Tetesi: Uhakiki: Maprofesa UDSM washindwa kuwasilisha vyeti vya sekondari,wawa wakali


Wivu wa kizamani
 

Ikiwa ni kweli ule usemi kuwa UDSM ni "vipanga" inabidi utazamwe upya!

Waturudishie vil**za wetu tu UDOM wamalize kozi zao! Kumbe hayo maajabu yapo hadi kwa maprof!

Kuna ishara kuwa hawa watu wote wenye PhD waanze kuhakikiwa peke yao popote walipo, then tushuke masters, bachelor's, diplomas na certificates ziwe za mwisho! Tunaweza kuwa na uwiano mzuri wa magumashi ktk kila level ya taaluma!
 
Hapo kwenye vyeti kuna watu watakufa kwa presha.. dah sipati picha.. ama kweli kila zama na nabii wake...
 
kwanini uhakiki. mpe mtihani wa eneo lake akifeli anarudi home akifaulu cheti pembeni....kuna wana vyeti halali lakini hamna kitu pia...

yaan mm nisome kuanzia chekechea mpaka university.

Halaf ww u forge vyeti, utumie cha mdogo wako au cha uncle wako halafu unasema upo sahihi. Ww ni mwizi km wenz wengine. Mnapokonya haki za watu.

Utakuta mtu uliyesoma naye anaitwa Lucas mwenda unakuja kushangaa mnakutana chuo eti anaitwa Peter kisamvu unabaki kushangaa tu.

Km zoez hili liko serious wengi wataimba namba. Tena kweny sector ya afya, elimu, army, police na politicians humo kuna majipu yamevaa kinoma.

Ila sipati picha wanaotumia vyeti vya kuforge hali ikoje kwao hiv ukiangalia life kitaa lilivyogumu duh!
 
Aaa wapi...VC atakuwa kawaweka kwenye notebook yake...na hao wanapelekwa kwa mkuu...!!
 
Hoja yenu haijaeleweka. Ungehoji je, hiyo PhD kaisomea kweli au hapana. Mengine yote ni blabla tu.
 
Mi hata sijui cheti changu cha sekondari kiko wapi!

US mnabeba mabox....Sasa mnahitaji vyeti vya nini? .................US baby.........ila Kama utataka U-DAS au U-DED.......tutakuuliza cheti............
 
Kwanza aliyeanzisha hii mada sijui alikuwa ana maana gani. Ina maana hizo taasisi zilizowapa hizo PhD hazikujali vigezo vyao vya kuingilia? Isitoshe, anajua mfumo wa elimu enzi hizo ulikuwaje hapa Tanzania? Msipende " backward extrapolation" kwa kuwa sifa na vigezo vinabadilika kulingana na wakati. Kwanza hawa watu uwezo wao ulikuwa mkubwa sana kimasomo. Unawajua walimu wa UPE wewe? Unajua uwezo wao?
 
Haya bana...
Unajua hii kitu ni changamoto kubwa sana. Wengi wa wafanyakazi wameingia makazini kwa figisu figisu. Ukisema ukague vyeti......kutakuwa na vilio na kusema meno. Lakini lazima tuanzie somewhere...tujifunze kula kwa jasho. Kama huna cheti basi urudi shule ukitafute.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…