Nitakujibu na ukifata ushauri huu utapona kabisa within 2 moths.
Kwa jinsi nilivyosoma maelezo yako unaweza kuwa na leaky gut na hii imepelekea SIBO (Small intestine bacterial overgrowth).
Leaky gut kwa maelezo rahisi ni kwamba chekecheke la utumbo wako ambamo ufyonzaji wa viini lishe hufanyika limelegea na hivo kuruusu vitu visivyotakiwa kupenya vipenye, incluiding harmful bacteria.
Changamoto ikiwa ya muda mrefu hupelekea imbalance ya microbiome tumboni.
Microbiome kwa luga rahisi ni kwamba tumboni kuna bacteria wazuri na wabaya, bakteria wazuri ni kinga na pia wanaahusika katika digestion, imbalance yetu tunaongelea ni kwamba bakteria wabaya kuwa wengi kuliko bakteria wazuri.
Sasa unapotaka kusolve swala la leaky gut inabidi uwe strict sana kwenye swala la lishe:
1.ONDOA vyakula vyote ambayo vinaharibu gut(mfumo wa chakula), vitu hivi ni kama vyakula vilivyosindikwa+vinywaji, vyakula vya ngano,antibiotics, vionjo mbalimbali vya kiwandani, mafuta yaliyosafishwa ie margarine.
2. RUDISHA vyakula vya kuimarisha mfumo wa chakula.Vyakula hivi ni kama ifuatavyo:
- Supu ya mifupa ( bone broth) kama unaweza kuotengeneza ama ukapata mahali wanaipika.
- Maziwa mtindi ya asili. Achana na yale ya kwenye pakiti. Maziwa mtindi tunasema yana probiotics ( probiotics ni viumbe wadogo ambao wana uwezo wa kutibu mfumo wako wa chakula). Maziwa yanapoferment yanatengeneza live becteria ambao ni wazuri kwa gut yako.
- Mboga za majani, zipikwe kidogo sana . Ama ukiweza tengeneza juisi ya mbogamboga hii itaharakisha mchakato wa kupona. Juisi ya mboga inapromote good bacteria growth.
- Bidhaa za nazi. Mfano mafuta ya kupikia ya nazi ( haya yatumie kama kiungo chako). Mafuta ya nazi tunasema yana aina ya fat ambazo tunaita ni medium chain fatty acid ambazo ni rahisi kuchakatwa (digested) ukilinganisha na mafuta mengine, ukikosa mafuta ya nazi basi pikia mafuta ya olive.
- Vyakula vyenye mafuta mazuri kama: parachichi,mbegu za maboga , mayai nk. Vitasaidia kuharakisha uponaji wa gut yako.
Anza kufatilia then utanipa majibu.
NB: mimi siyo daktari kwahiyo kuna mahali naweza kuwa nimekosea, wale vipanga mnaruusiwa kunisahihisha.