Ugumu wa ajira Kwa wanafunzi wa SUA

Sitasahau nilipokwenda kusoma mahali fulani. Test ya kwanza kabisa nikiwa mgeni mgeni nikagonga 82% mwamba nikasema Yes hawa wenye pua ndefu hawa watanikoma. Kuja kuangalia mwishoni kwenye comments kidogo nianguke. Kumbe 82% sijui ni C+/B- dah! Na comments mbaya kweli kutoka kwa Prof. Ndiyo nikajua kuwa hawa watu wako siriazi sana na elimu yao hawa. Eti A- inaanzia 92%! Kufa sikufa ila cha moto nilikiona kwa kweli hasa mwaka wa kwanza! šŸ™Œ
 
Duh hatari mkuu
 
Hivi huo mfumo wa kuajili kwa kuangalia results badala ya ujuzi na cheti bado upo?.
Kwa hawa wanaosoma kwa kuunga unga madesa hawa hawajisomei na hawajui kitu mbali na kukariri ujuzi wataupata wapi? Graduate wa chuo kikuu lakini utafikiri mmemwokota barabarani. Au huijui elimu yetu ilivyo hoi bin taaban? Wameruhusu vyuo vikuu vingi bila kuwa na PhDs za kutosha matokeo yake mtu mwenye masters tena ya kuunga unga ndiyo anafundisha wanafunzi 500+. Unategemea nini hapo? Ndiyo maana makampuni mengi yanapiga makelele kwamba graduates wetu hawaajiriki!

The situation is dire!
 
SUA ni chuo cha hovyo chenye kujifanya kina pass mark za juu.

Hivi unajua hiyo 50 wengi huwa ni 40 mnaongezewa?

Nimewahi kuwashauri hilo ila wale viongozi watoto wao hawasomi hapa hivyo hawajali,UE wametoa masaa 3 imekuwa 2 bila maelezo yoyote?

Unawezaje kupunguza muda wa kufanya UE bila taarifa kwa wanafunzi na guide books zipo?

Sua wanatakiwa kubaki na kozi za kilimo tu.
 
Danganya wajinga!

Mimi nawajua wahitimu wa Sua kwa uongo mlioaminishwa hapo mazimbu na magadu.

Sua naijua nje ndani,na zaidi ya hapo naijua pia.

Hiki chuo kwa magumashi ni namba one tanzania,elimu iko chini ya kiwango.
Wewe mwanachuo unafundishwa kuendesha trekta
Unafundishwa kufuga samaki
Unafundishwa kufuga kisasa
Unafundishwa kilimo ikolojia
Unaishi morogoro kwann ukae mtaani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…