Tetesi: Uhakiki: Maprofesa UDSM washindwa kuwasilisha vyeti vya sekondari,wawa wakali

Tetesi: Uhakiki: Maprofesa UDSM washindwa kuwasilisha vyeti vya sekondari,wawa wakali

Hii ndio Tanzania, kwa hiyo waachwe kwa vile maprofea?
Wewe ndugu yangu, miaka ni mingi sana, hawa watu wanaweza kuwa wamepoteza vyeti hivyo. Hivi kwa ushabiki wenu mnadhani kuna professor aliye katika chuo cha umma bila kuwa na sifa za form four?
 
Njoo uombe kazi na qualification ya Masters au PhD ulaya uone kama utaombwa cheti cha form four.
 
90% ni seminarists ... wanaogopa nini ?
Wakati zoezi la kuhakiki vyeti vya watumishi wa umma nchini likiendelea,kizungumkuti kimejitokeza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Taarifa zitakazo sifa zinadokeza kuwa Maprofesa na Wahadhiri waandamizi wengi wameshindwa kuwasilisha vyeti vyao vya sekondari:kidato cha nne na cha sita.

Taarifa zinaonesha kuwa Wahadhiri hao wametoa hoja,wakiwa wamecharuka, kuwa hawakuajiriwa kwa vyeti vya sekondari. Wamedai kuwa vyeti vyao vya Shahada,Stashahada na Astashahada vinatosha na kutisha. Wahadhiri hao,taarifa zinasema,wamekubaliwa kuhakikiwa kwa vyeti walivyoviwasilisha,bila ya vya sekondari.

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)
 
Kwani kuwa pro.kubeba cheti cha form four kuna tatizo gani kam hukuforge?.....kama unakataa kuleta cha form four tutaaminije kama uprof.ni wa ukweli?....leteni vyeti vyenu vya form four na la saba.....uprof.ni kuwa smart kama unaona Hamna haja ya kuonesha cheti cha form four....hupaswi kuitwa prof....

Tatizo la wasomi kukosa vyeti vya elimu ya msingi and sekondari lipo kwa watu wengi waliosoma miaka ya nyuma... nilitegemea Mzee Tupatupa angelieleza hili vizuri.

  1. Miaka ya nyuma (pengine hata sasa pia) vyeti vilichelewa sana kufika shuleni baada ya mwanafunzi kumaliza rasmi elimu yake. Hili lilichangiwa na miundombinu mibovu na utendaji wa watumishi wa umma wa kipindi kile.
  2. Wanafunzi wengi waliokuwa wanafaulu na kwenda kusoma hatua inayofuata maeneo mengine walilazimika kuchukuliwa vyeti na wazazi/walezi wao na wengine walivihacha wakitegemea kuvirudia siku za mbele.
  3. Kutokana na hali duni ya utunzaji katika ngazi ya familia na ofisi za shule, vyeti vingi viliharibika au kupotea, kiasi kwamba ilifika wakati matumizi ya "transcripts" kwa mwanafunzi anayetaka kusoma elimu ya juu ikawa kitu cha kawaida.
  4. Hili lilisababishwa na changamoto zilizokuwemo kwenye mfumo wa kuripoti na kupata cheti kipya pale mwanafunzi anapoambiwa cheti halisi kimepotea. Wengi walizoea kwenda NECTA na kuomba "transcript", ambayo ilipatikana kirahisi kutokana na mazingira yaliyokuwepo.
Ni kweli inawezekana wapo waliotumia mwanya wa urahisi wa "transcript" kuendelea na masomo ya juu, lakini kwa jinsi ambavyo elimu ya juu (hasa uzamili, uzamivu, na kuendelea) zinavyotegemea uwezo wa mwanafunzi, nina hakika watu hao walishachujwa siku nyingi.

Yote kwa yote, bado ni muhimu mfumo ukajiridhisha kwa kuhakiki historia ya mhadhiri husika... historia ambayo itaweka wazi kama mhusika alikuwa "victim" wa mazingira ya upatikanaji wa vyeti siku za nyuma au alipita kiujanja ujanja .
 
Ukitaka kuwapata vizuri cheti siyo tija adimission number ya uanafunzi ya shule ya msingi
Dah.. nimesoma primary shule tisa, secondary shule sita na vyuo vikuu vitano 😀😀😀
 
EDUCATION history background itakuwepo tu kwa kila ngazi ya elimu mtu aliyopitia.
 
Wasiogope,ilikuwa ni rahisi kwa ngazi za cheti kitu kama hichi kufanyika.
 
Sijaona "logic" kwenye huu utetezi wako.Ni lazima uonyeshe vyeti vyote kwa nini wafiche.
Sikulaumu, avatar yako inatosha kabisa kujua ni mtu wa aina gani.
Kutokuonyesha cheti sio kuficha, ka mimi sina cheti hicho sio kwa sababu naficha, nilipata one ya single digit ilitakiwa niwe mstari wa mbele kukionyesha ovyo, sikwenda kukichukua kwa sababu mbalimbali, matokeo ya degree yanatosha kabisa kuonyesha kua nipo vizuri academically. Nikimuonyesha mtu vyeti vyangu vya juu alafu akaniomba cha form four hapohapo nafuta applicationyangu, naenda kampuni nyingine, I can't work chini ya watu wanaojali vyeti kuliko kitu kingine.
 
Hueleweki jomba jipange.
 
Upuuzi mtupu. Yaani mfano km mtu alifoji cheti cha f4 lakini digrii ya kwanza kafaulu vizuri, masters katisha, mpaka phd kangara. Tatizo nini? Kilichotakiwa kuangaliwa ni kama nimeajiriwa ktk ngazi ya digrii je kweli ninz digrii? Na uwezo, au weledi wangu ni wa digrii? Sio mambo ya kutafuta vyeti vya f4! Mbona cha dtd seven hakiulizwi? Elimu ys sekondaro ni km elementary au preparatory education. Ambapo huwezi kusoma digrii na ukafaulu bila kuwa na huu msingi. Cheti cha f4 na f6 wangeulizwa wale walioajiriwa katiks level zinazohitaji vyeti hiyo km qualification. Mfano watu wa vyeti na diploma.
 
Huyo atakuwa ni fisadi wa elimu. Inawezekana hata huo U professor wake ni fake vile vile.
Hawa lazima washupaliwe kabisa!!! Wapo wale ambao ktk familia, msjhindi alikuwa mmoja na wakaamua kutumia cheti kimoja familia nzima! Huyu Polisi, Yule Profesa, mwingine nesi, mwingine katibu wa chama, nk. sasa anayekataa kuleta cheti cha f.4 na 6 anataka thibitisha kwamba ni profesa aliyeanzia juu tu!

Unawezaje kusema eti uliajiliwa kwa cheti cha digrii, kwani wameambiwa wanapewa ajira upya kwa cheti cha f.4?
 
Sikulaumu, avatar yako inatosha kabisa kujua ni mtu wa aina gani.
Kutokuonyesha cheti sio kuficha, ka mimi sina cheti hicho sio kwa sababu naficha, nilipata one ya single digit ilitakiwa niwe mstari wa mbele kukionyesha ovyo, sikwenda kukichukua kwa sababu mbalimbali, matokeo ya degree yanatosha kabisa kuonyesha kua nipo vizuri academically. Nikimuonyesha mtu vyeti vyangu vya juu alafu akaniomba cha form four hapohapo nafuta applicationyangu, naenda kampuni nyingine, I can't work chini ya watu wanaojali vyeti kuliko kitu kingine.
Kwani wewe unadhani wanahakiki ili wakupe ajira? au wajue una divisheni gani? NO! Onyesha cheti ili tujue nani fisadi wa elimu. Kujua au kutokujua hilo halituhusu. Kama ulipata yote, hongera lakini bado tunataka cheti.

Mambo ya sikuchukuwa, ulijiunga na chuo gani hicho kisichohitaji original certificates. Kama kilipotea, onyesha taarifa ya usalama. Wapo watu tunawajuwa wana cheti cha familia. kila mmoja anatumia hicho hicho.
 
lazima wawe wakali sababu miaka yao wengi walisoma kwa kuunga unga and wengine walisoma nje ya nchi bila kuzingatia elimu waliokuwa nayo sekondari! kuna true story ya mtu mmoja sasaivi ni Prof pale SUA but hapo kabla alifika la saba then akaajiriwa shamba boy na mwingereza moja then baadae alimpleka uingereza akaaza course ya certificate akapiga diploma then degree and kwa ufaulu wake alipokuwa masters wamlipaga Phd moja kwa moja! ila kupewa Phd bila kufanya masters sio tatizo,ni kawaida! ila washkaji wake walikuja juu baada ya mshkaji wao baada ya kuishi uigereza kama 8 years karudi ana Phd na wanamkumbuka vyema kwamba kaishia la saba! and alikuwa shamba boy!
so usiwashangae sana na wao ndio wale wale! sema tunawahe
Very poor excuses.

Wote tunafahamu kuna namna zaidi ya moja kufika chuo kikuu. Hata kama uliingilia mature entry si unaeleza tu. Lakini kama uliingia kwa cheti cha sekondari cha mtu hiyo ni habari tofauti. Msipindishe mada.
 
Vyeti vya secondary vya nini wakati mtu unayo PhD kutoka Chuo Kikuu kinachotambulika? Utapataje Chuo bila Vyeti vya sekondari?
 
Kuna pahala hekima itumike kiuzito kuliko Sheria. Tukifuata sheria 100% bila kutumia hekima tutajikuta pabaya. Mimi ni conservative na mpenda ukamilifu lkn akili inawakia mtazamo wa kihekima pale sheria inapokosa macho ya mbali.
 
Vyeti vya secondary vya nini wakati mtu unayo PhD kutoka Chuo Kikuu kinachotambulika? Utapataje Chuo bila Vyeti vya sekondari?
Hivyo vya sekondari ulivyotumia ni vyako? Hilo ndo swali la kukuondoa au kubaki. HAtuhitaji kujua elimu yako ya juu ni ipi. tunataka kuona vyeti vya elimu yako.

Baadaye tutaangalia kama elimu yako inaendana na wadhifa wako. Siyo unapewa kuwa mkuu wa chuo kikuu kumbe wewe ndo bwege kuliko wote. Yupo mkurugenzi wa taasisi muhimu sana lakini eti hakuwahi kusoma digrii ya kwanza, ila akarukia ya pili kwa mwaka na PhD kwa miaka 2 tu!

Wale mafisadi wa elimu wa kitabu cha Msemakweli wako wapi?
 
Mkuu, Prof. Ndalichako naye alirushwa na kupelekwa ktk darasa la PhD huko Canada baada ya outstanding performance ktk degree yake ya kwanza.
 
Wakati zoezi la kuhakiki vyeti vya watumishi wa umma nchini likiendelea,kizungumkuti kimejitokeza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Taarifa zitakazo sifa zinadokeza kuwa Maprofesa na Wahadhiri waandamizi wengi wameshindwa kuwasilisha vyeti vyao vya sekondari:kidato cha nne na cha sita.

Taarifa zinaonesha kuwa Wahadhiri hao wametoa hoja,wakiwa wamecharuka, kuwa hawakuajiriwa kwa vyeti vya sekondari. Wamedai kuwa vyeti vyao vya Shahada,Stashahada na Astashahada vinatosha na kutisha. Wahadhiri hao,taarifa zinasema,wamekubaliwa kuhakikiwa kwa vyeti walivyoviwasilisha,bila ya vya sekondari.

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)
Nimecheka kwa dharaaauuu
 
Kwani wewe unadhani wanahakiki ili wakupe ajira? au wajue una divisheni gani? NO! Onyesha cheti ili tujue nani fisadi wa elimu. Kujua au kutokujua hilo halituhusu. Kama ulipata yote, hongera lakini bado tunataka cheti.

Mambo ya sikuchukuwa, ulijiunga na chuo gani hicho kisichohitaji original certificates. Kama kilipotea, onyesha taarifa ya usalama. Wapo watu tunawajuwa wana cheti cha familia. kila mmoja anatumia hicho hicho.

Huyo fisadi wa elimu ndio unamgundua vipi kwa cheti cha form four??
 
Back
Top Bottom