Ugunduzi wa aina mpya za Dawa za Kulevya daily ni anguko kuu kwa Vijana

Ugunduzi wa aina mpya za Dawa za Kulevya daily ni anguko kuu kwa Vijana

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2021
Posts
1,147
Reaction score
2,008
Huko Sierra Leone Serikali imetangaza Matumizi ya Dawa za Kulevya Kuwa Dharura ya Kitaifa huku Rais Julius Maada Bio akitangaza Mapambano dhidi ya Mihadarati aina ya 'Kush'

Kush inatajwa kuwa na uraibu sawa na Bangi na tramadol na imekuwa ikitumiwa zaidi na Vijana wasio na ajira wakikabiliana na Umasikini na Ukali wa Maisha

Wataalam wa afya wanakataza matumizi ya Kush ambayo pia hujulikana na K2 kwa kuwa huathiri Ubongo na kusababisha Mtumiaji Kujiua.

Nchi za Afrika zinapambana na ongezeko la matumizi ya Dawa za Kulevya ambapo Vijana ni Waathirika Wakuu

Nchini Tanzania Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) ilikamata Kilogramu 4.623 za aina mpya ya dawa ya kulevya inayoitwa Methylene Dioxy Pyrovalerone (MDPV) Jijini Dar es Salaam ikisafirishwa na Raia wa Comoro (Ahmed Bakar Abdou (32).

Akiongelea tukio hilo Jijini Dar es Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo alisema Dawa hiyo ina kemikali inayoweza kuleta madhara ya haraka kwa Mtumiaji ikilinganishwa na dawa nyingine za kulevya na pia imeongezwa nguvu ya kilevi inayozidi cocaine, methamphetamine na heroin

Dawa hii ya kulevya huuzwa kwa njia ya mtandao (internet) na husafirishwa kupitia kampuni za usafirishaji vifurushi na hufichwa kwa kuwekwa chapa za majir bandia kama vile bath salts, Ivory Wave, plant fertilizer, Vanilla Sky, na Energy.

Chanzo chake ni nini? Ni kufeli kwa System za Udhibiti wa Dawa za Kulevya na Afrika na Duniani au ni nini?

Eitherway, ni muhimu changamoto hii itatuliwe mapema, vijana wanaangamia na tutashtuka wakati 90% ya Vijana watakuwa mateja

Ni lazima Serikali ije na mkakati wa Kunusuru Vijana hasa wakati huu ambapo tatizo la Ukosefu wa Ajira linazidi kuota mizizi

--------

Vyanzo: Millard Ayo, BBC


View: https://x.com/millardayo/status/1775909056802099391?s=46&t=CGt_zHZdoG4Dz50u37Hezg

Sierra Leone's President Julius Maada Bio has declared a national emergency because of the rampant drug abuse in the country.

Kush, a mixture of additive substances with similar effects to cannabis and tramadol, has been prevalent in the country for years - especially in urban areas.

"Our country is currently facing an existential threat due to the devastating impact of drugs and drug addiction, in particular the devastating synthetic drug kush," President Bio said in an address to the nation on Thursday.

"This deadly kush is taking a devastating toll on our communities."

He said his government was working to dismantle drug trafficking networks in the country.

The drug - which is also known as K2 - is easily accessible to unemployed young people seeking an escape from poverty and traumas of life.

Health experts warn that kush intake can lead to permanent brain damage and suicidal actions.

In February, Sierra Leone's government established a rehabilitation centre for victims of drug abuse and set up a ministerial task force.

Sierra Leone's neighbours, Guinea and Liberia, are also fighting to contain an increase in kush consumption.

In Liberia, President Joseph Boakai declared drug abuse a public health emergency and announced a committee to tackle the "existential threat", during his first state of the nation address in January.
 
Kuna vijana wanavuta gundi, muda mwingi kichupa cha gundi kipo puani, vijana wameharibika hawajijali na hakuna aliyepiga marufuku kuvuta gundi kama kilevi na haijawekwa kwenye orodha ya dawa za kulevya
 
Back
Top Bottom