Ugumu anaoupitia Harmonize ni kielelezo tosha kwanini sanaa yetu haikui. WCB inaua wasanii nje ya lable yao

Wasipokuelewa hadi hapo waendelee tu kulalamika na ku hate AF
 

Hyo ndo game ya muziki... sijaelewa hapo unaposema BURNABOY kaachiwa nafasi? ...ina maana wengine hawafanyi tena muziki? ....... mwambieni msanii wenu atoe ngoma kali na ajitume otherwise acheni majungu na kutafuta huruma .... halafu usilazimishe kila mtu apende unachotaka wewe!!! na unapoongea ni vizuri ukawa na ushahidi na akiba ya maneno mana sidhani kama YOUTUBE wakikwambia uthibitishe kwamba wao hawa post hzo shows za konde boy utakuwa na huo ushaidi!?

Fanya kazi kijana acha majungu.
 
Watu wengine hata sielewagi akili zao zipoje,mtu anaanzaje kusema wanigeria wanaachiana kufanya muziki seriously?,ndio hizo sababu wanazoletaga hapa eti Diamond mbinafsi anataka kuwa juu peke yake au hawaachii wenzake nao wakue international artist wakubwa kama yeye,music ni biashara kila mtu anakula kutokana na bidii yake, Diamond kawaonyesha njia wasanii wengi wa Tanzania lakini wao wanataka waachiane, sijawahi ona popote pale duniani,Huko Nigeria fikiria miaka mitatu au minne nyuma ambapo watu kama kiss Daniel,tiwa savage,korede bello,harrysong,olamide,patoranking,davido, Wizkid,p square,na wengine walipokuwa ktk peak ya hali ya juu,mtu anaanzaje kusema wanigeria wanaachiana?, harmonize aache kutafuta huruma za watu ajue kuwa 90 asilimia ya mashabiki wake ni wale waliokua WCB,hao asilimia kumi wote ni haters wa Diamond na WCB kwa ujumla, kutafuta huruma hakumsaidii,atoe nyimbo kali zaidi watu watamkubali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kaka me ktk hao wa TZ mil 50 nitoe...sijawah taka msanii awe DIAMOND peke yake kwanza SIMUELEWI naona anapiga kelele tu na kaanza na wizi siku hizi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Exactly.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ulikua mzuri sana kila mtu alipewa nafasi yake kwa ukali wake.
Ndo mana unaona hata diamond amefika alipofika
kwa sasa kuna namna mziki umetengenezwa haupendezi tena
Kivipi,ilisemekana muziki haukui kwa kuwa unadhibitiwa na Ruge(RIP). Huyo Diamond amepambana huku media karibia zote hazipigi nyimbo zake na hakukata tamaa, vita vyake na Ruge(clouds in general) nilikuwa nam-support Ruge kwani kwake vita ile ilikuwa ya kibiashara na haikuwa personal. Hali kadhalika hapa Harmonise apambane kwani hii ni biashara ya muziki na biashara ni vita,mambo ya ujamaa kwenye biashara hayapo.
Ameamua kujitegemea aache kulialia na kibaya zaidi aache kujilinganisha na mtu, mashabiki ndiyo watamuweka katika kiwango anachostahili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huku Tz tunapambana kushushana yaani mpaka media za YouTube hazipost show za harmonize ili tu akose mvuto.
Yaani mashabiki wa Harmonize wana akili sawa na mashabiki wa Kiba, and possibly, tunaodhani ni mashabiki wa Konde ni wale wale wa Kiba!! Hizo media unazosema hazi-post ngoma za Konde kisa WCB ni media zipi?! Unamaanisha hivi v-blog uchwara ambavyo havijafikisha hata Subscribers 100K, au?! Ikiwa Konde mwenyewe channel yake ina takribani ya Subscribers 1.5M na bado Views zinasua sua; hivi unaamini ki-blog uchwara chenye Subscribers chini ya 100K ndo zita-boost Views za Konde? Btw, hivi unaamini kabisa kwamba majority ya subscribers wa hivi v-blog hawaja-subscribe channel ya Konde?

Ngoja nikusaidie kitu kimoja, ambacho watu wa Digital Makerting wanakifahamu!! Hapa nitakuonesha Data Analysis ya Mond, Harmonize na Millard Ayo


Hapo juu ni Data Analytics ya Konde's Instagram Account! Hapo unaambiwa kwamba 82% ya Instagram Followers wa Konde Boy pia wamem-Follow Diamond! Kwa maana nyingine, 82% ya Followers wa Konde wametokana na Followers wa Mond!!

Sasa tuangalie akaunti ya Diamond:-


Utaona hapo Instagram Account ya Diamond haina common followers na Harmonize bali ana common followers na hao wanne tu!! The question is: WHY wakati tumesema 82% ya Followers wa Harmonize wapo pia kwa Diamond na hapa tunasema Diamond hashei followers na Harmonize!!!

Jibu ni kwamba, Diamond amejiunga Instagram July 30, 2012 wakati Konde kajiunga December 14, 2014. Sasa hiyo 82% ni kwa sababu Followers wale wale wa Diamond ambae alijiunga mapema zaidi, ndiyo wakam-follow Harmonize ambae by the time hakuwa na followers!

Mtu kama Millard ana-share 56% na Diamond kwa sababu akaunti ya Ayo nayo ni ya muda mrefu; August 06, 2012; na kwahiyo kuna Followers walianza kum-follow Ayo ndipo wakaenda kwa Mond!!!

MAANA ya hiyo analysis ni kwamba, Harmonize HANA followers wa kutosha wa kwake mwenyewe bali 82% ya Followers wake wametokana na Diamond! Majority ya hawa ni mashabiki wa Diamond na Wasafi! Baada ya Harmonize kuondoka Wasafi, asilimia kubwa ya Followers wake ambao wanatokana na Diamond/Wasafi, hivi sasa hawahangaiki kumaliza bundle zao kwenda ku-watch videos zake!!

So, hiyo ndiyo sababu na maelezo mengine yote, kama vile eti anabaniwa, mara sijui Youtube Media hazi-post, yote hayo ni POROJO tu!! Kwahiyo fanyeni kazi na achaneni na tabia za kutafuta public sympath, kama zile za Konde kutangaza kwamba kuzuiwa kwa shoo yake Mbeya kulikuwa na mkono wa mtu!!!!!
 
Mzee baba umeua umemaliza kila kitu asipokuelewa basi.
 
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…