Ugumu wa maisha ni jambo la kusadikika halipo kiuhalisia na sijawahi kuliona na halitatokea

Kwahio kila mtu ana basic needs ? (Chakula, Mavazi na Malazi) nadhani pamoja na gazeti lako ulikuwa unataka kusema kwamba ugumu wa maisha unatokana na uzembe wa mtu kutokurahisisha maisha yake...

Nami nakuuliza wale waliopo vitani sasa hivi..., au waliolima vanilla wakakosa masoko na hata kurudisha gharama ya kununua mbegu na hivyo kufirisika au wale wanaolipa kodi na matozo lakini watunga sera wanashindwa kuwaletea huduma au wale waliouza shamba na kusoma waje wawe wauguzi leo unawaambia wakauze uji.... (Je hao pia ni uzembe wao)?
 
Maisha magumu ni pamoja na mkulima wa Hanang mazao yake kuliwa baada ya mchunga ng'ombe wa Hanang kupitisha ng'ombe shambani kwake.
 
Maisha magumu ni mchungaji ng'ombe wa Hanang aliyepata mtaji wa kufungua biashara kulimbikiziwa kodi na tozo pindi anapoanza biashara tu.
TRA wanasikiliza mtu ambaye anafungua biashara unapewa msahama, wewe nenda kawaeleze ukweli jamaa wanapenda mtu mkweli
 
Maisha magumu ni pamoja na mchunga ng'ombe wa Hanang aliyegeuka fundi umeme kujenga nyumba yake kisha ikabomelewa akiwambiwa amevamia eneo la mtu au serikali.
 
Maisha magumu yanawekwa na viongozi wa nchi na nchi zinatoka kutawala wengine. Ila ukiingia level flani ya kujitambua unaweza kuona picha yote. Lakini ni wachache watafika huko.
 
Maisha magumu ni pamoja na mchunga ng'ombe wa Hanang aliyegeuka fundi umeme kufungwa kwa kesi ya kuiba vifaa vya umeme mahali alipopewa kazi ya ufundi umeme.
 
Maisha magumu ni pamoja na wachunga ng'ombe walioko Hanang kuumwa mbu msituni kuugua malaria na kushindwa kwenda hospital kupata tiba
Yapo majani ukiyala ladha ya damu inabadilika inakuwa kama na uchungu, baadhi ya vyakula ukila MBU hawakudhuru!
Mambo ya neti nimekuja kuyakuta mjini, miaka yote niko porini sijawahi umwa maralia mimi
 
Maisha magumu ni pamoja na mke wa mchunga ng'ombe wa Hanang kupotelewa na mume wake asijue alipo kama ameliwa na fisi porini, ametumbukia korongoni au ametekwa.
 
Yapo majani ukiyala ladha ya damu inabadilika inakuwa kama na uchungu, baadhi ya vyakula ukila MBU hawakudhuru!
Mambo ya neti nimekuja kuyakuta mjini, miaka yote niko porini sijawahi umwa maralia mimi
Kuna wachunga ng'ombe wengi wa Hanang wanaugua malaria kila siku.
 
Samico Tanzania 🇹🇿
 
Umeshawahi kuwa mtu mwingine ambaye ni tofauti kabisa na wewe?

Maana umetoa personal experience tu na kufanya kama vile kila mtu anaweza kuishi kama wewe.
Niwe mtu mwingine vipi wakati niliumbwa ili nije kuishi mimi na si mwingine!

Yaani umeumbwa kuwa JUMA ila wewe unataka uishi kama ROSE si ndiyo mwanzo wa mashoga kuwepo kwa style hii
 
Maisha magumu ni pamoja na mchunga ng'ombe wa Hanang kuporwa mifugo yake na wezi wa mifugo huko porini.
 
Maisha magumu ni pamoja na mchunga ng'ombe wa Hanang kuporwa mifugo yake na wezi wa mifugo huko porini.
Mimi nilikwambia yalinikuta mengi, Kuna siku nilikuwa porini wakaja watu na mapanga nikatimua mbio kuelekea nyumbani!
Kundi lote la mifugo lilitimua mbio kunifuata nyuma.. Mifugo wanauwezo wa kusoma alama ya hatari kutoka kwa mchungaji! Hilo nalo ni somo jinngine nitakuja kuwafundisha humu
 
Niwe mtu mwingine vipi wakati niliumbwa ili nije kuishi mimi na si mwingine!

Yaani umeumbwa kuwa JUMA ila wewe unataka uishi kama ROSE si ndiyo mwanzo wa mashoga kuwepo kwa style hii
Sasa mbona wewe unataka watu waweze kulazimisha waishi kama wewe wakati wao si wewe?

Yani wewe una miguu unaweza kutembea bila msaada, unalazimisha kiwete asiye na miguu atembee kama wewe? Unamshangaa kwa nini hawezi kutembea na kusema tatizo la mtu kushindwa jutembea halipo, kwa sababu wewe unaweza kutembea bila msaada?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…