Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Shule za vijijini ni kawaida kukuta darasa lina watoto 120 mwalimu ni mmoja na hapo hilo darasa imebidi ligawanywe kati kati nusu wanakuja asubuhi na nusu wanakuja mchana kwasababu vyumba vya madarasa havitoshi na walimu pia hakuna.
Mapokeo ya watoto ni tofauti, kuna wale wepesi kuelewa, wengine wanapata msaada nyumbani kutoka kwa wazazi au kaka na dada waliowatangulia. Kuna wale ambao wazazi wao pia hawakunufaika na elimu na uwezo wa kuwasaidia watoto wao hawana. Wazazi wengine wana majukumu mengi ya kujenga Taifa muda wa kukaa na watoto wao hawana kabisawau ni mdogo sana. Mwalimu mwenye darasa la watoto 120+ anawezaje kuwapa msaada wa ziada wale waliojiweza au walio nyuma ya viwango!
Unakutana na kijana anashindwa kutumia smart phone kwakua hawezi kusoma na kuandika. Ana simu yake Twanga Pepeta ambayo namba zake za muhimu ziko saved anajua kuminya button ya kijani na nyekundu. Kijana wa aina hii ni rahisi kufanyiwa vitendo vya kiutapeli kwakua hajui dunia inaendaje zaidi ya kusikia habari za kijiweni.
Huko elimu ilikoanzia mwanzo waliitoa kwa watoto wa matajiri tu, mwisho waligundua universe ikijua kusoma na kuandika faida ya biashara zao itakua kubwa, na hata kuielimisha jamii katika maswala ya uchumi, afya na siasa ni rahisi.
Tujiandae kusomea watoto wetu mabango ya mabasi mtu anakwenda Mwenge anayajua mabasi kwa alama. Yakiwa mawili sehemu moja inabidi aulize hata kama kibao cha Mwenge kipo.