Tetesi: Uhakiki: Maprofesa UDSM washindwa kuwasilisha vyeti vya sekondari,wawa wakali

Tetesi: Uhakiki: Maprofesa UDSM washindwa kuwasilisha vyeti vya sekondari,wawa wakali

Nakuonea huruma YULE Waziri na YULE Naibu Waziri Hahahahahaha Hahahhahahaaa wakitoka huko wakawahiki na hao!!
 
Wakati zoezi la kuhakiki vyeti vya watumishi wa umma nchini likiendelea,kizungumkuti kimejitokeza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Taarifa zitakazo sifa zinadokeza kuwa Maprofesa na Wahadhiri waandamizi wengi wameshindwa kuwasilisha vyeti vyao vya sekondari:kidato cha nne na cha sita.

Taarifa zinaonesha kuwa Wahadhiri hao wametoa hoja,wakiwa wamecharuka, kuwa hawakuajiriwa kwa vyeti vya sekondari. Wamedai kuwa vyeti vyao vya Shahada,Stashahada na Astashahada vinatosha na kutisha. Wahadhiri hao,taarifa zinasema,wamekubaliwa kuhakikiwa kwa vyeti walivyoviwasilisha,bila ya vya sekondari.

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)

Kwa haibu hii, kwa kweli watu watazidi kumlilia Kikwete kwani Magufuli hana mchezo na vihiyo serikalini.
 
Tatizo ni cheti cha form four au kichwani mwake elimu ya profesa anayo maana kama Hana cheti lakini elimu ya kiprofesa ipo tatizo nini

Wengine wanatumia vyeti vya watu wengine mpaka wametusua zamani kulikuwa na shule za wazazi na chache sana private kama sio za taasisi za dini. Kuchamba kwingi kunataka kuibua visivoiburika wangewakaushia manake wengine wameungaunga sana na siku hizi vitu vitaishia mitandaoni, by the way mwisho wake unatabilika kuna watu wataumbuka tu.
 
Hili zoezi linaweza kuwa na utata mwingi tu.Kuna kada linaweza lisifike kabisa.Ni vizuri likaanzia ngazi za chini kabisa.Huwezi kuwa na PhD isijulikane ngazi ya chini.History background ni muhimu kufahamika vizuri,ndiyo maana kuna admission kila ngazi ya elimu.
 
Mbona hata mimi sikumbuki namba yangu? Huu ni utoto sasa.

Sidhani kama kuna tatizo kubwa kwa watu waliosoma hadi miaka ya mwishoni mwa miaka ya 80 au mwanzoni mwa miaka ya 90 tatizo lilianzia katikati ya miaka 90 na kuendelea yaani mpaka sasa ambapo forgery ya vyeti ndipo iliposhamiri
 
lazima wawe wakali sababu miaka yao wengi walisoma kwa kuunga unga and wengine walisoma nje ya nchi bila kuzingatia elimu waliokuwa nayo sekondari! kuna true story ya mtu mmoja sasaivi ni Prof pale SUA but hapo kabla alifika la saba then akaajiriwa shamba boy na mwingereza moja then baadae alimpleka uingereza akaaza course ya certificate akapiga diploma then degree and kwa ufaulu wake alipokuwa masters wamlipaga Phd moja kwa moja! ila kupewa Phd bila kufanya masters sio tatizo,ni kawaida! ila washkaji wake walikuja juu baada ya mshkaji wao baada ya kuishi uigereza kama 8 years karudi ana Phd na wanamkumbuka vyema kwamba kaishia la saba! and alikuwa shamba boy!
so usiwashangae sana na wao ndio wale wale! sema tunawahe
Lengo ni elimu au cheti cha la saba au sekondari, hivi ukisoma kwa ku ungaunga hiyo siyo elimu kwani elimu ni nini
 
Wakati zoezi la kuhakiki vyeti vya watumishi wa umma nchini likiendelea,kizungumkuti kimejitokeza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Taarifa zitakazo sifa zinadokeza kuwa Maprofesa na Wahadhiri waandamizi wengi wameshindwa kuwasilisha vyeti vyao vya sekondari:kidato cha nne na cha sita.

Taarifa zinaonesha kuwa Wahadhiri hao wametoa hoja,wakiwa wamecharuka, kuwa hawakuajiriwa kwa vyeti vya sekondari. Wamedai kuwa vyeti vyao vya Shahada,Stashahada na Astashahada vinatosha na kutisha. Wahadhiri hao,taarifa zinasema,wamekubaliwa kuhakikiwa kwa vyeti walivyoviwasilisha,bila ya vya sekondari.

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)
Kwan lazima utuambie uko Dodoma?
 
Hahaha wakianza na Mbowe ufipa yote inalipuka
 
Wakimaliza huko
Waende kwenye vyama vya Siasa

Kwenye bunge la katiba si ndio wanasiasa wa ccm mlisema kinachotakiwa ni kujua kusoma na kuandika tu!!! Ama hujui kwamba ulikuwa unashabikia ujinga na sasa unajichanganya?
 
Tatizo ni cheti cha form four au kichwani mwake elimu ya profesa anayo maana kama Hana cheti lakini elimu ya kiprofesa ipo tatizo nini
Huyo atakuwa ni fisadi wa elimu. Inawezekana hata huo U professor wake ni fake vile vile.
 
Kumbukumbu zipo shuleni,vyuoni naNECTA,wahakiki wanaweza kupata taarifa za ukweli wa vyeti huko.
 
wasiwasi wangu ni kua hili nalo lije kuishia mikwara tuu,yapo mengi yaliyoanzwa kwa mikwala na sasa imekua ni muhali kuyakumbushia,mfano sukari iliyo kamatwa kugawiwaa buree kwa raia.
 
Wakati zoezi la kuhakiki vyeti vya watumishi wa umma nchini likiendelea,kizungumkuti kimejitokeza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Taarifa zitakazo sifa zinadokeza kuwa Maprofesa na Wahadhiri waandamizi wengi wameshindwa kuwasilisha vyeti vyao vya sekondari:kidato cha nne na cha sita.

Taarifa zinaonesha kuwa Wahadhiri hao wametoa hoja,wakiwa wamecharuka, kuwa hawakuajiriwa kwa vyeti vya sekondari. Wamedai kuwa vyeti vyao vya Shahada,Stashahada na Astashahada vinatosha na kutisha. Wahadhiri hao,taarifa zinasema,wamekubaliwa kuhakikiwa kwa vyeti walivyoviwasilisha,bila ya vya sekondari.

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)
Lete source na limeanza lini hilo zoezi maarufu?
 
Wakisimamisha mishahara yao tu, utawaona wakizagaa nchi nzima kutafuta vyeti vyao. Hata kama hajui kilipo, anashindwa nini kuingia baraza la mitihani kupata uthibitisho wa elimu na majina yake wakati akiwa form 4 na 6.

Wapo wengi walioiba vyeti vya ndugu wakapata ajira, baadaye wakacheza walivyojua kurudisha majina, lakini wengine wameendelea na majina hayo hayo wakati ktk utumishi wapo wengine wenye vyeti vyao. Waambieni walete vyeti! FINITO! Hawataki mwisho wa kupokea mshahara wa serikali.
 
Back
Top Bottom