Uhaba wa Dola nchini: Badala ya kutupiana lawama tutafute mwarobaini. Tuishauri serikali

Nchi ni ya ajabu sana, wakati wengine wanatafuta mbadala wa malipo kwa Dollar bado Mwigulu amekazana kuomba apewe dollar 😲

Dollar zitakuwepo kama tunafanya mauzo makubwa nchi za nje na hasa Amerika na washirika wake, sasa bidhaa zetu nyingi tunanunua China, nchi za kiarabu na India hizo Dollar tunataka za nini?

Mbali ya export vyanzo vingine vya Dollar ni maliasili zetu, Direct Capital Investments, ushuru na mauzo ya visa na vibali.

Dollar zinazokusanywa kwenye vibali kwa mfano, zinaishia wapi kama siyo kwenye safari nchi za nje huku kundi kubwa la viongozi na machawa wakijiidhinishia posho na imprest za kufanya manunuzi ya bidhaa binafsi kwenye mitaa ya Manhattan?.
Kwahiyo hiyo currency ya china ndio tutazipata bila kufanya export?
 
Ingawa swali lako halieleweki .... Nikufahamishe tu kuwa currency ya China kama kuna bidhaa unaagiza China zinapatikana. Hebu jaribu kuwasiliana na benki yetu ya CRDB ...utajifunza kitu.

Sina haja yakwenda CRDB hizo currency huwezi kuzipata kama hu export bidhaa. Hizo yuan za kichina zitakua ni chache. Tukisema tuanze kufanya import zote kwa fedha ya kichina bado tutakua na uhaba. Wachina tunawauzia maparachichi, soya, Mbaazi. Sisi tunanunua mashine, mavazi, tuongeza na mafuta hapo lazima tutakua na uhaba.
 
Chakula chochote kinachonunuliwa kwa kusafirisha nje kinunuliwe kutoka ghala za serikali tena kwa dola. Hivyo serikali itenge fedha ya dharura kununua kutoka kwa wakulima ili all food crop export itoke kwenye maghala ya serikali.
What about perishable farm produce?
E.g. Avocados?
 
Sina haja yakwenda CRDB hizo currency huwezi kuzipata kama hu export bidhaa. Hizo yuan za kichina zitakua ni chache. Tukisema tuanze kufanya import zote kwa fedha ya kichina bado tutakua na uhaba. Wachina tunawauzia maparachichi, soya, Mbaazi. Sisi tunanunua mashine, mavazi, tuongeza na mafuta hapo lazima tutakua na uhaba.
Pesa za kigeni zinapatikana kwa kufanya mauzo ya bidhaa zetu nje ya nchi, kadiri unavyouza sana ndivyo unavyojilimbikizia akiba ya fedha za kigeni. Bado sijaelewa hoja yako ni ipi?
 
Tunavyouza nje ni vichache kuliko matumizi (matumizi ya fedha za kigeni ni makubwa)
 
Pesa za kigeni zinapatikana kwa kufanya mauzo ya bidhaa zetu nje ya nchi, kadiri unavyouza sana ndivyo unavyojilimbikizia akiba ya fedha za kigeni. Bado sijaelewa hoja yako ni ipi?
Nilichokuwa nakueleza ni kwamba solution ya kutatua swala la uhaba wa dolla sio kuachana na dolla na kuanza kutumia yuan au ruble ya kichina. Kwani hata hiyo hifadhi ya yuan ya kichina itakua haitoshelezi kwasababu hatufanyi export ya kutosha yakutuwezesha kuwa na fedha nyingi ya kigeni. Solution ni kuongeza uzalishaji, kuexport kwa sana, kuvutia watalii na wawekezaji wa kigeni au kwenda kukopa kama hatuwezi kufanya hayo mengine. Kwasasa solution ya haraka chukua dhahabu kanunue mafuta, punguza baadhi ya matumizi yasiyo ya lazima ili bajeti isiathiriwe.
 
Umofia kwenu.

Mengi yamesemwa kuhusiana na hili sakata la upungufu wa dola nchini. Kimsingi Dola ya Marekani ndiyo inatumika kama fedha ya kununua bidhaa za kimataifa. Mojawapo ya bidhaa hizo ni pamoja na mafuta ghafi ambayo yanashikilia sehemu muhimu ya mfumuko wa bei nchini.

Nasema yapo mengi yamesemwa na wataalam na sisi wataalam pori wa michongo lakini naona katika yanayozungumzwa mengi ni lawama na kauli ambazo hazitoi mwelekeo wa kukabili changamoto hii. Tukiendelea kulaumiana tutaendelea kuathirika wote na kadhia hii.

Kwa nia njema, ninaleta kwenu Great Thinkers wa JamiiForums kwamba maoni na ushauri kuntu uelekeze namna ya kupita huu mkwamo. Inawezekana hoja zetu zikapuuzwa lakini tutakuwa tumetimiza wajibu wetu muhimu kupitia ibara ya 18 ya Katiba ya JMT (1977 na marekebisho yake).

MAONI

  1. BOT ianzishe hifadhi ya dhahabu haraka ili kukabiliana na tatizo hili, kwani dhahabu inatumika kufanya exchange ya forex kunapotokea nakisi
  2. Serikali itoe sapoti na msukumo kwa bidhaa zote za export hususan zile zilizopo kwenye mfumo wa Fair Trade ili wazalishaji waweze kuexport kwa wingi.
  3. Chakula chochote kinachonunuliwa kwa kusafirisha nje kinunuliwe kutoka ghala za serikali tena kwa dola. Hivyo serikali itenge fedha ya dharura kununua kutoka kwa wakulima ili all food crop export itoke kwenye maghala ya serikali.
  4. Serikali iichunguze kampuni ya forodha ya SILENT OCEAN hususan mwenendo wake wa biashara wa miezi 24 iliyopita kwani imenyooshewa vidole kusafirisga dola nje ya nchi kwa njia haramu.
  5. ............
Weka maoni yako
Mbona matajiri hapa hawalalamiki kuwa hakuna dola
Nyinyi makapuku hata hamna shughuli yeyeto inayohitaji matumizi ya dollar, ndio kutwa kuchwa kupiga ramli na kelele humu...
 
Tuna option ya kupunguza matumizi ili tusitumie zaidi ya kile tunachozalisha.
Ndio, kama:-
  • Kuagiza mafuta machche
  • Kutokununua magari
  • Kuzuia safari zisizo za lazima nje
  • Kutokununua nguo, samani n.k nje, kwa vile vitu vinavyoweza kuzalishwa na wazawa
  • Kuboresha utalii
  • Kuuza madini nje n.k
 
Nilichokuwa nakueleza ni kwamba solution ya kutatua swala la uhaba wa dolla sio kuachana na dolla na kuanza kutumia yuan au ruble ya kichina. Kwani hata hiyo hifadhi ya yuan ya kichina itakua haitoshelezi kwasababu hatufanyi export ya kutosha yakutuwezesha kuwa na fedha nyingi ya kigeni. Solution ni kuongeza uzalishaji, kuexport kwa sana, kuvutia watalii na wawekezaji wa kigeni au kwenda kukopa kama hatuwezi kufanya hayo mengine. Kwasasa solution ya haraka chukua dhahabu kanunue mafuta, punguza baadhi ya matumizi yasiyo ya lazima ili bajeti isiathiriwe.
Suluhisho la muda mfupi ni kukopa au kupata msaada
 
Tukubaliane kwanza kuwa hatua ya kwanza ni kupunguza matumizi na ikiwezekana Dollar zote zilizoko nchini zitumike kwa uangalifu sana tukijua kuwa matumizi ya Dollar katika kufanya malipo kimataifa siku za usoni utakoma.
 
Mbona matajiri hapa hawalalamiki kuwa hakuna dola
Nyinyi makapuku hata hamna shughuli yeyeto inayohitaji matumizi ya dollar, ndio kutwa kuchwa kupiga ramli na kelele humu...
Tajiri umefuata nini kwenye kijiwe cha makapuku?😡

Pita huku🔥🔥🔥
 
Back
Top Bottom