Ni ukweli mchungu kwamba mtaani hali ni ngumu sana kuanzia upatikanaji wa pesa mpaka bei za bidhaa. Binafsi, mbali na kwamba ni muajiriwa, lakini pia najishughulisha na biashara zinazogusa moja kwa moja wananchi, kwa hiyo ninachoandika nina kifahamu vizuri.
Kwa hali ilivyo sasa, anaweza tokea mtu au mwanaharakati akaunganisha watu kufanya maandamano makubwa sana ambayo yanaweza yasiishe salama.
Watanzania ni wapore sana, lakini njaa inaweza kumfanya mtu afanye chochote kile.
Hivyo, Bunge na serikali kwa ujumla, suala la ugumu wa maisha, hususani bei za vyakula, fanyeni kitu kupunguza ugumu huo.