Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 17,434
- 27,177
Wanaume wengi, hasa Dar wamebaki na sehemu za kukojolea na si kuzalishia tena, hii inatokana na life style . Chips mayai ya kisasa, Mayonaise, biriani, pombe-visungura na streess za kuliwa betting!
Wakati Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ikipanua huduma zake za Upandikizaji Mimba (IVF), Madaktari wanasema ubora hafifu wa Mbegu za kiume na idadi ndogo ya Mbegu miongoni mwa Wanaume ni changamoto kubwa zinazokabili mpango huo.
Kwa mujibu wa Wataalamu, karibu theluthi mbili (2/3) ya visa vya Ugumba vinavyotibiwa katika kituo hicho vinatokana na Wanaume, ikijumuisha kutokuwa na Mbegu kabisa, idadi ndogo ya Mbegu, uwezo duni wa Mbegu kuogelea au umbo lisilo la kawaida la Mbegu.
Baadhi ya Wanaume huonekana kuwa na afya njema lakini vipimo hufunua matatizo makubwa ya Uzazi, mara nyingi yakihusishwa na Mtindo wa maisha kama vile matumizi ya Pombe, uvutaji sigara, Msongo wa mawazo, ukosefu wa usingizi wa kutosha na matumizi ya dawa za kulevya.
Utafiti mkubwa wa Kimataifa uliochapishwa katika Jarida la 'Human Reproduction Update' unabainisha kuwa uwezo wa Wanaume kuzalisha idadi nzuri ya Mbegu za kiume Duniani umeshuka kwa zaidi ya 50% kati ya mwaka 1973 na 2018, huku kasi ya kupungua ikiongezeka mara dufu hadi kufikia 2.6% kwa mwaka tangu mwanzoni mwa karne ya 21.
Tujadili.