Ugumu wa ajira Kwa wanafunzi wa SUA

Ugumu wa ajira Kwa wanafunzi wa SUA

Na hapa unasemaje?
Screenshot_20240713-214227.jpg
 
Sitasahau nilipokwenda kusoma mahali fulani. Test ya kwanza kabisa nikiwa mgeni mgeni nikagonga 82% mwamba nikasema Yes hawa wenye pua ndefu hawa watanikoma. Kuja kuangalia mwishoni kwenye comments kidogo nianguke. Kumbe 82% sijui ni C+/B- dah! Na comments mbaya kweli kutoka kwa Prof. Ndiyo nikajua kuwa hawa watu wako siriazi sana na elimu yao hawa. Eti A- inaanzia 92%! Kufa sikufa ila cha moto nilikiona kwa kweli hasa mwaka wa kwanza! 🙌
 
Duh hatari mkuu
 
Hivi huo mfumo wa kuajili kwa kuangalia results badala ya ujuzi na cheti bado upo?.
Kwa hawa wanaosoma kwa kuunga unga madesa hawa hawajisomei na hawajui kitu mbali na kukariri ujuzi wataupata wapi? Graduate wa chuo kikuu lakini utafikiri mmemwokota barabarani. Au huijui elimu yetu ilivyo hoi bin taaban? Wameruhusu vyuo vikuu vingi bila kuwa na PhDs za kutosha matokeo yake mtu mwenye masters tena ya kuunga unga ndiyo anafundisha wanafunzi 500+. Unategemea nini hapo? Ndiyo maana makampuni mengi yanapiga makelele kwamba graduates wetu hawaajiriki!

The situation is dire!
 
SUA ni chuo cha hovyo chenye kujifanya kina pass mark za juu.

Hivi unajua hiyo 50 wengi huwa ni 40 mnaongezewa?

Nimewahi kuwashauri hilo ila wale viongozi watoto wao hawasomi hapa hivyo hawajali,UE wametoa masaa 3 imekuwa 2 bila maelezo yoyote?

Unawezaje kupunguza muda wa kufanya UE bila taarifa kwa wanafunzi na guide books zipo?

Sua wanatakiwa kubaki na kozi za kilimo tu.
Me nilikuwa na wazo kuhusu pass mark kwa vyuo vikuu Kwa mfano pass mark ya SUA ni 50+ambayo ni 40-49D
50-59 ni C
60-64 B
65-69B+
70-100A

Hii inawapa wakati mgumu vijana kwenye ajira Kwa mfano mtu mwenye G.P.A ya 3.5 SUA vyuo vingine anakuwa na G.P.A ya 4.3.

Kwahyo kwenye qualifications za GPA mwanafunzi wa SUA tiyari kigezo cha GPA kinanamtoa nje, hizi pass mark zinaumiza sana wanafunzi na kwenye competition za ajira wanafunzi wanapata ugumu sana .

Pass mark inabidi iwe moja ili kuleta usawa kwa vyuo vyote
 
Danganya wajinga!

Mimi nawajua wahitimu wa Sua kwa uongo mlioaminishwa hapo mazimbu na magadu.

Sua naijua nje ndani,na zaidi ya hapo naijua pia.

Hiki chuo kwa magumashi ni namba one tanzania,elimu iko chini ya kiwango.
Wewe mwanachuo unafundishwa kuendesha trekta
Unafundishwa kufuga samaki
Unafundishwa kufuga kisasa
Unafundishwa kilimo ikolojia
Unaishi morogoro kwann ukae mtaani
 
Back
Top Bottom