Makari hodari
JF-Expert Member
- May 17, 2022
- 3,758
- 7,249
Huku mwisho ulivyomaliza nalazimika kukuuliza bwana… na wewe ni mmiliki wa madaladala?!Nimeenda gengeni leo kununua bidhaa, nilikuwa sina mahitaji ya hivyo ni kitu kidogo tu cha shilingi mia mbili, nimempa muuzaji mia tano lakini ananiambia hana chenji.
Nikaenda magenge mengine kama matatu hali ni hiyohiyo, ikabidi niondoke bila ya kununua ninachohitaji.
Hali pia kwenye usafiri wa umma ndio hivyohivyo, konda hawana chenji ndogo. Wanafunzi wanapata shida pia kwa sababu makonda wanawataka wawe na chenji kamili ili wawapakie, kama hawana wanaachwa na usafiri.
Kama wafanyabiashara ina maana hakuna biashara watakayofanya hasa huku uswahilini kwa sababu wanunuzi bidhaa zao ni mia, hamsini, mia mbili. Ina maana wateja wote ambao watahitaji bidhaa ndogondogo wasihudumiwe na wafanyabiashara wasiuze kwa sababu ya chenji.
Chenji zote zipo kwenye madubu, kwa nini serikali;
1. Isimamishe biashara ya madubu
2. Kama haiwezekani kusimamisha, uwepo utaratibu wa kuwataka wenye madubu kupeleka chenji benki pindi wanapotoa kwenye mashine.
3. Serikali kupitia benki kuu wasizalishe chenji za kutosha ili kuepusha adha kwa wafanyabiashara na wateja.
4. Kama haiwezekani kuzalisha chenji za kutosha, tuhamie kwenye kulipa kwa mtandao, serikali iondoe makato ya kulipa ili kurahisishia wafanyabiashara.
Nimepanda daladala nauli ni mia sita, ila konda ilibidi achukue mia tano kwa kila abiria kwa sababu ya ukosefu wa chenji. Sasa fikiria gari yenye abiria 50 ina maana konda kaacha 5000 kwa safari moja, ina maana huyu konda akienda safari 10 kwa siku ataacha zaidi ya 50000/- kwa siku. Fikiria kwa mwezi ni shilingi ngapi? Utaona pesa nyingi zinapotea na bado hapo boss anataka hesabu, kuna mafuta, service, na bado serikali inataka kodi.
Kuna shida gani mkilipwa shilingi “500” kwa safari kutoka kwa kila raia?! Mbona mnapata pesa nyingi sana kwa siku?! 🤔
Dah aisee! Kumbe akili zenu wamiliki hufananaga na madereva na makonda wenu eeh?! 😀