yalionesha ni vidonda, baadae majibu ya hospitali yakaanza kuonesha sina tatizo lolote huku hali ikiendelea kuwa mbaya ndio ikabidi nibadili teknolojia.
 
Pole sana mkuu ni ulcers hizo. Nami zimenitesa miaka 6 nilikua nasikia hivyo shauri ya vidonda vya tumbo. Kama unaweza nipatie namba yako PM utapona kabisa 100% kuna mama anatibu kienyeji maeneo ya Goba. Kama upo Dar.

Vidonda vibaya sana. Nilikua short tempered, kujamba sasa, tumbo linawaka moto sio kawaida, maumivu ya shingo na mgongo, kusahau isivyo kawaida na wakati nilikua mwepesi wa kumbukumbu. Yaani trust me utapona kabisa. Mimi pia nilifanya endoscopy pale Regency, na nikatumia dawa za hospital bila kupona kabisa.
 
Pole sana mkuu, mimi namfahamu mtu ambaye alikua kwenge stage mbaya sana ya vidonda alikua hawezi kula nyama, maharage etc akatumia dawa fulani ya kienyeji aisee sasa hivi anakula nyama na maharage ana feel amepona japo hajaenda kuconfirm hospitali.
 
Mkuu weka hio teknolojia na sisi tupate unafuu mkuu.hali mbaya
Nilitumia dawa za hosp kwa miaka 3 mfululizo sikupona,ila nilitumia zile za natural sasa nimepona,
Mwanzoni majibu ya hosp yalionesha ni vidonda,baadae majibu ya hosp yakaanza kuonesha sina tatizo lolote huku hali ikiendelea kuwa mbaya ndio ikabidi nibadili teknolojia

Sawa kaka nakuja PM unipatie hizo namba.Sema nilikua nashauri uweke hapa na wengine inaweza kuwasaidia mana wahanga tupo wengi.
Pole sana mkuu ni ulcers hizo. Nami zimenitesa miaka 6 nilikua na silka hizo shauri ya vidonda vya tumbo. Kama unaweza nipatie namba yako PM utapona kabisa 100% kuna mama anatibu kienyeji maeneo ya Goba. Kama upo Dar.

Vidonda vibaya sana. Nilikua short tempered, kujamba sasa, tumbo linawaka moto sio kawaida, maumivu ya shingo na mgongo, kusahau isivyo kawaida na wakati nilikua mwepesi wa kumbukumbu. Yaani trust me utapona kabisa. Mimi pia nilifanya endoscopy pale Regency, na nikatumia dawa za hospital bila kupona kabisa.


Alitumia dawa gani mkuu.Mshauri akapime tena
Pole sana mkuu, mi namfahamu mtu ambae alikua kwenge stage mbaya sana ya vidonda alikua hawezi kula nyama, maharage etc akatumia dawa fulani ya kienyeji aisee sasahivi anakula nyama na maharage ana feel amepona japo hajaenda ku confirm hospitali.

Mkuu hii nimewai kuitumia. Sio haba ilinisaidiasaidia. Nitarudia tena
Mkuu Ushimen

Nakuunga mkono kabisa. Hiyo smooth ya Kabeji ni tiba kabisa na fast reliever ya maumivu ya tumbo ikitumika kikamilifu.
 
Ambition plus,Asee nikushauri kwa uzoefu, kwanza kunywa juice ya cabbage mara mbili au zaidi kwa siki, tiba ya uhakika kabisa hiyo mzee, unaweza ukanganya na carrot unapo blend, fanya hiyo kwa anagalu wiki tu utaona utofauti mkubwa,

jipe likizo ya vitu vya gesi, mananasi, maziwa fresh acha kabisa, carbonated drinks zote achana nazo,

kunywa juice tu ya embe, kula ndizi mbivu, parachichi, papai n.k,

kwa sasa punguza wali kwa anagalau wiki moja,

punguza hasira na stress

halafu ukishapata nafuu, anza kuwa unakula pilipili (usishangae ni dawa pia) itakusaidia kukata naumivu baada ya muda
 
Nitakujibu na ukifata ushauri huu utapona kabisa within 2 moths.
Kwa jinsi nilivyosoma maelezo yako unaweza kuwa na leaky gut na hii imepelekea SIBO (Small intestine bacterial overgrowth).

Leaky gut kwa maelezo rahisi ni kwamba chekecheke la utumbo wako ambamo ufyonzaji wa viini lishe hufanyika limelegea na hivo kuruusu vitu visivyotakiwa kupenya vipenye, incluiding harmful bacteria.
Changamoto ikiwa ya muda mrefu hupelekea imbalance ya microbiome tumboni.
Microbiome kwa luga rahisi ni kwamba tumboni kuna bacteria wazuri na wabaya, bakteria wazuri ni kinga na pia wanaahusika katika digestion, imbalance yetu tunaongelea ni kwamba bakteria wabaya kuwa wengi kuliko bakteria wazuri.

Sasa unapotaka kusolve swala la leaky gut inabidi uwe strict sana kwenye swala la lishe:

1.ONDOA vyakula vyote ambayo vinaharibu gut(mfumo wa chakula), vitu hivi ni kama vyakula vilivyosindikwa+vinywaji, vyakula vya ngano,antibiotics, vionjo mbalimbali vya kiwandani, mafuta yaliyosafishwa ie margarine.

2. RUDISHA vyakula vya kuimarisha mfumo wa chakula.Vyakula hivi ni kama ifuatavyo:
  • Supu ya mifupa ( bone broth) kama unaweza kuotengeneza ama ukapata mahali wanaipika.
  • Maziwa mtindi ya asili. Achana na yale ya kwenye pakiti. Maziwa mtindi tunasema yana probiotics ( probiotics ni viumbe wadogo ambao wana uwezo wa kutibu mfumo wako wa chakula). Maziwa yanapoferment yanatengeneza live becteria ambao ni wazuri kwa gut yako.
  • Mboga za majani, zipikwe kidogo sana . Ama ukiweza tengeneza juisi ya mbogamboga hii itaharakisha mchakato wa kupona. Juisi ya mboga inapromote good bacteria growth.
  • Bidhaa za nazi. Mfano mafuta ya kupikia ya nazi ( haya yatumie kama kiungo chako). Mafuta ya nazi tunasema yana aina ya fat ambazo tunaita ni medium chain fatty acid ambazo ni rahisi kuchakatwa (digested) ukilinganisha na mafuta mengine, ukikosa mafuta ya nazi basi pikia mafuta ya olive.
  • Vyakula vyenye mafuta mazuri kama: parachichi,mbegu za maboga , mayai nk. Vitasaidia kuharakisha uponaji wa gut yako.

Anza kufatilia then utanipa majibu.
NB: mimi siyo daktari kwahiyo kuna mahali naweza kuwa nimekosea, wale vipanga mnaruusiwa kunisahihisha.
 
Yes kama nikila embe,nanasi, (citrus zote)soda,majuis ya dukani,vitu vya baridi,viazi,nyama yaani kifupi sina chema tumbo linanivuruga wakati wote.Nikila kidogo tumbo linajaa gesi.Nimekua mkali kama pilipili.kila saa mahasira.Na mind vitu vya kijinga hadi wakati mwingine najishangaa
kwa uelewa wangu ukishakuwa na vidonda vya tumbo tumbo inatakiwa uangalie sana mfumo wako wa maisha hasa katika ulaji

haujafikia hatua mbaya, yaani kutapika damu

usile vitu vinavyoleta gesi mf maharage,na jamii ya mikundekunde,usile vipolo chakula chochote kilicho lala
usinywe kabisa vinywaji vya kiwandani vina acid,pendelea kutumia juice fresh ya kutengeneza nyumbani

pendelea kunywa maji glas moja dk 10 kabla ya kula

ktk mboga za majani usile mboga ya maboga(majani yake)

pendelea kutumia dawa za asili mf juice ya kabich ni nzuri sana unakunywa glas moja asubuhi na jioni 1,juice ya carrot etc.

kama za hospital zimeshindwa jaribu dawa za kienyeji au asili na uangalie ulaji wako utapona

vitu vingine muda mwingine vya kiroho zaidi fanya maombi au upatiwe huduma ya maombi,unaweza hisi ni vidonda vya tumbo kumbe siyo kwa upande wa pili

utapona.

In Shaa Allah.
 
Yaani hio juice ya cabbage inachanganywa na maji mkuu au?
 
2011 nilikuwa na tatizo kama lako. Likaisha waliniandikia midawa mingi nikashindwa nikaitupilia mbali likaisha tatizo
 
Back
Top Bottom